skip to Main Content
Ni Supa Jackpot Ya Bilioni Moja Kwa 1000.
Z A

Ni Supa Jackpot Ya Bilioni Moja kwa 1000.

Cheza sasa kwa 1000 ushinde Bilioni 1 na SportPesa.

Jackpot mbili kila wiki za SportPesa!.

Dar es Salaam. 26 Mei ,2022. KAMPUNI ya Michezo na Burudani SportPesa leo imezindua rasmi Jackpot mpya inayoitwa Supa Jackpot kama moja ya huduma yao nyingine kwa wachezaji wake.

Akizungumza ofisini kwake, Oysterbay, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas alisema leo ni siku nyingine ambayo kampuni ya Sportpesa inatambulisha huduma hiyo.

Z A‘’Najua bado watu wanashauku na Jackpot yetu ambayo imeliwa siku si nyingi zilizopita, kwa muktadha huo baada ya kuona wachezaji wetu wameanza kuzoea viwango vikubwa basi tumeonelea tuwaletee bidhaa ambayo inaendana na matamanio yao. Kwa hivyo tunazindua rasmi leo Jackpot hii ambayo itaanzia bilioni moja na itaenda kwa jina la SUPA JACKPOT’’.

Akiendelea Tarimba anasema Supa Jackpot itakuwa na jumla ya timu 17 na pia kiwango cha pesa ambacho mchezaji atatakiwa kuweka ni Tsh 1000 ili aweze kucheza.

Lakini upekee wa Jackpot hii upo kama ifuatavyo. Jackpot imegawanyika katika makundi au vipengele vitano vya zawadi ambavyo vyote mchezaji anachaguo la kushiriki na kushinda.

Kipengele namba moja ni cha timu 17 ambacho ukishinda unaondoka na kuanzia bilioni 1 kutegemeana na Jackpot imesimamia kiasi gani. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 16 mpaka 12.

Kundi la pili au Kipengele namba 2 ni cha timu 16 ambacho ukipatia mechi zote unashinda kuanzia Tshs milioni 750. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 15 mpaka mechi 11.

Kundi la tatu au kipengele namba tatu ni cha timu 15 ambacho ukipatia mechi zote kwa usahihi unashinda kuanzia Tshs milioni 500. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia mechi 14 mpaka mechi 10

Kipengele cha nne cha Supa Jackpot ni cha timu 14 ambacho ukipatia mechi zote kwa usahihi utashinda kuanzia Tshs milioni 300. Kipengele hiki bonasi zake zinaanzia timu 13 mpaka timu 10

Na kipengele cha mwisho hichi ni kipengele ambacho kimezoeleka kila siku ni cha timu 13 ambacho ukipatia kwa usahihi unashinda kuanzia Tsh mil 200

Cha ziada ambacho ni mabadiliko kidogo ni kwenye kombinesheni. Kama mtakumbuka Jackpot iliyoliwa ilikuwa unaweza kucheza dabo kombinesheni 7, kwenye hii kombinesheni zimeongezeka mpaka timu 10.

‘’Tumewaletea Jackpot hii ili wale wote wenye ndoto za kuwa mabilionea basi wapate nafasi ya kushinda kama ahadi yetu tuliyoweka hapo awali kuwawezesha watanzania na kutengeneza mabilionea wapya kupitia mchezo wa ubashiri’’. Na pia Jackot hii ina viwango tofauti vya zawadi kama ilivyoainishwa hapo juu.

Kuanzia leo tutakuwa na jumla ya Jackpot mbili kila wiki moja ni ile ambayo ilikuwapo awali inayoanzia milioni 200 ambayo kwa wiki hii ni 222,883,040 na itakuwa inachezwa kwa dau la Tsh 1000 kila siku za Jumatano na Alhamisi na hii mpya ya Supa Jackpot ambayo itakuwa na jumla ya timu 17, itakuwa inachezwa siku ya Jumamosi na Jumapili na dau lake ni Tsh 1000’’.

Anamalizia kwa kusema dhamira kuu ya Sportpesa ni kuendelea kuwapa kile ambacho ni bora na chenye manufaa kwa wachezaji wake pamoja na jamii nzima ikiwemo serikali hasa kwenye maswala ya kodi.

‘’Nachukua fursa hii kuwahamasisha watanzania mchangamkie fursa hizi kwani mmeona washindi wote waliopita akiwepo bilionea mpya Florian Masawe namna walivyotimiza ndoto zao na Sportpesa za kuwa mamilionea na bilionea hapa nchini.

Kama bado haujajisajili na Sportpesa au una akaunti na umesahau nywila wasiliana na kitengo chetu cha huduma kwa wateja au tembelea www.sportpesa.co.tz ……………Mwisho

Share this:
Back To Top