Multibet-Multibet-

UKISIKIA ZALI NDIO HILI

Wasawahili wana msemo, mgaagaa na upwa hali wali mkavu, hivi ndivyo msemo huo ulivyojidhiirisha kwa mkazi wa Ngúruhe, wilaya ya Mkoa wa Iringa ambaye amejishindia kitita cha Sh 15, 203,640 za Multibet ya SportPesa, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 ambazo alicheza alfajiri ya Jumamosi ya Tarehe 25-Februari-2023.

Akizungumza katika ofisi za SportPesa baada ya uhakiki na makabidhiano ya mfano wa hundi Rajab anasema alianza kucheza na SportPesa miaka mitatu iliyopita baada ya kuwa anaona kwenye magazeti ya michezo na kurasa mitandao ya kijamii.

‘’Mimi nilianza kucheza 2020 ambapo nikiwa mtaani kwangu nilikuwa naona habari za SportPesa kupitia magazeti ya michezo. Pia siku nyingine nilikuwa naona washindi kupitia kurasa za mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram na Youtube, kwenye simu za rafiki zangu’’.

Multibet-Akiendelea Rajab anasema hakuanza kucheza papo hapo ila alichukua muda kwa sababu hakupata mtu ambaye alimuelekeza kwa wakati ule alipoona namba za SMS kujiunga kwa kuwa yeye anatumia simu ya kitochi.

‘’Unajua mimi napenda kusoma magazeti ya michezo ya Tanzania. Sasa kuna siku moja nimeona piga *150*87# nikaiandika pembeni na kuikariri. Changamoto ikawa sina mtu wa kunielekeza zaidi, hivyo sikuendelea na hatua zilizofuata za kujisajili na kucheza.

Siku moja nilipata safari ya Dodoma na nilipofika huko katika shughuli zangu za hapa na pale nilikutana na mzee mmoja (jina kapuni) ambaye yeye alikuwa anabashiri kwa kutumia simu ya kiswaswadu kama yangu.

Nilipomuuliza anielekeza mzee yule hakusita kunifundisha na kuanzia muda ule nilianza kujaribu kucheza na nikaweza. Tangu nimeanza kucheza nimeshawahi kushinda vihela vidogo vidogo kama 2000, 3000, 4000 na kiwango kikubwa kuliko vyote nilivyowahi kushinda ni 20,000’’. Alisema Rajabu.

Kuhusu ni namna gani ameweza kushinda pesa hii ya Multi bet katika mechi nyingi anasema aliweka mkeka wake siku ya ambapo aliweka mkeka huu siku ya Jumamosi ,Tarehe 25 mwezi wa February 2023 mida ya saa 12:02 Alfajiri, ambapo aliweka jumla ya timu 15.

Multibet-‘’Mimi ninachokumbuka siku hiyo niliamka asubuhi sana wakati najiandaa Kwenda shamba nilikuwa nimeandaa timu za kuweka mkeka tangu siku ya Alhamisi. Ilipotimu Jumamosi alfajiri niliweka mkeka na kisha kuendelea na ratiba zangu za shambani ambapo huwa nasimamia banda la mifugo”.

Kwenye akaunti yangu ya SportPesa nilikuwa na Sh 300 tu na ndiyo niliyotumia kuweka mkeka huu ulioshinda. Niliweka mechi mchanganyiko za Tanzania, kombe la klabu bingwa Africa na za ulaya.

Kwa ufupi nilicheza mechi ya Azam VS KMC, Everton VS Aston Villa, Leicester VS Arsenal, West Ham VS Nottingham, AS Vita VS JS Kabylie, Costal Union VS Tanzania Prisons kwa uchache tu.

Akizungumza kwa niaba ya SportPesa mkuu wa kitengo cha mawasiliano Sabrina Msuya alimpongeza mshindi kwa ushindi wake adhimu na kuwataka watanzania kutumia fursa zinazopatikana SportPesa ili kuboresha Maisha yao.

‘’Nianze kwa kukupongeza Rajabu kwa kuibuka na kitita kinono cha Milioni kumi na tano na ushehe, lakini pia nichukue nafasi hii kuwaasa watanzania kuendelea kuiamini SportPesa kwani ina njia nyingi zinazoweza kumfanya mteja kushinda.

Mteja wetu Rajabu aliweka Sh 300 kwenye mkeka wake wa mechi 15 na katika mkeka huu ulioshinda Odds zake zilikuwa 50,000 na ushehe. Ukizidisha  unapata kiasi alichoshinda cha zaidi ya Milioni 15.

Kwa hiyo baada ya kodi ambayo amelipa TRA Sh 1,520,334, Rajabu amebakiwa na Sh 13,683,306 kama faida yake ya moja kwa moja’’ Alisema Sabrina.

Nimalizie tu kwa kuwaasa Watanzania kujisajili na kucheza nasi kupitia Sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

Share this: