skip to Main Content
MKULIMA KALIUA ALAMBA 10,681,562 JACKPOT BONUS YA SPORTPESA
Mshindi Jackpot Bonus Peter Andrew Dotto akishikilia mfano wa hundi ya Tzs 10,681,562 baada ya kushinda bonus ya SportPesa Jackpot.

MKULIMA KALIUA ALAMBA 10,681,562 JACKPOT BONUS YA SPORTPESA

Mkulima wa mpunga, kutoka wilaya ya Kaliua, Tabora Peter Andrew Dotto, ameshinda Sh 10,681,562, katika Jackpot Bonus ya Sportpesa ya katikati ya wiki, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi ofisi za Sportpesa, Dar-Es-Salaam, Peter anasema alianza kucheza na Sportpesa mwaka 2019

‘’Nilianza kucheza na Sportpesa miaka mitatu iliyopita baada ya kaka yangu mkubwa ambaye ni wa kwanza kushinda Sh 600,000 wakati huo ilikuwa ni mwezi wa kumi na mbili na kimaisha kwa wakati ule tulikuwa tunapitia kipindi kigumu sana.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Peter anasema tangu ameanza kucheza na Sportpesa au tangu alipofundishwa na kaka yake kucheza amewahi kushinda mara tatu kabla ya ushindi huu na hiyo ilikuwa mwaka 2020.

‘’Nafikiri ilikuwa bahati yangu kwa wakati ule ambapo nilishinda Sh 100,000, Sh70,000 na Sh 190,000 kwenye hizi multibet’’.

Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki, Peter anasema kwanza yeye hana tabia ya kucheza kila siku au mara kwa mara, pili siku akiamua kucheza huwa anaweka mikeka si chini ya saba.

 “Sijui kwa wengine lakini kwangu mimi sina kawaida ya kucheza kila siku ila uwa nikitaka kucheza huwa najitahidi nichambue na kuweka japo mikeka ambayo haipungui saba. Ujue kabla sijashinda mkeka huu wiki moja nyuma niliweka mikeka kama 7 na mmoja wapo ulipata mechi 9.

Rafiki yangu wa karibu naye aliweka mkeka kama mimi lakini yeye alishinda Jackpot bonus na kupata Sh 300,000. Kitendo kile kilinitia hamasa ya kwa nini safari ijayo isiwe yangu. Nilichambua mikeka kwa umakini mkubwa na matokeo yake ndio unayaona haya nimeshinda Sh 10,681,562’’.

Anaendelea kusema mkeka huu alioshinda aliuchambua kwa takriban siku 2 baada ya kuziona mechi za Jackpot siku ya Jumatatu. ‘’Kama nilivyosema hapo awali mkeka huu niliupitia kwa umakini mkubwa na ninaamini ndoto zangu za kwanza katika kushinda Jackpot za Sportpesa imeanza kutimia.

Akiongelea ni namna gani atatumia pesa hii aliyoshinda Peter alisema atawekeza kiasi kikubwa cha pesa katika kuboresha biashara yake ya kilimo na nyingine kwenye ujenzi.

‘’Kwa bahati nzuri hii pesa niliyoshinda imekuja wakati muafaka ambapo nilikuwa nimejenga nyumba na ipo kwenye linta hivyo nitatumia sehemu ya pesa kuendeleza ujenzi’’.

Akimpongeza mshindi, Meneja Uhusiano na Mawsasiliano wa SportPesa Sabrina Msuya alimtaka kuendelea kucheza na Sportpesa na pia kuwafundisha wengine ambao bado wanasita kujisajili na Sportpesa ili na wao washinde kama yeye.

‘’Nikupongeze Peter kwa ushindi wako na pia nikutake ukawe mfano mzuri kwa watanzania wengine, hasa hasa kwenye jamii unayotoka. Najua bado kuna watu ambao bado hawajafanya maamuzi ya kujiunga na kucheza.

Kwa kuwa wewe unatokea Tabora basi jitahidi uwahamasishe na wengine ili wajisajili na kucheza na Sportpesa ili na wao washinde kama wewe’’. Alimalizia Sabrina.

Share this:
Back To Top