Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier LeagueSimba SC vs Yanga SC
  • Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier League 2025/26
  • Waamuzi Waarabu wa Morocco TPLB yathibitisha, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo
  • Viingilio vya mchezo muda mfupi baada ya kutangazwa sold out zimeanza

Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier League. Mshindi wa mchezo wa Mei 3, 2026 ana nafasi kubwa kutwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Wananchi. Kutokana na ukubwa mchezo Waarabu wa Morocco wataamua mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

SOMA HII: Simba SC vs Yanga SC | Taarifa mpya ya majeruhi; Oura, Kibabage na Kagoma, NBC Premier League, Ratiba, Uwanja, matokeo, msimamo na Takwimu | SportPesa Blog

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier League | Utabiri

Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier League
Prince Dube na De Reuck kwenye Kariakoo Dabi.

Kazi inaendela Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC njia ya ubingwa NBC Premier League hii inatokana na tofauti ya alama zilizopo. Bingwa mtetezi anaongoza ligi akiwa na pointi 47. Mnyama ana pointi 42 nafasi ya pili tofauti ya pointi 5. Ikiwa Yanga SC atashinda ataongeza tofauti ya pointi 8 na kama Simba SC itashinda itapunguza deni la pointi 2.

Kuelekea mchezo huo wageni wanapewa nafasi kubwa kupata matokeo. Hii inatokana na kupoteza mchezo uliopita wa Muungano Cup 2026, Uwanja wa New Amaan Complex. Yanga SC haitakubali kupoteza mchezo wa pili mfululizo jambo ambalo hata wenyeji wanatambua.

Rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi tano zilizopita ushindi ulikuwa mali ya Yanga SC. Licha ya rekodi hiyo bado kuna nafasi kwa wenyeji kupata ushindi. Matokeo kamili yatapatikana mara baada ya dakika 90.

Waamuzi Waarabu wa Morocco Mei 3, 2026

Mwamuzi wa Morrocco Hamza El Faruq
Mwamuzi wa Morrocco Hamza El Faruq

Waamuzi kutoka Morocco watakuwa watasimamia Kariakoo Dabi, Mei 3,2026, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo saa 12: 00 jioni. Karim Boimanda Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu ,(TPLB) amethibitisha hilo. Ameongeza kuwa uamuzi umezingatia kanuni za ligi.

“Waamuzi hawakuja kwa pendekezo la klabu kwa sababu kanuni inaruhusu. Kamati inapoona kuna umuhimu inaweza kutumia waamuzi wa ndani au nje kulingana na uamuzi wake,”.

Walioteuliwa ni Hamza El Fareq mwamuzi wa kati akisaidiwa na Lahsen Agaou, Hamza Massiri na Mustapha Kechaf wote kutoka Morocco. Tayari waamuzi hao wapo Dar. Mei 2, 2026 wamefanya mazoezi Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

SOMA HII: Waamuzi Simba SC vs Yanga SC, ‘Dabi ya Kariakoo’ NBC Premier League, Ratiba, matokeo, msimamo na Takwimu | SportPesa Blog

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

H2H Simba SC vs Yanga SC

TareheMashindanoMatokeo
5 Nov 2023Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 1–5 Yanga
20 Apr 2024Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–1 Simba
8 Ago 2024Ngao ya Jamii (Community Shield)Yanga 1–0 Simba
19 Okt 2024Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 0–1 Yanga
25 Jun 2025Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–0 Simba
1 Machi 2026Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 0–0 Simba
29 Apr 2026Kombe la Muungano (Fainali)Simba 1–0 Yanga

Viingilio mechi ya Simba SC vs Yanga SC na sold out mapema

Viingilio vya chini Mzunguko ni Tsh. 15,000, VIP B ni Tsh. 30,000 na VIP A ni Tsh. 50,000. Tayari wenyeji wametangaza sold out kwa mzunguko. VIP B na VIP A bado mashabiki wanaendelea kununua tiketi. Hii inatokana na ukubwa wa mchezo huo wa Kariakoo Dabi.

SOMA HII: Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC | Matokeo, takwimu | SportPesa Blog

Hitimisho

Kariakoo Dabi Simba SC vs Yanga SC ni njia ya ubingwa NBC Premier League ikiwa ni mzunguko wa pili. Matokeo ya mchezo uliopita NBC ilikuwa Yanga SC 0-0 Simba SC. Je mchezo huu nani atakomba pointi tatu uwanjani? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa matokeo na taarifa zaidi.

Share this: