skip to Main Content
NBA-PLAYOFFS-INARUDI TENA

NBA-PLAYOFFS-INARUDI TENA

Tunajua wiki hii kuna mechi nyingi za kimataifa lakini kwa kuwa SportPesa ni mdau wa michezo, kikapu ikiwemo, leo tunakuangazia NBA PlayOffs. Hizi ni mechi za Basketball ambazo huchezwa baada ya ligi ya kawaida ya NBA kwisha, ili kumpata mshindi wa Jumla wa kikapu marekani.

Mechi hizi huendeshwa kwa mfumo wa mtoano ambapo timu bora saba hushindania nafasi ya kuwa bingwa wa Marekani kwa msimu husika. Kabla ya kufikia miaka ya 2020s, NBA Play Offs ilikuwa inachezwa kwa kushirikisha timu zote za NBA.

Ingawaje, wahafidhina wa mchezo huu wanatafsiri NBA Playoffs kama shindano la tofauti na ligi ya NBA, wakiamini mfumo unaotumika kwenye shindano la NBA PlayOffs ni wa kipekee, ukihusisha raundi nne zinazokutanisha timu bora saba, zikihusiha upande wa mashariki(Eastern Conference) na upande wa Magharibi (Western Conference)

Kwa msimu huu ligi ya kawaida ya NBA itaisha rasmi Tarehe 9 Mwezi wa 4, 2023, hivyo kutoa nafasi kwa mechi za kufuzu Play Offs. Mechi ya kwanza ya kufuzu itaanza kucheza kuanzia Tarehe 11, Mwezi 4, 2023 ambapo timu inayoshika nafasi ya 7 ya upande wa Mashariki itacheza na timu inayoshika  nafasi ya 8 ya upande wa Mashariki.

Siku hiyo hiyo tena ya Tarehe 11, mechi ya pili ya kufuzu itazikutanisha timu inayoshika nafasi ya 7 upande wa Magharibi itapambana na timu inayoshika nafasi 8 kwa ubora upande wa magharibi.

Mechi ya tatu ya kufuzu Play Offs itapigwa Tarehe 12, Mwezi wa 4, 2023 ambapo timu ya upande wa Mashariki inayoshika nafasi ya 9 kwa ubora, itapambana na timu ya upande wa Mashariki inayoshika nafasi ya 10 kwa ubora.

Ratiba inaendelea na kuonyesha mechi ya nne ya kufuzu Play offs itachezwa Tarehe 12, Mwezi 4, 2023 ambapo timu ya upande wa Magharibi inayoshika nafasi ya 9 itambana na timu inayoshika nafasi ya 10 upande wa Magharibi. Hapa mshindi wa mechi hii kati ya 9 na 10 atacheza na timu iliyofungwa kati ya 7 na 8.

Aprili 14 kutakuwa na mechi ya tano ya kufuzu Play Offs, ambapo timu ya Mashariki iliyopoteza mchezo kati ya 7/8 itakutana na timu iliyoshinda mashariki katika mchezo baina ya 9/10. Mshindi wa mechi hii ataingia moja kwa moja kwenye ranki ya 8 na kufuzu kucheza PlayOffs.

Siku hiyo hiyo ya Tarehe 14, mchezo wa sita wa Play offs utapigwa baina ya timu ya Magharibi iliyofungwa kati ya mchezo wa 7/8 na mshindi wa mechi iliyochezwa ya mshindi wa mechi 9/10. Mshindi wa mechi hii atawekwa kwenye ranki namba nane na kufuzu kwenda PlayOffs.

Baada ya mechi hizo sita, Tarehe 15, Mwezi wa 4, 2023 Mashindano rasmi ya Play Offs yataanza.

Kwa namna mfumo wa NBA PlayOffs ulivyo gatuliwa mechi za nusu fainali za uapnde wa Magharibi na Mashariki yaani East and West Conference utachukua wiki mbili zingine 5. Hapa namaanisha mashindano haya ya Play Offs yatafika mpaka Juni 2023.

Ikumbukwe fainali ya Play offs huchezwa mara nne lakini kama bado hakuna bingwa basi mechi tatu zitaongezwa ili kumpata bingwa.

Tukirudi nyuma kujikumbusha namna msimu wa 2022 ulivyokuwa. Mashindano ya kufuzu Playoffs yalianza Tarehe 16 Mwezi wa 4 na kuisha Juni 16 2022.

Baadhi ya matukio ambayo yameingia kwenye kumbukumbu za msimu uliopita Kwanza hakuna timu ya jiji la Los Angel’s iliyofuzu kucheza mechi za kufuzu PlayOffs.

Pili Timu iliyokuwa na historia ya kufungwa katika msimu uliopita kutoka upande wa Mashariki (Eastern Conference), Pelicans ilifanikiwa kuingia hatua ya kucheza mechi za kufuzu. Mara ya mwisho jambo kama hili kutokea ilikuwa msimu wa Mwaka 2020.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mechi za kufuzu NBA PlayOffs, wachezaji wanne wenye umri wa miaka 22 au pungufu (Anthony Edwards, Ja Morant, Tyrese Maxey na Jordan Poole) walifunga vikapu 30 au zaidi katika baadhi ya michezo waliyocheza.

Utah Jazz imekuwa timu ya 5 katika misimu 10 iliyopita ya PlayOffs, kushinda mechi za kuwania kufuzu, kwa kushinda mechi, ikiwa nyuma kwa pointi nne, zikiwa zimebaki sekunde 40.

Golden State Warriors walifanikiwa kurudi kwenye kuwania kufuzu PlayOffs baada ya kushindwa kupita kuanzia msimu wa 2019.

Namalizia kwa kuweka kumbukumbu sawa timu zilizofanikiwa kushiriki mashindano ya kufuzu PlayOffs kwa msimu uliopita 2022 kutoka upande wa Mashariki (Eastern Conference) ni pamoja na  Miami Heat, Boston Celtics, Milwaukee Bucks, Philadelphia 76ers, Toronto Raptors, Chicago Bulls, Brooklyn Nets, Atlanta Hawks.

Kwa upande wa Magharibi (West Conference) timu zilizofanikiwa kufuzu kwenda kwenye mashindano ya kufuzu Play offs ni Phoenix Suns, Memphis Grizzlies, Golden state Worriors, Dallas Mavericks, Utah Jazz, Denver Nuggets, Minessota Timberwolves, na New orleans Pelican.

Kwa msimu wa mwaka huu timu ambazo tayari zimepata uhakika wa kushiriki mashindano ya kufuzu kucheza PlayOffs kwa Mwaka huu kutoka upande wa Mashariki (Eastern Conference) ni pamoja na Milwaukee Bucks, Boston Celtics na Philladelphia 76ers.

Kwa Upande wa Magharibi (West Conference) timu ambazo zimepata uhakika wa kushiriki ni pamoja na Denver Nuggets. Waliosalia wote bado wanasaka point za kuruhusiwa kuingia kwenye mashindano ya kufuzu.

Ni matumaini yetu kwamba mtafurahia kufuatilia na kubashiria mechi za Playoffs pindi zitakapo anza.

Share this:
Back To Top