- Mchezaji wa mpira wa miguu raia wa Tanzania, Feisal Salum kinara wa ufungaji NBC Premier League 2025/26
- Rekodi za Mei ndani ya ligi ni nzuri akifunga magoli 8 na tuzo 3 za Man of the Match
- SportPesa Blog tumekuletea takwimu za kiungo wa Azam FC ndani ya Ligi Kuu Bara
Anaitwa Feisal Salum kinara wa ufungaji magoli NBC Premier League 2025/26. Mchezo uliopita wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 3-0 KMC FC, Fei Toto alifunga magoli 2 akifikisha magoli 14. Ana umri wa miaka 28 ameletwa duniani Januari 11, 1998. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga SC amesema; “Sishindani na mtu kwenye suala la ufungaji magoli,”.
SOMA HII: Feisal Salum ‘Feitoto’ ashtua! tetesi za usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Feisal Salum kinara wa ufungaji magoli NBC Premier League 2025/26

SOMA HII: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Ndani ya Azam FC, Feisal Salum ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Florent Ibenge ambaye ameongeza mkataba mpaka 2028. Uwezo wake sio kufunga pekee bali hata kutengeneza asisti akiwa nazo 8. Hiyo inamfanya kuwa mchezaji muhimu akihusika kwenye jumla ya magoli 22 .
Baada ya mechi 25, Azam FC imefunga jumla ya magoli 38 inashikilia nafasi ya 3 kwenye msimamo kiwa na pointi 52. Kiungo huyo alitwaa tuzo ya Man of the Match mchezo uliopita dhidi ya KMC Complex. Amevunja rekodi aliyoandika 2024/25 kwenye upande wakufunga magoli alipofunga 4, kazi ipo kwenye asisti alitoa jumla ya 13, je nayo ataivunja bado mechi 5? Endelea kufuatilia SportPesa Blog.
Takwimu za Feisal Salum Mwezi Mei 2026 (NBC Premier League)
| Kipengele | Takwimu |
|---|---|
| Mechi | 6 |
| Magoli | 8 |
| Man of the Match | 3 |
Takwimu za Feisal Salum – NBC Premier League 2025/26

| Kipengele | Takwimu |
|---|---|
| Magoli | 14 |
| Asisti | 8 |
| Michango ya Magoli (Magoli + Asisti) | 22 |
| Magoli Ndani ya Eneo la 18 | 12 |
| Magoli Nje ya Eneo la 18 | 2 |
| Magoli ya Penati | 3 |
Maeneo hatari kwa Feisal Salum 2025/26
| Aina ya Magoli | Idadi |
|---|---|
| Ndani ya 18 | 12 |
| Nje ya 18 | 2 |
| Jumla ya Magoli | 14 |
Hitimisho
Kiungo Feisal Salum ni miongoni mwa wazawa wenye uwezo mkubwa katika kutimiza majukumu ndani ya uwanja. Ubora wake umekuwa ukiimarika kila wakati. Mwendelezo wake ulifanya atajwe kuwa kwenye tetesi za mabosi wa Simba SC na Yanga SC na mwisho akaongeza mkataba Azam FC.

