Polisi Tanzania vs Yanga SC: NBC Premier League, Live Score, Matokeo, Ratiba, h2h, Habari za timu
- Mtihani wa kwanza kwa kocha Fadlu Davis utakuwa kesho Alhamisi kwenye ratiba ya mechi ya Polisi Tanzania vs Yanga SC.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
- Polisi Tanzania wanaingia katika mchezo huu wakiwa nafasi ya 6 na pointi zao 15, huku Yanga SC wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 25. Mara ya mwisho timu hizi kukutana matokeo yalikuwa Yanga 7-1 Polisi Tanzania kwenye mashindano ya CRDB Federation.
- Fuatilia matokeo ya mchezo huu live kupitia SportPesa Score.
Mechi kali itapigwa kesho Alhamisi kwenye ratiba ya Polisi Tanzania vs Yanga SC, ambao unatarajiwa kuwa mtihani wa kwanza wa kocha mpya, Fadlu Davis. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Polisi Tanzania wanaingia katika mchezo huu wakiwa nafasi ya 6 na pointi zao 15, huku Yanga SC wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 25.
SOMA HII PIA: Polisi Tanzania vs Yanga SC | Azam FC vs Singida Black Stars | NBC Premier 20/11/2026
Weka mkeka wako kwenye mechi hii ya Polisi Tanzania vs Yanga SC kupitia Odds zilizoboreshwa za SportPesa ushinde pesa nyingi kwa kugusa hapa chini

Habari za timu na majeraha

Kocha mpya wa Yanga SC, Fadlu Davis anatarajiwa kuwa na mtihani wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC atakapovaana na Polisi Tanzania huku sehemu kubwa ya mastaa wake wakiwa wamepona. Ukiachana na, Zouzoua Pacome ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, ni kiungo Duke Abuya pekee ndiye alikuwa na majeraha na tayari ameanza mazoezi. Polisi Tanzania hawajatoa taarifa ya kukosekana kwa nyota wao wowote, hivyo taarifa ya ujumla inasubiriwa muda mchache kaba ya mchezo kuanza.
SOMA HII PIA: Ratiba na Matokeo ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27 | SportPesa Blog
Polisi Tanzania vs Yanga SC, takwimu za head-to-head (h2h)

Historia inaonyesha kuwa Yanga SC wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Polisi Tanzania katika michezo iliyopita. Katika mikutano 9 waliyokutana Yanga SC wameonyesha ubora wao kwa kupata ushindi mnono, ambapo wameshinda mechi zote 6. Mechi 3 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare, huku Polisi wakiwa hawajawahi kupata ushindi kwa Yanga SC. Katika michezo hiyo Yanga SC wamefunga mabao 21 na mashujaa wakifunga mabao 7 pekee.
Je, unataka Mamilioni ya SportPesa? Shinda mpaka Milioni 800, cheza kindege sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi, kwa kubonyeza picha hapo chini.

Alichosema kocha wa Yanga SC

Akizungumzia maandalizi yao, kocha wa mipira ya kutenga wa Yanga SC, Kagisho Dikgacoi amesema: “Tunaamini timu ipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania. Tulifanya maandalizi mazuri kupitia kambi yetu ya Zanzibar, ambapo wachezaji wameonesha mwitikio mzuri kwa kocha mpya na mbinu mpya za kiufundi tunazoanza kuzifanyia kazi. Pia, wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa wameungana na kikosi kuanzia jana.
“Mchezo dhidi ya Polisi Tanzania hautakuwa rahisi. Wametoka kupata ushindi dhidi ya Kagera, hivyo watakuwa na hamasa kubwa ya kutupa ushindani. Tunafahamu Polisi Tanzania ni timu yenye nguvu na inayocheza kwa ushindani mkubwa. Lakini naamini wachezaji wetu wapo tayari, wanafahamu jukumu lililo mbele yao na umuhimu wa kupata alama zote tatu ili kupunguza tofauti ya pointi kati yetu na wapinzani wetu.”
SOMA HII PIA: Yanga SC 3-1 KVZ Mchezo wa Kirafiki Zanzibar | Highlights | SportPesa Blog
Hitimisho
Mchezo wa Polisi Tanzania vs Yanga SC unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika NBC Premier League, hasa kufuatia ujio wa kocha mpya wa Yanga SC, Fadlu Davis ambaye amewahi kuhudumu Simba SC. Wengi wanatamani kuona ikiwa mbinu zake zitairudisha Yanga SC katika ubora wa kiwango chao. Endelea kufuatilia SportPesa blog kwa uchambuzi zaidi na taarifa za mchezo huu wa Polisi Tanzania vs Yanga SC na michezo mingine.

