- Hii hapa ratiba ya Yanga SC CAF Champions League 2026/27 ikipangwa Kundi B.
- Watoto wa Jangwani watakabiliana na mechi kali ikiwemo Yanga SC vs MC Alger, Zamalek SC vs Yanga SC.
- Mchezo wa kwanza watakuwa nyumbani 28,Novemba 2026 watawakaribisha MC Alger

Hapa tumekuletea ratiba ya Yanga SC CAF Champions League 2026/27 hatua ya makundi.Ikumbukwe kwamba watoto hawa wa Jangwani walitinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1 dhidi ya CFFA FC.Oktoba 17,2026 CFFA FC 0-4 Yanga SC na Oktoba 21,2026, Yanga SC 4-1 CFFA FC.Mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar katika droo ilichozwa Misri walipangwa Kundi B.
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1
Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

Ijue ratiba ya Yanga SC CAF Champions League 2026/27
| Mechi | Tarehe | Mahali |
| Yanga SC vs MC Alger | 28 Novemba 2026 | Nyumbani |
| Club Africain vs Yanga SC | 5 Desemba 2026 | Ugenini |
| Zamalek SC vs Yanga SC | 18 Desemba 2026 | Ugenini |
| Yanga SC vs Zamalek SC | 8 Januari 2027 | Nyumbani |
| MC Alger vs Yanga SC | 15 Januari 2027 | Ugenini |
| Yanga SC vs Club Africain | 22 Januari 2027 | Nyumbani |
Maoni ya Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC
Ali Kamwe, amebainisha kuwa wana kazi kubwa katika kutafuta matokeo.Licha ya kuwa kwenye kundi lenye timu bora alisema wana kikosi chenye wachezaji wenye uzoefu.Kamwe aliongeza kuwa wataingia kwenye kila mchezo kutafuta ushindi.
“Kila timu ambayo ipo hatua ya makundi ni bora.Tuna amini wachezaji wanatambua umuhimu wa kutafuta matokeo, tutaingia uwanjani kwa hesabu za ushindi.Mashabiki tuendelee kuwa pamoja malengo ni kuona tunasonga mbele na inawezekana kwenye mpira,”.
SOMA HII PIA:Vilabu vya Tanzania CAF: Simba SC, Yanga SC, Azam FC na Singida Black Stars
Msimamo wa Kundi B
| Nafasi | Timu | Mechi (P) | W | D | L | GD | Pointi |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Club Africain | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| 2 | MC Alger | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| 3 | Yanga SC | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| 4 | Zamalek SC | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
Hitimisho
Kwenye ratiba ya Yannga SC CAF Champions League 2026/27 watafungua mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex.Watafunga hesabu wakiwa nyumbani msimu wa 2026/27 katika kusaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali.Mechi ya kwanza ugenini inatarajiwa kuwa Desemba 5,2026 vs Club Africain.

