skip to Main Content
Mwongozo Wa Timu – Manchester United
manchester-united

Mwongozo wa timu – Manchester United

Manchester United bila shaka ni timu bora na inatambulika kama klabu ya mpira wa miguu inayojulikana zaidi duniani. Tembelea mbali katika kona ya sayari hii utakuwa na uwezo wa kumuona mtu kavaa jezi ya United, wanaweza kuwa wanapata shida kuonyesha Manchester ilipo kwenye ramani ya dunia.

Timu ina hitoria ya aina yake. Imenyanyua mataji mengi zaidi kuliko timu yoyote katika Ligi Kuu ya England, na mafanikio yake pia yameifanya kuwa klabu yenye thamani kubwa nchini England – na moja kati ya tatu zenye thamani kubwa zaidi duniani. Sehemu kubwa ya mafanikio yake yamekuja kwa nyakati mbili chini ya makocha ambao walikuwa na staili tofauti kutoka moja kwenda nyingine. Lakini wote waliiongoza Manchester United kwenye mafanikio ya kuvutia. Majina yao yalikuwa ni Matt Busy na Alex Ferguson.

Kwa kipindi cha miaka, United imekua sumaku kwa wachezaji bora sana duniani. Kama ilivyo kwa timu ya Ferrari katika mashindano ya Formula 1, kuna kitu fulani kuhusu kuwa sehemu ya timu nyekundu na kila mchezaji mkubwa kuwa sehemu ya historia. Bado kumekuwa na nyakati za kupinda, na hata majanga ambayo bado United inakubali makovu yake. Hapa tutaangalia kwa kina wakati tunapozama kwenye kila kitu utakachotaka kujua kuhusu Mashetani Wekundu.

Siku za Mwanzo

Iliundwa mwaka 1878 kama klabu ya mpira wa miguu ya Newton Heath Lancashire and Yorkshire Railway, awali timu hiyo ilikuwa ikicheza dhidi ya timu nyingine za kampuni ya reli. Mchezo wao wa kwanza wa mashindano ulifanyika Novemba mwaka 1880 na ilikuwa dhidi ya Bolton Wanderers Reserves. Na haukuwa mwanzo chanya, ambapo vijana kutoka Manchester walifungwa mabao 6-0. Waliendelea, hata hivyo mwaka 1892 walikuwa sehemu ya ligi mpya ya soka iliyoundwa.

Mwaka 1902, ulikuwa rahisi mno kwa kipindi chao chote. Klabu ilikabikiwa na wakati mgumu kwenye ligi daraja la pili na walikuwa na matatizo makubwa ya kifedha. Nahodha wa klabu Harry Stafford alimpata mfanyabiashara mzawa ambaye alikuwa tayari kuwekeza na nia ya mpango wa kuiendesha moja kwa moja. Lakini kulikuwa na sharti  la kubadilisha jina, hivyo klabu ya soka ya Newton Heath Lancashire and Yorkshire Railway Football ikawa Manchester United.

Mafanikio hayakuja haraka kwa kubadilisha jina, lakini hayakuwa mbali, na muwekezaji mpya alileta kila kilichohitajika na kuwa klabu ya kulipwa. Mwaka 1906 wakafuzu kwenye Ligi Daraja la Kwanza na mwaka 1908, walishinda ligi kwa mara ya kwanza. Taji jingine la ligi na FA yaliongezwa kabla ya kila kitu kusimama kutokana na vita kubwa ya mwaka 1914. Lakini kwa wakati huo, Manchester United ilishajiimarisha yenyewe kama klabu bora ya soka Uingereza.

Busby na Ferguson – makocha wawili

Kiukweli kuielewa Manchester United, unahitaji kuelewa vipindi viwili vikuu kwenye historia yao, na kila moja ilichangiwa na kocha wa timu wa wakati huo. Kwanza kwa miaka ilikuja haraka baada ya vita ya pili ya dunia. Raia wa Scotland, Sir Matt Busby alikuwa mchezai mwenye mafanikio kwa njia yake, akicheza zaidi ya mechi 300 kwa  wapinzani wa United Manchester City na Liverpool miaka ya 1930. Alifanya kazi kama kocha wa mpira wa miguu wakati wa miaka ya vita, na akateuliwa kuwa kocha  pale United wakati uchezaji wake ulipofika mwisho.

Busby alikuwa kocha kwenye zama mpya. Alitawala kwa kutengeneza ukurasa mpya kwa kusajili wachezaji, uchaguzi wa timu na mazoezi kitu ambacho hakikuwepo wakati huo. Busby aliitengeneza timu ya vijana na yenye wachezaji wenye vipaji. Waliichukua timu kwenye levo nyingine mpya za mafanikio, wakishinda mara kadhaa mataji ya FA, Kombe la Dunia mfululizo, pamoja na kuwa timu ya kwanza ya soka ya Uingereza kuunda mashindano ya Ulaya. Timu ikanasa hisia ya jamii na vyombo vya habari. Ambao waliitwa kama “Busby Babes” (Watoto wa Busby) kutokana na kujaa vijana.

Busby alikaa hapo kwa robo karne, na wakati alipojiweka pembeni kutoka katika klabu hiyo mwaka 1971, ilichukuliwa kwamba United kamwe haitapata mafanikio tena. Kama ilivyokuwa, wakaenda mbali kusubiri mafanikio kwa miaka 15 kabla ya nyakati nyingine zilipowadia chini ya kocha mwingine wa Scotland, Sir Alex Ferguson.

Wakati Ferguson alipotua hapo mwaka 1986, United ilikuwa klabu ambayo ipo safarini, hatarini kukaribia eneo la kushuka daraja ambapo kwa wakati huo ilikuwa inaitwa Ligi Daraja la Kwanza. Misimu kadhaa ya mwanzo chini ya Ferguson kidogo ilikuwa bora, wakimaliza katikati ya msimamo na hiyo ikawafanya kupoteza kiti chao. Lakini mafanikio Ulaya yakawafanya kurudi kutwaa taji mwaka 1993 – likiwa la kwanza tangu miaka ya Busby – pamoja na kurudi kwenye mataji ya ligi. Mwishoni mwa miaka ya 90, kasi ya Manchester United ilikuwa haizuiliki, na kulikuwa na swali ni taji gani lilillokosekana kwenye kabati pale Old Trafford.

Timu ilifanikiwa kwa mara ya kwanza – lakini haikuw a mara ya mwisho – wakashinda mataji mawili mwaka 1996 na mwaka 2004, wakashika kwa kuweko rekodi ya kutwaa mataji 11 ya FA. Wakati Ferguson alipotangaza kustaafu mwishoni mwa msimu wa mwaka 2013, ilikuwa ni baada ya United kutwaa taji la 20 la Ligi Kuu katika historia ya klabu hiyo. Inamaanisha kwamba kwa kipindi cha robo karne akiwa pale, United ilishinda jumla ya mataji 38. Hayo yakiwemo 13 ya Ligi Kuu, matano ya FA, na mara mbili taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ni mafanikio ambayo hakuna kocha ameyakaribia.

Janga la Munich

Busby na Ferguson – kati yao, wawili hao waliongoza United kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne na sehemu kubwa ya kupindi kati ya vita ya pili ya dunia na sasa. Hayo ni mafanikio makubwa na inaonyesha namna gani ustahimilivu unaweza kuwa na mafanikio kwenye mpira wa miguu. Bila shaka, hata wakati wa mafanikio kwa makocha hawa, haukuwa muda wote mzuri. Ferguson alikabiliwa na vimbuka kadhaa vya utata, kutoka kwenye kupigania kutoshuka daraja na kuishutumu UEFA na kugombana na David Beckham kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Lakini hivyo vilikuwa ni kama vimbuka kwenye kikombe cha chai ikilinganishwa na tukio la kutisha lililowatokea vijana wa Busby mwaka 1958.

Mnamo Februari 6, timu ilikuwa inarudi nyumbani baada ya kushinda kwenye robo fainali ya kombe la Ulaya dhidi ya Red Star Belgrade. Pamoja na wachezaji kulikuwa na kundi la waandishi wa habari ambao waliongozana kwa ajili ya mchezo huo, pamoja na benchi la ufundi na mashabiki. Kiujumla walikuwa watu 44 kwenye ndege, ambayo ilisimama Munich kwa ajili ya kuweka mafuta.

Hali mbaya ya hewa ikawafanya kushindwa kuruka mara mbili, na kukatokea majadala mkubwa wa mabishano kama watatakiwa kujaribu kuruka mara ya tatu au kubakia Munich kwa usiku wote kusubiri hali ya hewa kuimarika. Rubani na msaidizi wake wakakubaliana kujaribu mara moja zaidi, na matokeo yake yalikuwa moja ya janga kubwa zaidi katika historia ya michezo.

Ndege ilishindwa kupaa kwa kasi na ikachepuka kwenye njia yake ya kurukia, kwenda kukonga nyuma na kulipuka moto. Ilikuwa ni miujiza watu waliokuwa kwenye nyumba sita zilizogongwa walitoka bila kujeruhiwa, lakini abiria 23 kati ya 44 waliokuwa ndani ya ndege walipoteza maisha usiku ule.

Janga hilo kamwe halijawahi kusahauliwa, na kumewekwa orodha ya majina ya wote waliofariki. Bado kwa kuongezea hilo, janga hilo la Munich lilimaliza timu ya United ambayo haikuwa imefungwa katika mechi 11, timu ambayo ilikuwa inaelekea kubeba taji lake la tatu mfululizo la ligi, na tayari walikuwa na FA na Ngao ya Hisani na ilifuzu kucheza nusu fainali ya Kombe la Ulaya.

Ghafla, wachezaji nane na watu watatu wa benchi la ufundi walifariki, na wengine waliumia vibaya. Kiukweli ni wachezaji wawili tu kati yao ndio waliopona kwenye ajali hiyo na kuwa fiti kucheza tena. Matt Busby mwenyewe alilazwa kwa miezi miwili.

Kulikuwa na mazungumzo kwenye vyombo vya habari  kwamba, Manchester United ingepotea baada ya janga hilo. Bado Busby aliendelea licha ya kushauriwa kustaafu na mkewe, alirudi kufanya kazi msimu uliofuata. Akarudia mafanikio yake aliyokuwa nayo mwaka 1945 na kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10, kizazi kipya cha watoto wa Busby kiliundwa.

Wachezaji alama

Mchango wa Busby na Ferguson kwenye mafanikio ya United unaelezeka. Hata hivyo, hawakwenda wenyewe katikati ya uwanja na kushinda mechi. Kama tulivyotaja huku nyuma, Old Trafford mara zote imekuwa sumaku kwa wachezaji wakubwa, na hii ndio timu iliyoweka heshima ya usajili wakati madirisha ya usajili yanapofunguliwa. Ni kitu ambacho tunaweza kuzungumza kwa urahisi kwa siku nzima, lakini ngoja tuangalie majina makubwa yaliyonogesha.

  • Sir Bobby Charlton – akiwa na umri wa miaka 20 wakati huo, Charlton alikuwa mmoja wa waliobahatika kwenye ajali ya Munich, akiondoka na majeraha madogo. Alikwenda kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kwa timu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka 15 iliyofuata, akifunga mabao 199 na mechi zaidi ya 600. Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha England kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1966. Charlton alikuwa mtu ambaye pamoja na Matt Busby, waliisaidia Manchester United kuchomoza kwenye mafanikio.
  • George Best – jina la “mwenye akili” ni moja kati ya uliyoyasikia mara kwa mara, lakini limetokea kwenye kamusi, na kutokea picha ya George Best. Kama maisha yake, kipindi chake cha uchezaji kilichomoza kwa muda mfupi lakini chenye kung’aa – alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 27 na alifariki katika umri wa miaka 60. Bado alikuwa na miaka 10 pale United, na kwa kipindi cha miaka hiyo alicheza mechi 500. Kama kijana, alikimbia kwenye ulingo wa Benfica kuisaidia United kutawala Ulaya.
  • Bryan Robson – ni kitu kimoja tu kwa nyota kugeuka na kufunga mabao kwa timu inayotawala. Lakini kama Charlton na Best, Robson aliwasili Old Trafford wakati wa nyakati ngumu mwanzoni mwa miaka ya 80. Alichangia mafaniko yaliyohitajika, akifunga mabao kutoka sehemu tofauti na alikuwa muhimili wa klabu wakti ilipokuwa inamhitaji. Leo hii anapendwa na mashabiki waaminifu wa Old Trafford kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita.
  • Ryan Giggs – Ukizungumzia uimara, bado mashabiki wa United wanapata wakati mgumu kuweka orodha ya wachezaji bora bila kumuweka Ryan Giggs. Alikuja kutokea timu ya vijana na alianza kucheza timu ya wakubwa akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 1991 na alicheza mechi yake ya mwisho mwaka 2013 muda mfupi baada ya kutimiza umri wa miaka 41. Giggs alikuwa pale kwa kipindi chote cha zama za Ferguson, na ametwaa mataji mengi zaidi kwa timu katika historia yake. Kuna yeyote atakayefikia rekodi yake ya kucheza mechi 963?
  • Eric Cantona – Kitu fulani kuhusu mchezaji anachoweza kufanya, lakini anafanyaje. Siku hii, ni ngumu kumuelezea Cantona, na kumfanya kuwa anayependwa zaidi na mashabiki mwanzoni mwa miaka 90, bado utaendelea kusikia jina lake likiimbwa kwenye majukwaa ikiwa ni zaidi ya robo karne tangu aondoke.

Kuna majina mengi unaweza kuyataja, kutoka Denis Law hadi David Beckham na kutoka Wayne Rooney hadi Cristiano Ronaldo, lakini watano wa hapo juu walisaidia kuunda taswira halisi ya Manchester United. Labda wengine wanaweza kujiuliza kwa nini, hata wakati huu timu haitawali soka, kuna mashabiki wanawasapoti kwa hali na mali Mashetani Wekundu hao. Tunajua walifanya hivyo kabla, watanyanyuka tena, na mashabiki watiifu watakuwa pale nyuma yao wakati wakifanya hivyo.

 

Share this:
Back To Top