ACHOMOKA NA 5.766,244 ZA SUPA JACKPOT BONUS YA SPORTPESA
Mwanafunzi kutoka chuko kikuu cha Dar-Es-Salaam, Majuto Safari Mwaigunga, wikiendi iliyopita amejishindia jumla ya Sh 5,766,244, kama Supa Jackpot bonus, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 kati ya 17, alizocheza.
Majuto, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu university of Dar-Es-Salaa, alianza kucheza na SportPesa mwezi mmoja uliopita, baada ya kushawishiwa na rafiki yake (hakutaka kumtaja jina) na pia baada ya kuwa anawaona washindi wa Jackpot za SportPesa wakitangazwa mara kwa mara katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter.
‘’Kusema ukweli mimi bado mgeni kwenye hii michezo ya kubashiri. Wakati nimeanza kujifunza kuhusiana na mambo ya kubashiri, utafiti wangu ulionyesha SportPesa ndio kampuni ya ubashiri yenye odds kubwa na pia bonus nono za Jackpot kuliko kampuni yoyote nchini.
Haikuwa rahisi kwa namna ambavyo kila mtu anaona mimi ni mshindi. Nakumbuka wakati ndio nimeanza nina siku kama 20, nilijaribu kuweka ubashiri wangu kwenye Supa Jackpot mara mbili na baada ya kutoambulia chochote nilicheza Mid-Week Jackpot ambapo napo sikufanikiwa kushinda Jackpot wala bonus za Jackpot.
Mara ya tatu nikasema bora niendelee kupambana na Jackpot kubwa, yaani hii Supa Jackpot kwa sababu, Jackpot hii zipo kama tano za viwango tofauti, hivyo ninaweza kucheza hata Jackpot tatu tofauti ma kutegemea matokeo makubwa’’.
Akiongelea mkeka wake huu wa Supa Jackpot ambao umeshinda bonus, Majuto anasema yeye huwa na kawaida ya kufuatilia mikeka ya Supa Jackpot mara nyingi kuanzia Alhamisi, na kisha huchukua kama lisaa limoja kufanya tathmini.
‘’Mimi kwa namna nilivyojipanga mara zote huchukua muda kuzifuatilia timu zilizopo kwenye mkeka wa Supa Jackpot. Nikishaziona na kuhakikisha ndio zenyewe, basi huanza kupekua kwenye google kitu kinaitwa Head-to-Head.
Hapo nitatizama hizi timu zimesha kutana mara ngapi, na matokeo yake yalikuwaje. Kisha hutizama fomu ya timu kwa muda huo. Kwa mfano katika mechi 5 zilizopita matokeo ya timu husika yalikuwaje?
Muda mwingine huwa nachagua timu ambazo zinatoka ligi moja kama zipo kwenye mkeka. Kwa mfano timu za Championship au ligi ya daraja la pili ufaransa, ujerumani, uturuki, uholanzi etc.
Au naweza nikakadiria matokeo kutokana na namna odds za timu husika zilivyowekwa. Nikimaliza hapo, huwa natizama mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana matokeo yalikuwaje na kama wachezaji wa wakati ule mpaka muda wanaenda kukutana ni hao hao au kuna mabadiliko makubwa katika kikosi.
Baada ya kujiridhisha na taarifa nilizoziona kuhusiana na timu zilizowekwa, hufanya maamuzi ya kuweka mkeka na kusubiria matokeo.
‘’Siku ya Jumamosi nilienda Buza kwa dada yangu. Nilipofika huko niliweka bando na kuanza kufuatilia matokeo ya mkeka wa Supa Jackpot nilioweka.
Kwa muda niliokaa kule buza niliweza kufuatilia matokeo ya mechi zote za Jumamosi na Jumapili. Kuna muda wakati natizama, nilikuta nimeshashinda mechi 14 na baada ya nusu nilichungulia tena nikakuta nimepata mechi ya 15.
Nilifurahi sana baada ya kuwa nimeweza kupatia mechi hiyo ya kumi na moja kwani nilijua na mimi nitapata Supa Jackpot bonus kama wenzangu nilivyokuwa nawaona wanatangazwa. Kilichofuata nilipata sms ikinipa hongera kwa kushinda 5.766,244 kama Supa Jackpot bonus’’. Alisema Majuto
Kuhusu atafanyia nini kiasi hichi alichoshinda Majuto anasema yeye kwa sasa yupo mwaka wa tatu hivyo pesa hii itakuwa mtaji kwake wa kuanzia maisha baada ya kumaliza chuo muda si mrefu ujao.
‘’Unajua kwa sasa mimi nipo likizo. Ushindi huu umekuja wakati muafaka, nikiwa na mud awa kutafakari na kutuliza akili juu ya nini nifanye na hii pesa. Kwa haraka haraka huu ndio mtaji wangu wa shuguli nitakayoenda kufanya baada ya kumaliza chuo.
Akitoa neno la pongezi kwa mshindi, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Majuto kwa kufanikiwa kushinda Supa Jackpot bonus na kumtaka aendelee kucheza ili aweze kushinda zaidi.
Nianze kwa kukupongeza kwa ushindi wako wa Supa Jackpot na pia nichukue nafasi hii kuwahamasisha watanzania ambao bado hawataki kuamini SportPesa ndio baba wa Jackpot zote nchini.
Majuto ni ushuhuda mwingine kwenu, ambao kama alivyosema yeye ni mwanafunzi wa chuo na alianza kucheza mwezi mmoja uliopita. Sidhani kama ukicheza Jackpot au mikeka mingine kama ya multibet unakuwa na kikomo cha kushinda.
Ni juhudi yako tu ya kucheza na kutokata tamaa, ukiamini siku yako itafika, basi na wewe mtanzania utafanikiwa. Mechi za Supa Jackpot yetu ya wikii hii zimeshtoka na kiwango cha Supa Jackpot ni 1,093,