skip to Main Content
Muongozo Wa Timu – Liverpool FC
liverpool-stadium

Muongozo wa timu – Liverpool FC

LIVERPOOL FC ni timu ya kwanza kuanzishwa uingereza. Klabu hiyo yenye maskani yake Anfield limekuwa moja ya nembo ya soka la Uingereza kwa kipindi cha miaka 130 iliyopita, na imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi mara 19, rekodi ambayo imevunjwa na Manchester United pekee. Bado barani Ulaya Liverpool imekuwa na nyakati za kuvutia. Mataji 14 ya Liverpool ya Ulaya,yakiwemo sita ya Ulaya yamekuwa mafaniko makubwa kwa timu ya Uingereza.

Kwa miaka, Liverpool imekuwa na nyakati za kuvutia kwa mechi zake – zote kwenye uongozi na sapoti. Lakini nyakati nzuri zimechanganywa na wakati mgumu wa kutokuwa na mafanikio na hata majanga. Habari ya Liverpool FC ni moja ambayo imejazwa na vitu vingi vyenye mipaka kwa jiji lenyewe, hebu tuangalie.

Siku za mwazo

Inajulikana wazi kwamba Liverpool ina makazi yake Uwanja wa Anfield, kaskazini mashariki mwa Liverpool, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1892. Kitu ambacho hakitambuliki ni kwamba, Anfield kulikuwa nyumbani kwa timu nyingine maarufu zaidi ya Liverpool, Everton. Kiukweli ni baada ya timu ya klabu ya Everton kuparaganyika chini ya John Houlding, mmiliki wa Anfield, ndio Liverpool FC ilipozaliwa.

Everton wakabadilisha sehemu yao na kwenda Goodison Park, ni dakika 10 kutembea kwa miguu, hivyo Houlding akaanzisha timu ya wachezaji wake. Klabu ikaja kujulikana kama Liverpool FC na kuanzia siku hiyo, alama ya klabu iliyoaanzishwa, lakini ilikuwa moja ya timu ya mpira wa miguu pinzani zaidi katika jiji hilo.

Liverpool haraka ikapata mafakio kwenye ligi ya nyumbani ya Lancashire, shukrani kwa mikakati ya Houlding ya kutafuta wachezaji nchini Scotland na kuwasajili. Kiukweli msimu wa kwanza, lilikuwa ni jambo la kawaida kuona wachezaji wote wana asili ya Scotland. Wote wanaofikiri kuchukuwa wachezaji nje badala ya kuwaendeleza wazawa ni tatizo kwenye soka la kisasa na kwamba haikutakiwa kutokea kwenye soka la zamani, wanatakiwa kufikiria tena!

Mwaka 1893, Liverpool iliingia kwenye ligi ya soka, ikipata mafanikio ya kupanda kwenye ligi kubwa mwaka 1896. Moja ya mataji 19 ya ligi lilikuja mwaka 1901, na ‘Wekundu’ hao walishinda tena mwaka 1906. Sehemu ambayo miongoni mwa timu kubwa za Uingereza zimejidhatiti, na kiku ambacho hawajawahi kukikatia tama hadi leo.

Masta wa Ulaya

Liverpool ni moja ya timu “kubwa sita” kwenye Ligi Kuu ya England, na moja kati ya tano ambazo hazijawahi kushuka daraja kutoka kwenye Ligi Kuu – nne nyingine ni Manchester United, Chelsea, Tottenham na Arsenal. Licha ya rekodi ya nyumbani ambazo klabu nyingi zitakuwa zinaziota, Wekundu hao kamwe hawajaweza kufikia mafanikio ya wapinzani wao wakubwa, Manchester United kwenye ligi ya nyumbani. Badala yake imekuwa shujaa Ulaya na Liverpool ni moja ya timu yenye mafanikuio makubwa.

Kushinda taji la ligi kwa mara ya sita mwaka 1964 kuliwapa Liverpool FC tiketi ya kwanza kwenye soka la Ulaya, wakifuzu kucheza Ligi ya Ulaya mwaka 1965. Mchezo wao wa kwanza ulikuwa dhidi ya Knattspyrnufélag Reykjavíkur, na Wekundu hao walishinda kwa uwiano wa mabao 11-1. Na ikawafanya wafuzu kucheza nusu fainali kabla ya kupoteza kwa staili ya aina yake kwa kufungwa kwa uwiano wa mabao 4-3 mbele ya waliokuja kuwa mabingwa Inter.

Mwezi mmoja baadaye, walifika fainali yao ya kwanza ya Kombe la Washindi la UEFA. Wakati huu walipoteza kwa Borussia Dortmund hadi muda wa ziada, lakini ilionekana kwamba taji la kwanza la Ulaya kwa Liverpool lilikuwa linakaribia.

Muda ulivyosonga, Wekundu hao walitakiwa kusubiri kwa miaka nane kabla na hatimaye kushinda taji la Ulaya mwaka 1973. Lakini mara taji la Ulaya lilipokuja, mvua ya mfanikio ikanyesha Anfield, kwa mataji sita zaidi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi ya Ulaya na Super Cup kwa miaka kadhaa.

Tangu kuingia kwa milenium mpya, Liverpool imeongeza mataji zaidi ya Ulaya. Bado inaweza kuwa rahisi kwao kuongeza zaidi, ambapo sio kipindi ambacho walichoondolewa kwenye Ligi ya Ulaya kati ya mwaka 1984 na 1991. Ikifuatiwa na wakati wa giza zaidi kwa historia ya Liverpool FC, na tutazungumza kuhusu hayo.

Mipango iliyoachwa

Kila klabu ya michezo ambayo inakusanya watu ambao wamekuwepo kwa karne kadhaa, watakuwa wana uzoefu wa kushuhuhudia wakati wa majanga katika miaka hiyo. Kwa Liverpool, unaielezea kwa siku mbili za giza, ambayo ni chini ya miaka minne.

Mara ya kwanza walidondoka Mei 29, mwaka 1985, na ilikuwa siku ya fainali ya Kombe la Ulaya mwaka 1985. Liverpool walikuwa mabingwa watetezi na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda taji dhidi ya Juventus. Uwanja wa Heysel nchini UBelgiji ulitoa taswira ya aina yake kabla ya mchezo. Pia kuliwa na swali juu ya kuwaachia mashabiki wa soka wa Ubelgji jukwaani.

Hofu hiyo ilithibitishwa. Haraka sehemu ya mashabiki wa nyumbani ikajazwa na mashabiki wa Juventus kabla ya mchezo kuanza, mashabiki pinzani walitengwa na nyaya tu, ambapo walikuwa wanasukumana kila wakati. Wakati mchezo ukikaribia kuanza, kundi la mashabiki wa Liverpool wakabadilisha sehemu na kwenda kule kwa mashabiki wa nyumbani na wakafanya vurugu zilizosababisha ukuta kudondoka, na matokeo yake watu 39 walikufa na 600 kujeruhiwa. Cha ajabu mchezo uliendelea, kulikuwa na hofu kwamba mchezo ungesitishwa kungekuwa na fujo zaidi. Hata hivyo, Juventus walishinda kwa bao 1-0 na timu iliyofanya vurugu ilionekana wazi.

Miaka mine baadaye, Liverpool FC ikajikuta yenyewe kwenye majanga zaidi. Ikiikabili Nottingham Forest kwenye nusu fainali FA pale uwanja wa Hillsborough mjini Sheffield, umati wa mashabiki wa Liverpool wakavunja fensi. Wachezaji walijaribu kuwasaidia mashabiki waliokwama kwenye fensi. Janga hilo liligharimu maisha ya watu 98.

Matukio hayo yote yameacha makovu, lakini muhinu ni kuelewa kwamba kuna nyakati nzuri zilikuja kutoka kwao pia. Majanga hayo ndio yaliyosababisha kuangaliwa upya kwa usalama wa viwanja. Na tukio la Hillsborough ndilo lililomaliza wakati wa mashabiki kusimama uwanjani na badala yake vikatengenezwa viti vya kukaa.

Liverpool FC Wachezaji

Iwe nyumbani kwenye ligi au Ulaya, Liverpool FC ina habari ya mafanikio tu, shukrani kwa watu walioizunguka. Kwa zaidi ya miaka, baadhi ya magwiji wa soka wamepaita nyumbani pale Anfield. Ni ngumu kuwataja wote, lakini ngoja tujaribu kuyaelezea majina ya wale walioupenedezesha mchezo huu kwa miaka.

  • Kevin Keegan – Hakuna mtu anayefikia mwenye morali ya straika huyo wa Wekundu hao kwa miaka. Alisajiliwa akiwa na umri wa miaka 21 akitoea Scunthorpe, alifanya mambo ya kufurahisha, akifunga kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nottingham Forest. Hilo lilikuwa moja ya mabao yake 100 kwa Liverpool, na alikuwa nguzo ya timu kutwaa mataji matatu ya ligi, mawili ya UEFA, na moja la FA na la Ulaya kwa kipindi cha miaka sita hapo Anfield.
  • Ian Rush – Huku Keegan akiwa ameondoka na kukawa na ukame wa mataji, vyombo vya habari vilikuwa vinanoa visu vyao mwaka 1980, na vilkagundua usajili wa kinda kutoka Wales. Katika msimu wake wa kwanza alitumika akicheza timu ya akiba, lakini wakati nafasi ilipokuja, hakuangalia nyuma. Rush alikuwa mchezaji wa aina yake, akifunga kwa kufurahia kwa kipindi cha miaka sita. Hata aliposajiliwa Juventus, alirudi Anfield kwa mkopo na kufunga mabao mengine 30 kwa Wekundu hao!
  • John Barnes – Barnes alijiunga na Liverpool mwaka 1987, wakati timu ilikuwa na wakati mgumu nje ya dimba. Hata hivyo, ujio wake ulibadilisha safu ya ushambuliaji ya Liverpool kutoka kuwa ya kawadia hadi ya hatari na iliyoogopewa. Ujuzi wake wa soka na hata alipoumia kulikuwa na pengo lake na wakati alipoathiriwa na maumivu ya kisigino kocha Graeme Souness akamhamisha kwenda kiungo mchezeshaji.
  • Mo Salah – Mara zote sio ishu kuangalia kurasa za historia, wakati mwingine nyakati zote nzuri zipo mbele ya macho yetu. Salah alijiunga na Liverpool mwaka 2017 na alifunga mabao 44 katika msimu wake wa kwanza – akipitwa mabao matatu tu na rekodi iliyowekwa na Ian Rush ya kufunga mabao mengi kwa msimu mmoja mwaka 1980. Wakati Liverpool ilipomaliza utawala wa kutwaa taji la Ligi Kuu wa Manchester Ciy mwaka 2020, ni sawa kusema kwamba, Salah alikuwa tofauti kati ya timu hizo mbili. Salah bado ana miaka 28 na ana miaka bora zaidi inaweza kuwa mbele yake.
  • Steven Garrard – Siku hizi wachezaji wanakuja na wanaondoka, hivyo ni wazi kwamba Salah anaweza kujikuta akiwa njiani kwenda Tottenham au PSG au Juventus haraka au baadaye. Kamwe yeye ni tofauti na mchezaji kama Steven Gerrard, mmoja wa wachezaji bora zaidi wa klabu – akimalizika soka lake LA Galaxy na baadaye likizo ya kustaafu. Gerrard alizaliwa Whiston, kijiji ambacho si zaidi ya dakika 15 kuendesha kutoka Anfield. Alijiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 18 na alibakia hapo kwa miaka 17 na kucheza mechi 710. Alifunga mabao 186, lakini muhimu zaidi, amekuwa akifunga mabao wakati ambao yanahitajika zaidi, ikiwemo fainali ya Ligi ya Europa mwaka 2001, maajabu ya Istanbul mwaka 2005 na fainali ya Kombe la FA mwaka 2006, ukitaja kwa uchache.
  • Kenny Dalglish – kwa wote walipita kabla, kama shabiki muaminifu wa Liverpool akiulizwa kutaja jina la tu ambaye anajumlisha yote hayo kwa timu yao, atakuwa ni Kenny Dalglish. Kama ilivyo kwa wengine kwa karne ya 19, anatoka Scotland, na wakati alipofunga kwa mpira wa kumvisha kanzu golikipa wa Bruges, Birger Jensen kwenye fainali ya Ligi Daraja la Kwanza mwaka 1978, ndio wakati alipotengeneza urafiki mkubwa na mashabiki. Alikuwa katikati ya muhimili wa safu ya ushambuliaji ya Liverpool kwa miaka 13, na kwa miaka mingine mitano alikuwa kocha mchezaji. Katika zaidi ya mechi 500, alifunga mabao 169, lakini idadi hiyo inakuambia sehemu tu ya habari yake. Huyu ndio alikuwa mtu ambaye alikuwa kila kitu kuhusu klabu na watu wanaomzunguka, na ndiye aliyehudhuria mazishi mengi katika janga la Hillsborough. Ni gwiji wa aina yake wa Anfield.

Kuna majina machache ambayo yamechangia, yote katikati na kwa njia nyingine, kuifanya Liverpool FC kuwa taasisi ya aina yake kama ilivyo leo. Na uwepo wa wachezaji kama Salah, Virgil van Dijk na Sadio Mané, majaliwa ya baadaye yanaonekana kuwa kwenye mikono salama.

Bado kuna majina mengi makubwa ambayo yangeweza kutajwa. Kutoka Billy Liddell kabla ya miaka ya vita hadi Fernando Torres miaka ya 2000, na kutoka Michael Owen pale mbele hadi Ray Clemence golini, orodha inaendelea.

Liverpool ni timu ambayo ilizaliwa kwa ugumu, na ni moja ya timu ambayo imeshinda sehemu mbalimbali kwa miongo, imetengeneza morali na timu yenye maadili katika klabu za Ligi Kuu na duniani, na inaelezea kiwango cha ukweli kwa klabu ya mpira wa miguu.

Share this:
Back To Top