Tanzania vs Nigeria 17/11/2026: AFCON 2027 Qualifier Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi
- Tanzania vs Nigeria ni mchezo wa Kundi L wa kufuzu AFCON 2027, unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumanne 17/11/2026 nchini Tanzania.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwac kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
- Mechi hii ya mkondo wa pili inakuja ikiwa ni siku 4 tu zimepita tangu kumalizika kwa mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Novemba 13, 2026 ambapo matokeo yalikuwa Nigeria 3-1 Tanzania.
- Fuatilia matokeo ya mchezo huu kupitia SpoPesa Score.
Ratiba ya mechi za kufuzu mashindano ya AFCON 2027 inaendelea wiki hii, ambapo Jumanne itapigwa mechi kali ya Tanzania vs Nigeria. Mechi hii ya kud L la kufuzu AFCON 2027 ITAPIGWA Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ijumaa ya 13/11/2026 matokeo yalikuwa Nigeria 3-1 Tanzania. Makala hii inachambua kwa ufupi mchezo wa marudiano.
SOMA HII PIA: Taifa Stars vs Nigeria: Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi
Ratiba ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria

Mechi ya Tanzania vs Nigeria 2026 imepangwa kufanyika Jumanne, tarehe 17 Novemba, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex. Tayari kikosi cha Taifa Stars kimewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi hiyo. Kikosi hiko cha Stars kinaongozwa na Kocha mkuu Miguel Gamond.
Shinda mpaka Milioni 800 sasa, cheza ‘aviator’ kindege cha SportPesa gusa hapa chini
Matokeo ya Tanzania vs Nigeria na historia ya mechi

Taifa Stars na Super Eagle zimekutana katika mechi 9 katika historia. Nigeria amekuwa na rekodi bora zaidi ambapo wameshinda mechi 6. Mechi 3 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare.
SOMA HII PIA: Taifa Stars: Rekodi na Matokeo Muhimu Katika Soka la Tanzania
Nafasi zao katika kundi L
AFCON 2027 Kundi L linajumuisha timu 4 ambazo ni; Tanzania, Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau. Mpaka sasa Guinea-Bissau wanaongoza msimamo na pointi zao 7, wakifuatiwa na Nigeria ambao wana pointi 6. Madagascar wako katika nafasi ya 3 na pointi zao 2, huku Tanzania wakiburuza mkia baada ya kuvuna pointi 1 tu baada ya kucheza mechi 3.
Kuhusu Tanzania kufuzu AFCON 2027

Licha ya kuburuza mkia kwenye msimamo, ikumbukwe Taifa Stars tayari ina nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika AFCON 2027 kwa kuwa Tanzania ni mwenyeji mwenza. Kwa mujibu wa mfumo wa CAF, timu yenye nafasi ya juu zaidi miongoni mwa Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau ndiyo itakayochukua nafasi nyingine ya kufuzu kutoka kundi hili. Kwa Tanzania, mechi za kufuzu AFCON 2027 zinaendelea kuwa fursa ya kujenga kiwango cha ushindani kabla ya fainali hizo.
SOMA HII PIA: Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) za msimu wa 2025/2026 | Orodha ya wachezaji | MVP
Habari za kikosi cha Tanzania

Kikosi cha Tanzania dhidi ya Nigeria kinaongozwa na kocha Miguel Gamondi. Tayari kikosi hiko kimewasili Zanzibar tayari kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa Jumanne. Hakuna taarifa ya majeruhi wapya baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria.
Hitimisho
Tanzania vs Nigeria ni miongni mwa mechi kali ambazo zinasubiriwa kwa hamu. Nigeria katika nafasi ya pili ya kundi L watatamani kuchanga karata zao vizuri ili kukata tiketi ya kufuzu, hii ni kwa kuzingatia kundi hilo limesaliwa na tiketi moja pekee. Endelea kufuatilia SpotPesa blog kwa taarifa zaidi.


