Simba SC vs Yanga SC Oktoba10,2026ShalulileShalulile

Peter Shalulile wamoto mechi 9 magoli 6: Takwimu zake Ligi Kuu ya NBC, hizi hapa

  • Peter Shalulile straika aliyetikisa usajili Yanga SC wa Tanzania kwenye dirisha kubwa la usajili 2026/27 ni balaa.
  • Nyota huyo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu pekee amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 6 ndani ya mechi 9 za kwanza akifunga mabao 5 na kuasisti mara 1.
  • Staa huyo wa zamani wa Mamelodi alijiunga na Yanga SC akitokea kikosi cha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kwa ada inayokadiriwa kufikia Bilioni 1.8
  • Baada ya kufunga mabao zaidi ya mabao 100 akiwa Afrika Kusini, sasa yuko Tanzania na Makala hii inakuchambua kwa ufupi takwimu za Peter Shalulile.

Straika mpya wa Yanga SC, Peter Shalulile amezidi kuwa gumzo nchini, hii ni kutokana na kasi yake ya kucheka na nyamu tangu alipotua Yanga SC. Shalulile alijiunga na Yanga SC ya Tanzania kwenye dirisha kubwa la usajili 2026/27 kwa ada inayokadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 1.8 za kitanzania. Tangu atambulishwe rasmi nyota huyo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ya NBC pekee amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 6 ndani ya mechi 9 za kwanza akifunga 5 na kuasisti bao 1. Makala hii inachambua kasi ya staa huyo.

SOMA HII PIA: Peter Shalulile atikisa usajili Yanga SC 2026/27: Atua Jangwani na mabao 136, asisti 35 hizi hapa rekodi zake

Safari ya soka ya Peter Shalulile

Peter Shalulile
Peter Shalulile

Peter Shalulile alianza safari yake ya soka nchini Namibia kabla ya kuhamia Afrika Kusini, ambako aling’ara zaidi. Alianza kucheza soka la kulipwa na klabu ya Tura Magic nchini kwake kabla ya kujiunga na Highlands Park nchini Afrika Kusini. Huko ndiko alikoanza kuonyesha uwezo wake wa kipekee wa kufunga mabao, na kuvutia macho ya klabu kubwa. Uhamisho wake kwenda Mamelodi Sundowns ulikuwa hatua kubwa kwake, ambapo akiwa na Sundowns, Shalulile aligeuka kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Afrika, akishinda mataji mengi ya ligi na ya Afrika na kuwa mfungaji bora mara kadhaa.

Zaidi ya Shilingi Milioni 800 inatoka muda huu, cheza kindege cha SportPesa, gusa hapa chini

image
 

Rekodi ya mabao na mafanikio barani afrika

Yanga SC
Shalulile 

Shalulile ameacha alama isiyofutika katika soka la vilabu barani Afrika. Akiwa na Mamelodi Sundowns, alikuwa nguzo muhimu katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa kama Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Uwezo wake wa kufunga mabao muhimu umemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki na mchezaji anayeheshimika na wapinzani.

Ameshinda tuzo kadhaa za mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (DStv Premiership) na alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Sundowns kwa ufanisi mkubwa. Rekodi yake ya kufunga mabao katika CAF Champions League pia inamweka katika orodha ya washambuliaji bora wa kizazi chake. Kwa mujibu wa rekodi za Tranfermarket akiwa na jezi ya klabu tatu alizozichezea, Shalulile ameandika rekodi ya kipekee akifanikiwa kufunga mabao 136 katika mechi 313 alizocheza.

SOMA HII PIA: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo kilele cha Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Uhuru | Shalulile afungua akaunti ya mabao | SportPesa Blog

Uhusiano wa kutua Yanga SC

Peter Shalulile
Peter Shalulile

Safari ya, Peter Shalulile kutua Yanga SC ilianza kama tetesi, kabla ya taarifa rasmi kuthibitisha amekamilisha usajili. Usajili wake unatajwa kuhusisha kiwango kikubwa cha fedha kinachokadiriwa kufikia fedha za kitanzania Bilioni 1.8.  Tangu atue Ligi Kuu Tanzania (NBC Premier League) na mashindano ya kimataifa, amekuwa nyota hatari akiiongoza vyema safu ya ushambuiaji ya Yanga SC. Amefunga mabao 5 mpaka sasa, likiwemo bao 1n dhidi ya Simba SC, huku pia akiasisti mara moja.

SOMA HII PIA: Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog

Hitimisho

Peter Shalulile ni mshambuliaji mwenye kipaji cha kipekee ambaye amethibitisha uwezo wake barani Afrika. Msimu huu mpaka sasa anashika nafasi ya tatu kwenye listi ya wafungaji bora, lakini kuna kila uwezekano akawa anataka kubeba kiatu cha dhahabu kama ataendelea na kasi yake. Endelea kufuatilia SporPesablog kwa taarifa zaidi.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.