Tanzania 0-0 Nigeria 17/11/2026: AFCON 2027 Qualifier highlights, Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

Matokeo Full TimeMatokeo Full TimeMatokeo Full Time

Tanzania 0-0 Nigeria 17/11/2026: AFCON 2027 Qualifier highlights, Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

  • Dakika 90 zimemalizika Uwanja wa New Amaan Complex, huku ubao wa matokeo ukionyesha Tanzania 0-0 Nigeria.
  • Ni katika mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027.
  • Mchezo huu ni wa Kundi L ambapo Nigeria walikuwa na mahitaji makubwa ya ushindi ili kuongoza msimamo wa Kundi hilo.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi matukio ya mchezo huu.

Tanzania 0-0 Nigeria ndivyo ambavyo ubao wa matokeo wa Uwanja wa New Amaan Complex umeonyesha baada ya dakika 90 kukamilika. Ni katika mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027. Mchezo huu ni wa Kundi L, ambapo Nigeria walikuwa na mahitaji makubwa ya ushindi ili kuongoza msimamo wa Kundi hilo.

SOMA HII PIA: Tanzania vs Nigeria 17/11/2026: AFCON 2027 Qualifier Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

Kipindi cha kwanza Tanzania 0-0 Nigeria

Matokeo Half Time
Matokeo Half Time

Nigeria waliingia katika mchezo huu kwa nguvu Wakisaka nafasi ya kupata matokeo mapema. Nigeria walijenga mashambulizi ya haraka, hasa dakika ya 10 kuifungua safu ya ulinzi ya Tanzania. Nigeria walikaribia kupata bao dakika ya 33 baada ya shambulizi lao kugonga mwamba.

Dakika ya 37 Nigeria walijenga shambulizi kutokea winga wa kulia, huku Manula akifanya kazi kubwa kuokoa na shambulizi hilo kuwa kona. Licha ya majaribio hayo safu ya ulinzi ya Tanzania ilikuwa imara kuyadhibiti. Dakika 45 za kwanza zilikamilika bila timu bao.

SOMA HII PIA: Nigeria 3-1 Tanzania, Africa Cup of Nations Qualification 2027 | Highlights | H2H| SportPesa Blog

Shinda mpaka Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘Aviator’ gusa hapa chini

image

Kipindi cha pili Tanzania 0-0 Nigeria

Tanzania 0-0 Nigeria
Nado vs Nigeria

Tanzania ilianza kwanguvu kipindi cha pili ambapo, dakika ya 53 mashambulizi mawili mazito likiwemo la, Kibu Denis na mlinzi wa Stars liliishia kugonga mwamba. Dakika ya 75 Nigeria walikosa bao la wazi baada ya safu ya ulinzi ya Tanzania kujichanganya. Filimbi ya mwamuzi kuashiria dakika 90 zimekamilika ilipulizwa huku matokeo yakiwa ni 0-0.

SOMA HII PIA: Taifa Stars vs Nigeria: Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

Hitimisho

Kibu X Iwobi
Kibu X Iwobi

Matokeo ya Tanzania 0-0 Nigeria umeathiri msimamo wa Kundi L ambapo mpaka sasa Nigeria wamekusanya pointi 7 wakiwa nbafasi ya 2. Tanzania wao wanaendelea kuburuza mkia licha ya kufanikiwa kuongeza pointi moja. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.