Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC raia wa Mali | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

July 30, 2026
Simba SC ni unbeatenIbrahim DoumbiaIbrahim Doumbia
  • Ni Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC raia wa Mali mwenye umri wa miaka 19.
  • Julai 24,2026 alitambulishwa rasmi kuwa ni mnyama kwa usajili wa miaka miwili akitokea AS Korofina
  • Mfungaji bora wa ligi ya Mali akifunga mabao 17 na asisti 5
  • Ameanza kazi Rwanda kwenye mashindano ya Kagame Cup 2026 chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker

Miamba ya Dar imemuongeza kundini Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC kuelekea 2026/27. Huyu ni raia wa Mali ambaye ana umri wa miaka 19. Anatajwa kuwa na kasi kwenye eneo la wapinzani jambo ambalo limempa nafasi kuwa hapo. Mara baada ya kutambulishwa unyamani alijiunga na kikosi kambini Rwanda kwa maandalizi ya msimu mpya.

Matokeo ya Simba SC Rwanda: Simba SC 0-0 Jamus SC, Kagame Cup hali ni tete | Wachezaji wapya kazini | Lineups

Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator game banner featuring a red biplane and the message ‘Kamata hadi TZS 800,000,000 kwa raundi.’

Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC takwimu zake

Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC
Doumbia Ibrahim mshambuliaji mpya Simba SC.

Mkakati wa usajili Simba SC: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog

Nyota huyu Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC takwimu zake zinaonyesha ni hodari katika kufunga. Kwa umri wa miaka 19 ni mshambuliaji kijana ambaye ana nafasi katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20. Hii inadhirisha kwamba ni kipaji halisi.

Akiwa ndani ya Klabu ya AS Korofina ya Mali aliibuka kuwa mfungaji bora. Jumla alifunga mabao 17 na asisti 5.Mshindani wake wa karibu katika ligi kuu ya Mali alikuwa ni Ibrahim Traore wa FC Diarra ambaye alimaliza msimu akiwa amefunga mabao 14. Kutokana na kasi ya kufumania nyavu inatajwa kuwavutia Simba SC ambao wamempa kandarasi ya miaka miwili.

Katika michuano yote akiwa katika timu ya taifa ya Mali chini ya miaka 20 amefunga mabao 22 baada ya mechi 26. Ni miongoni mwa wachezaji bora nchini Mali amekuwa akitajwa kuwa amejenga ufalme wake kwenye eneo la ushambuliaji.

Hatari kubwa ya Doumbia ipo kwenye eneo hili

Mshambuliaji Doumbia hatari kubwa ipo kwenye mipira ile yakutengwa hasa kona na faulo. Ni mjanja kwenye kukaa kwenye nafasi akilitizama lango na kufunga hasa kwa mapigo ya vichwa. Magoli mengi ambayo amefunga ni kwa mtindo huo.

Hivyo mabeki watakuwa na jukumu lakulinda mshambuliaji huyu hasa inapotokea mipira yakutengwa. Akiwa ndani ya 18 ni mwenye hatari zaidi kufunga kuliko nje ya 18. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia katika kumalizia hatari. Mchezo wake wa kwanza ndani ya ushindani unatarajiwa kuwa Simba Day na ule wa pili Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC Agosti 12,2026 Uwanja wa Uhuru.

Ameanza kazi chini ya Steve Barker Rwanda

Kikosi cha Simba SC kimeweka kambi nchini Rwanda chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker. Mchezaji huyu yupo kambini akiendelea na maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Kwenye mashindano ya Kagame Cup 2026 mnyama akiwa kundi B naye amekuwa akipata nafasi katika mechi za ushindani.

Ni mechi mbili Simba SC imecheza mpaka sasa huku yeye akipata nafasi akitokea benchi. Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Jamus SC aliingia akitokea benchi. Mechi zote mbili Simba SC haijapata matokeo ubao ukisoma 0-0.

Neno la Doumbia

Mshambuliaji huyo kupitia mahojiano maalumu na Simba SC amesema kuwa anaamini watakuwa imara kadri mazoezi yanavyoendelea. Mchezaji huyo aliongeza kuwa maisha mapya yamekuwa na furaha kutokana na mapokezi ambayo amepata kutoka kwa wachezaji wenzake.

Hitimisho

Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC katika changamoto kubwa. Msimu uliopita 2025/26 kiongozi safu ya ushambuliaji alikuwa ni Seleman Mwalimu aliyefunga mabao 9. Kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo akarejea Wydad Casablanca kutokana na mvutano uliopo. Kazi kubwa itakuwa kwa Doumbia kuongoza safu ya ushambuliaji Msimbazi kuelekea msimu mpya 2026/27.

Share this: