skip to Main Content
SHILINGI MILIONI 11,555,580 ZA JACKPOT YA SPORTPESA ZAENDA TABATA!
Mr-Mremi-MJP-Bonus-winner-

SHILINGI MILIONI 11,555,580 ZA JACKPOT YA SPORTPESA ZAENDA TABATA!

Mkazi wa Tabata Liwiti, Charles Ndechihiko Mremi, wiki iliyopita aliondoka na kitita cha Sh 11,555,580, ikiwa ni bonus ya Jackpot ya baada ya kupatia kwa usahihi mech 12 kati ya mechi 13 alizocheza.

Akizungumza katika ofisi za SportPesa Oysterbay, Dar-Es-Slaam Charles anasema alianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2020, baada ya kuona jina la SportPesa katika jezi za Simba ambapo yeye anasema ni shabiki mkubwa wa timu hiyo.

‘’Mimi nilianza kucheza SportPesa 2020. Katika msimu ule wa mwaka nilikuwa nanunua jezi kila zilivyokuwa zinatoka. Sasa kwa miaka ile Simba ilikuwa vizuri sana na kila nilipokuwa nikinunua jezi nilikuwa nakutana na jina la SportPesa.”

Mr-Mremi-MJP-Bonus-winner-Nilipofuatilia niligundua kumbe hii ni kampuni ya kubashiri na kujua kwa undani wanafanyaje fanyaje kwenye biashara yao’’.

Charles anaendelea kusema wakati ameanza kucheza miaka miwili iliyopita alikuwa anashinda Sh 11,000, laki mbili, laki tatu na nyingine ndogo ndogo, ambazo zilimpa moyo wa kendelea kubashiri kila alipopata nafasi.

Kuhusu mkeka huu wa Jackpot alioshinda, Charles anasema aliziona mechi za Jackpot siku ya Jumatatu na kuweka mkeka wake siku hiyo hiyo, baada ya kupitia timu kwa kuangalia historia ya timu, magoli waliyofunga na pointi walizonazo katika msimamo wa ligi.

‘’Naweza kusema Mungu ni mwema sana kwangu, kwani kwanza, nilishinda mkeka wakati nikiwa ninaumwa na nimetoka hospitali. Charles anasema yeye ana kawaida ya kila Jumatatu na Alhamisi au Ijumaa kuweka mikeka ya Jackpot za SportPesa.

Mimi nina kawaida ya kuweka japo 2000 au 3000 kwenye simu yangu na kisha kucheza Jackpot za SportPesa ambazo moja huchezwa kati kati ya wiki na nyingine mwishoni mwa wiki. Katika mkeka wangu huu ulioshinda niliweka mkeka majira ya saa 6 mchana.

Kikawaida huwa sina muda wa kufuatilia matokeo ya mechi nilizocheza, mpaka mechi zikisha isha ndio nisubiri kuona sms kama nimeshinda au la.

Sasa kwa mkeka huu ilikuja sms ya hongera lakini kwa muda ambao sms inaingia nilikuwa sebuleni kwangu nimepumzika naangalia muvi, baada ya kutoka hospitali. Sikutumia simu yangu kwa muda, lakini sms ya hongera ilikuwa tayari imeshaingia.

Baadae kidogo nilipigiwa simu na mtoa huduma nikiulizwa kama nimeona sms. Kwa kuwa nilikuwa ninaumwa sikutilia maanani na nikajibu sijaona sms wanayoniambia.

Baada ya muda kidogo nilijaribisha kuwasiliana na namba iliyonipigia kwa kufanya kama natuma tigo pesa. Zoezi hilo halikufanikiwa hivyo ikanipa hisia labda ni matapeli wanajaribu kunichezea akili wanipige hela. Nilikumbuka kwamba nina jamaa yangu Juma Pembe.

Mr-Mremi-MJP-Bonus-winner-Juma anashiriki sana kwenye kubeti. nilimwelezea kilichojiri na yeye akashauri tutafute kwenyea mtandao (google) ofisi za SportPesa zilipo kisha tuje.

Ilipotimu asubuhi, Juma alinitumia ramani na nikaifuatisha mpaka kufika hapa. Kwa kweli nimefurahi sana kwa kuwa tangu nimefika nimepokelewa vizuri na kupitishwa katika hatua mbali mbali za uhakiki za kiofisi na sasa nimetoka kukabidhiwa mfano wa hundi wa pesa niliyoshinda’’. Alisema Charles.

Akizungumzia fedha hii ataifanyia nini Charles anasema kitu cha kwanza atafanya ni kufungua na kuwawekea kiasi cha fedha watoto wake wawili ambao bado ni wadogo sana. ‘’Fedha hii nimeipata katika wakati muafaka. Kitu cha kwanza nilichopanga ni kuwafungulia akaunti watoto wangu wawili na kuwawekea milioni nne kila mmoja. Zitakazo salia nitaangalia nifanyie nini”.

Naye mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya amempongeza Charles kwa ushindi wake wa bonus ya Jackpot na kumtaka aendelee kucheza kwani bado Jackpot kila wiki inazidi kuongezeka.

Nachukua fursa hii kukupongeza kwa ushindi wako na pia napenda kukwambia usibweteke kwa sababu umeshinda kiasi hiki cha Sh 11,555,580. Ushindi huu uwe chachu kwako na kwa wengine ambao wamekuzunguka na pia watanzania kwa ujumla ili muweze kubadilisha maisha au kutimiza ndoto zenu. Jackpot ya katikati ya wiki imesismamia Sh 508,027,160 wiki hii.

Akimalizia Charles aliwaasa watanzania kujaribu bahati zao kwa kucheza na SportPesa na pia kutokata tamaa. ‘’Mimi ni mfano kwenu, hivyo na nyinyi mjaribu bahati zenu kama nilivyofanya mimi’’. Alisema Charles.

Kucheza Jackpot bofya hapa.

Share this:
Back To Top