
Ratiba na Matokeo ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27 | SportPesa Blog
- Kwenye ratiba na matokeo ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27 wamepoteza mchezo mmoja pekee kati ya 10.
- Simba SC 2-1 Yanga SC,10/10/2026 ni matokeo ya mchezo waliopoteza uliopigwa Uwanja wa Uhuru.
- Mechi kali zinafuata ikiwemo Polisi Tanzania vs Yanga SC, Mbeya City vs Yanga SC na Yanga SC vs Azam FC.
Hapa tumekuletea ratiba na matokeo ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27. Mashabiki wengi wanatamani kujua ratiba kamili ya timu yao, matokeo ya mechi zilizopita, na msimamo wao katika ligi. Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina wa safari ya Yanga SC katika msimu wa 2026/27.Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini.
Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 unaendelea ukiwa na ushindani mkali, huku Yanga SC ikiwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa. Klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani, Dar es Salaam, imekuwa ikifanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano yote. Makala haya yanakupa picha kamili ya kile kinachoendelea ndani na nje ya uwanja kwa Wananchi.
SOMA HII PIA:Ratiba ya mechi zijazo Yanga SC | Matokeo na msimamo NBC Premier League
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1
Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-
Kamata ratiba na matokeo ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27
Kwenye ratiba na matokeo ya Yanga SC NBC Premier League kuna mchanganyiko wa mechi za nyumbani na ugenini.Timu hiyo ilifungua msimu wa 2026/27 kwa mchezo wa ugenini.Ilikuwa Namungo FC 1-3 Yanga SC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.Pointi tatu walibeba mabingwa watetezi na Maxi Nzengeli alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Ratiba ijayo kwa Yanga SC inaonyesha mchezo ujao wa ligi ni Novemba 20, 2026 itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania.Ijumaa Novemba 27, 2026 itavaana na Mbeya City na Desemba 4, 2026 inatarajiwa kumenyana na Azam FC.
Hivyo mechi za mwanzo za Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwenye ligi itakuwa Polisi Tanzania vs Yanga SC, Mbeya City vs Yanga SC na Yanga SC vs Azam FC.
Matokeo ya Yanga SC katika msimu huu
Mabingwa watetezi wamecheza mechi 10 ndani ya ligi.Imepata ushindi kwenye mechi 8, sare mchezo mmoja na ikipoteza mchezo mmoja.10/10/2026, Simba SC 2-1 Yanga SC ni mchezo pekee uliovuja rekodi ya timu hiyo kutofungwa ndani ya msimu mpya.
Katika mchezo huo wa Kariakoo Dabi, Yanga SC walianza kufunga kupitia kwa Peter Shalulile.Simba SC ilisawazisha kupitia kwa Neo Maema na Elie Mpanzu.Nyota Mpanzu alichaguliwa kuwa Man of The Match katika mchezo huo.
Msimamo wa Yanga SC kwenye ligi kuu
Yanga SC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili. imekusanya pointi 25 baada ya mechi 10.Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 23 huku ile ya ulinzi ikiruhusu mabao 5.
Vinara wa ligi ni Simba SC wakiwa na pointi30 baada ya mechi 10.Mnyama chini ya Steve Berkar amepata ushindi kwenye mechi zote.Ni pointi 30 amekusanya kwenye msimamo.
SOMA HII PIA:Ratiba ya Yanga SC CAF Champions League 2026/27 | Kundi B | Msimamo | SportPesa Blog
Hitimisho
Ratiba na matokeo ya Yanga SC NBC Premier League yamekusanya aina zote 3 katika uwanja.Wameoja ladha ya ushindi kwenye mechi 8, kipigo mchezo mmoja na sare mchezo mmoja.Timu hiyo inapambania taji la ligi ambalo lipo mkononi mwao kwa sasa.


