BODA BODA KONGWA ALAMBA Sh 7,887,966 JACKPOT BONUS YA SPORTPESA
Mkazi wa Chamahe, wilaya ya Kongwa, Dodoma Yosiah Ndoloji Ngubesi, ameshinda Sh 7,887,966, katika Supa Jackpot Bonus ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 14 kati ya mechi 17.
Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam,Yosiah anasema alianza kucheza na Sportpesa miaka mitatu iliyopita.
‘’Nilianza kucheza na Sportpesa mwaka 2019 baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari unaweza kushinda kupitia bashiri za michezo’’.
Kwa mujibu wa maelezo yake Yosiah ambaye pia ni dereva wa boda boda alivutiwa na Sportpesa, baada ya kuona kiwango cha bonasi za Sportpesa ni kikubwa kuliko makampuni mengine.
‘’Mimi kiasili ni mpenda soka, kwa maana ya kwamba mimi mwenyewe nacheza mpira pale kwangu na pia nafuatilia sana ligi mbali mbali za mpira ulimwenguni, nilipopata habari kuna mchezo ambao unaweza pata pesa na unahusiana na michezo ya mpira nilifarijika na kuanza kufuatilia.
Kwa kifupi nina jamaa yangu kwa majina anaitwa Samwel, yeye alitangulia kuanza kucheza michezo ya kubashiri kabla yangu. Kaka Samwel alinipa maelekezo ya namna ya kucheza kwa kutumia simu ya vitochi, ambayo ndiyo niliyoshinda nayo hii bonus.
Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Supa Jackpot bonus anasema aliweka mkeka mmoja tu siku ya Alhamisi jioni na alifuatilia matokeo kuanzia Jumamosi na Jumapili mpaka pale mechi ya mwisho ilipomaliza kucheza.
‘’Huwa nina kawaida ya kuweka wastani wa mikeka mitatu mpaka minne kila Jackpot zinapotoka. Sasa kwa mkeka huu ulioshinda niliweka mkeka mmoja tu. Bahati iliyotokea ambayo nayo naona ni kama kudra za mungu ni kwamba siku zote nikiweka mikeka 3 au 4 huwa napata wastani wa timu 7 mpaka 9.
Kwa huu mmoja mpaka zikiwa zimebaki timu tatu nilikuwa nimeshinda mechi 11 nasubiria mechi ya Vizela vs Boavista ili nipate japo bonus ya mechi 12 ambayo nayo niliipata. Baada ya mechi ya 12 nilisubiria mechi ya mwisho ambayo ilikuwa Nice vs Lorient ambayo mimi niliweka droo.
Hiyo ndiyo ilikuwa mechi ya 14 kati kati ya mechi 17 za Supa Jackpot. Nilipoona nimepata mechi 14 nilifurahi sana na hivyo kuamua Kwenda dukani na kujipooza na soda moja baridi sana kama sehemu ya kufurahia bonus.
Yosiah anawapa ushauri watanzania wasisite kuchukua fursa ya kujaribu bahati zao kwani ushindi hauna mwenyewe. Nichukue nafasi hii kuwataka watanzania wenzangu sio tu wale ambo tayari wanabashiri, bali hata wale ambao hawajaanza kubashiri wajisajili na Sportpesa na wao wajaribu bahati zao’’. Alisema Yosiah.
Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kama mtaji kwenye biashara yake ya boda boda na kiasi kingine ataangalia cha kufanya hapo baadae.
Akimpongeza Yosiah, Meneja uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa Sabrina Msuya amemtaka kuendelea kucheza na kuwa mfano bora kwa wengine na pia kuwaomba watanzania wengine kujisajili kuweka pesa na kucheza kwani ushindi hauchagui.
‘’Nikupe hongera Yosiah kwa ushindi huu wa bonus na pia nikuombe ukawe balozi mwema kwa wenzako kwani wewe ni ushuhuda tosha. Kwa watanzania waliopo majumbani, makazini, mashambani na wanaowajibika katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu, msiache kuchukua fursa hii, kwani hakuna anayejua bahati yake itaangukia wapi’’. Alisema Sabrina.