
JKT Tanzania vs Simba SC: H2H na Taarifa za Timu 21 Novemba 2026 | Prediction
- Wanaubonda kati ya JKT Tanzania vs Simba SC NBC Premier League, 21 Novemba 2026.
- Matokeo ya mchezo uliopita walipokutana ilikuwa JKT Tanzania 1-2 Simba SC, beki Wilson Nangu akifunga dhidi ya waajiri wake wa zamani.
- Kwenye msimamo,Simba SC nafasi ya kwanza ina pointi 30, JKT Tanzania ipo nafasi ya 4.
Wanakutana JKT Tanzania vs Simba SC ni ratiba inayofuata NBC Premier League kwa wababe hawa wawili.Novemba 21, 2026 pambano hili kali litapigwa, Uwanja wa Meja.Jen.Isahmuyo.JKT Tanzania kwenye msimamo inakamata nafasi ya 4 inakutana na Simba SC inayoongoza ligi 2026/27.
SOMA HII PIA:JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26/ Highlights, goal
Vuna mamilioni sasa hivi na ukipaisha kindege na SportPesa
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.
JKT Tanzania vs Simba SC taarifa kuhusu mchezo
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Mchezo | JKT Tanzania vs Simba SC |
| Uwanja | Meja.Jen.Isahmuyo |
| Tarehe | 21/11/2026 |
| Timu mwenyeji | JKT Tanzania |
Taarifa za timu na majeruhi
JKT Tanzania wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo unaofuata.Masau Bwire, Ofisa Habari wa timu hiyo amebainisha kuwa kila mchezaji yupo kamili.Amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani.
“Kila mchezaji yupo tayari kuelekea mchezo wetu ujao.Uzuri ni muda wa kila mtu kuhushudia kichapo cha kizalendo kinaendelea.Hakuna namna tupo kamili kwa mchezo na malengo ni kupata pointi tatu muhimu,”.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema wapo kamili kwa mchezo.Amebainisha kuwa mchezo dhidi ya Mashujaa FC ni maalumu kuelekea kwenye mchezo ujao.
“Mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Mashujaa FC ni maalumu kwa mechi zinazofuata.Wachezaji wapo tayari na tunatambua ushindani ni mkubwa.Kikubwa ni kuona tunapata matokeo mazuri,”.
Takwimu za head-to-head (h2h) na fomu ya sasa
Historia ya michezo kati ya JKT Tanzania na Simba SC inaonyesha ushindani mkubwa. Katika mchezo wa awali uliochezwa Novemba 8, 2025, Simba SC waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Tanzania. Takwimu hizi zinaashiria kuwa Simba SC wana rekodi nzuri dhidi ya wapinzani wao.
Fomu ya sasa ya timu zote mbili katika Ligi Kuu NBC itakuwa muhimu sana. Simba SC wanashika nafasi ya kwanza kwenye ligi na pointi 30,JKT Tanzania nafasi ya 4 wakiwa na pointi 11.Kagera Sugar inaburuza mkia ikiwa na pointi 6 baada ya mechi 11.
Wachezaji muhimu na mbinu za kimchezo
Simba SC wanategemea wachezaji wao wenye uzoefu na vipaji vya hali ya juu kuleta matokeo chanya. Libase Gueye, Elie Mpanzu, Clatous Chama, Nathaniel Chilambo ni silaha ya Steve Barker katika mechi za ushindani.Mbinu zao za kushambulia na ulinzi imara zitakuwa muhimu katika mchezo huu.
Kwa upande wa JKT Tanzania, watahitaji nidhamu ya hali ya juu na kutumia vizuri nafasi watakazopata ili kuweza kuwazuia Simba SC.Mlinda mlango Chalamanda, kiungo Nassoro Maulid, uwepo wa Bajana, Kapalata na Peter Paul eneo la ushambuliaji ni mashine za kazi kwa JKT Tanzania.
SOMA HII PIA:JKT Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27
Utabiri na mtazamo wa wahariri
Kutokana na rekodi ya H2H na nafasi ya Simba SC kwenye ligi, wao wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu. Hata hivyo, JKT Tanzania watajitahidi kutumia uwanja wa nyumbani (kama itathibitishwa) na kucheza kwa nguvu zote ili kupata matokeo mazuri. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mabao machache kutokana na ushindani mkali.
JKT Tanzania 1-2 Simba SC ni matokeo ya utabiri katika mchezo huu.Haya sio matokeo rasmi ni utabiri, matokeo rasmi yatapatikana baada ya mchezo.
Hitimisho
Mchezo kati ya JKT Tanzania vs Simba SC unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka. Simba SC wataingia uwanjani wakiwa na lengo la kuendeleza rekodi yao nzuri, huku JKT Tanzania wakitafuta ushindi muhimu. Endelea kufuatilia SportPesa kwa uchambuzi zaidi na taarifa za michezo.


