- Katika ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27 Kundi C mchezo wa kwanza itawakaribisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
- Simba SC vs Colombe Sportive hii ni mechi ya funga kazi mnyama atakuwa nyumbani kufunga hesabu za msimu katika hatua ya makundi.
- Makala hii tunaangazia ratiba ya Simba SC CAF katika hatua za makundi mechi 6 zakukata na shoka.

Kazi inaendelea kimataifa na hapa tumekuletea ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27.Mnyama amepangwa Kundi C timu nyingine ni RS Berkane ya Morocco, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Colombe sportive ya Cameroon.Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amesema wanatambua ugumu wa mechi zijazo watafanya maandalizi mazuri.
SOMA HII PIA:Vilabu vya Tanzania CAF: Simba SC, Yanga SC, Azam FC na Singida Black Stars
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1
Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

Kamata ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27
| Tarehe | Mechi |
|---|---|
| 27 Novemba 2026 | Simba SC vs Orlando Pirates |
| 04 Desemba 2026 | Colombe Sportive vs Simba SC |
| 18 Desemba 2026 | RS Berkane vs Simba SC |
| 08 Januari 2027 | Simba SC vs RS Berkane |
| 15 Januari 2027 | Orlando Pirates vs Simba SC |
| 22 Januari 2027 | Simba SC vs Colombe Sportive |
Msimamo Kundi C
| Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| Colombe Sportive | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Orlando Pirates | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| RS Berkane | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Simba SC | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
Maoni ya Steve Barker
Kocha Mkuu wa Simba SC, mara baada ya droo kupangwa alibainisha kuwa wapo na timu zenye ubora.Raia huyo wa Afrika Kusini aliongeza kuwa watafanya maandalizi mazuri kupata matokeo.Aliwaomba mashabiki kuwa na timu kila wakati.
“Tumeona ni kundi lenye timu bora na zenye wachezaji wazuri.Kwenye hatua hii ya makundi kikubwa ni maandalizi mazuri na kuwa tayari kwa kila mchezo.Wachezaji wapo tayari na wanatambua umuhimu wa kila mchezo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi katika kila mechi,”.
SOMA HII PIA:Simba SC imepangwa Kundi C CAF: RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe Sportive
Hitimisho
Kwenye ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27 kuna mechi za kisasi ikiwemo ule dhidi ya RS Berkane.Wababe hawa walikutana kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na bingwa alikuwa ni RS Berkane.Wekundu wa Msimbazi wametinga hatua ya makundi mara 7 hivyo wana uzoefu na mechi za kimataifa.

