Yanga SC 1-2 Aigles du Congo kilele cha Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Uhuru | Shalulile afungua akaunti ya mabao | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

August 10, 2026
Yanga SC 1-2 Aigles du CongoShalulile (-)Shalulile (-)
  • Mechi ya kimataifa ya kirafiki Yanga SC 1-2 Aigles du Congo kilele cha Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Uhuru
  • Peter Shalulile afungua akaunti ya mabao akiwa na uzi wa njano na kijani
  • Talas Tony atibua shughuli ya Wananchi kwa kufunga mabao yote mawili

Mara baada ya dakika 90 imekuwa Yanga SC 1-2 Aigles du Congo matokeo rasmi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Uhuru. Ni katika kilele cha tamasha la Wiki ya Mwananchi lililohitimishwa kwa burudani ya mechi kali iliyokuwa na ushindani mkubwa. Peter Shalulile alifungua akaunti ya mabao kwa mkwaju wa penati iliyomshinda mlinda mlango.

Yanga SC 1-2 Aigles du Congo
Shalulile mshambuliaji wa Yanga SC

Yanga SC 1-2 Aigles du Congo

Ni Yanga SC 1-2 Aigles du Congo mabao matatu yalifungwa ndani ya dakika 90 kali uwanjani. Bao la kwanza lilifungwa na Peter Shalulile dakika ya 26. Wageni walifunga mabao kupitia kwa Talas Tony dakika ya 36 na 65 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Uhuru. Mbali na wale waliokuwa ndani nje pia kulikuwa na Big Screen ambayo ilikuwa inawapa burudani mashabiki. Utambulisho wa wachezaji ni ishara kwamba pazia la msimu .

Tamasha la Yanga Day, SportPesa utambulisho wake wafana

Ukiachana na matokeo kwenye mchezo wa kirafiki tamasha la Yanga Day, SportPesa lilifana kutokana na utambulisho uliofanywa. Wachezaji wapya na wale ambao walikuwa na kikosi 2025/26 lilikuwa na upekee wake. Kwa mara ya kwanza Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC, Ali Kamwe alifanya utambulisho wake.

Kamwe aliingia Uwanja wa Uhuru akiwa amevaa jezi namba 6. Uzi huo mbele ulikuwa na nembo ya mdhamini mkuu SportPesa na upande wa mgongoni ambapo huwa panakaa jina paliandikwa Pesa Zipo Bank. Alianza kwa kuwatambulisha manahodha wawili Bakari Nondo na Dickson Job.

Wachezaji walioongeza mkataba

Ibrahim Bacca, beki kitasa ameongeza kandarasi ya miaka miwili. Yao Kouasi naye ameongezewa kandarasi ya miaka miwili.Mlinda mlango namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra naye ameongeza kandarasi ya miaka miwili. Hivyo mastaa hawa bado wapo Jangwani.

Ikumbukwe kwamba Bacca, Yao, Diarra na Bakari Nondo ambaye ni nahodha walibakiza mkataba wa mwaka mmoja. Ni uhakika kwamba bado wataendelea kuwa katika kikosi cha Yanga SC 2026/27.

Hitimisho

Yanga SC 1-2 Aigles du Congo mchezo uliokuwa na mvuto mkubwa kutokana na timu zote kuonyesha viwango bora. Mchezo unaofuata kwa Wananchi ni dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa Agosti 12,2026. Huu ni mchezo wa Ngao ya Jamii, utachezwa Zanzibar, New Amaan Complex.

Share this: