skip to Main Content
SportPesa Yaizawadia Simba SC Milioni 100!
X A

SportPesa yaizawadia Simba SC Milioni 100!

Kampuni ya michezo na burudani SportPesa leo imewazawadia milioni 100 klabu ya Simba baada ya kushinda mashindano ya ligi kuu Tanzania bara.

Simba wamejizolea fedha hizo kwa miaka minne mfululizo tangu kusign mkataba wa SportPesa kuwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo mwaka 2017.

Bonus ya 100M Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 100 Mkurugenzi wa Simba Sports Club Barbra Gonzalez, wachezaji wa Simba SC wakiwa katikati Beno Kakolanya na Gadiel Michael ikiwa kama bonasi ya timu kwa kuchukua ubingwa na ligi kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Tarimba Abbas alisema:

“Tukiwa kama wadhamini wakuu wa klabu ya Simba, kwa niaba ya SportPesa ningependa kuwapongeza sana sana kwanza kwa kuibuka mabingwa na ligi kuu Tanzania bara, pili kwa kuibuka washindi wa kombe la ASFC.”

“Hii inatupa faraja sana kuona matunda ya SportPesa kwa klabu ya Simba tukiangalia miaka minne iliyopita tangu kuingia mkataba nao rasmi”

“Klabu ya Simba kwa miaka minne mfululizo wamekuwa wakitwaa ubingwa wa ligi kuu na kupelekea kujipatia bonasi ya shilingi milioni 100 kwa mara nne tangu tuingie mkataba nao”

“Tunapenda kuwapa moyo na waendelee na juhudi hizi kwani ukiongelea Simba ni lazima utataja SportPesa nadhani wote tunalifahamu hilo. Msimu mwingine unakwenda kuanza hivyo basi tunatarajia mambo makubwa zaidi na kuona ushindi ili wazidi kuitangaza SportPesa hata nje ya nchi.”

“Na hivi sasa tupo katika mazungumzo mazuri na Simba katika kuongeza mkataba mpya baada ya huu wa awali kumalizika, mwaka huu,”alisema Tarimba.

Akipokea hundi hiyo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema kuwa anaipongeza SportPesa kwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo katika mkataba waliongia nao kwa kipindi cha miaka minne.

Tarimba na Barbra wakishikilia kombe la VPL

Mkurugenzi wa Simba SC Barbra Gonzalez akimkabidhi kombe la ligi kuu Tanzania bara Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas leo.

SportPesa wanastaili pongezi kwa kufanikiwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo katika mkataba ikiwemo sehemu ya bonasi.

SportPesa walianza kutupa bonasi ya Sh 50Mil baada ya kufanikiwa kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hii ni mara ya pili kwao kutupa Sh 100Mil za ubingwa wa ligi.

Kwa niaba wa wachezaji, beki wa Simba Gadier Michael alisema kuwa “Tuchukue nafasi hii kwa kuwashukuru SportPesa kwa udhamini ambao wamekuwa wakitupa unatupa morali, hivyo tuahidi kuendelea kupambana kwa ajili ya kuwatangaza SportPesa kimataifa.

Mwisho

 

 

 

Share this:
Back To Top