
- Wanakutana JKT Tanzania vs Azam FC NBC Premier League 2026/27, Uwanja wa Mej.Gen.Isamuhyo.
- Kwenye msimamo JKT Tanzania nafasi ya 4 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya 3.
- H2H mechi 6 zilizopita Azam FC ilishinda 4 na sare kwenye mechi 2.
Ni JKT Tanzania vs Azam FC mchezo unaofuata kwenye ratiba ya NBC Premier League 2026/27.Wababe hawa wanakutana Uwanja wa Maj. Gen. Isamuhyo ikiwa ni raundi ya 10.Saa 12:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki pambani hili lipatigwa, Oktoba 31,2026.
SOMA HII PIA:Azam FC: Matokeo, Ratiba na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27
Shinda mamilioni kwa kuanzia shilingi 1 tu na SportPesa
Una nafasi kushinda zaidi ya mamilioni sasa hivi ukisuka mkeka wako kupitia SportPesa.Nafasi ni yako sasa na odds zimeboreshwa.Kuna chaguo la 1UP, 2UP, 3UP hapa unavuna mapene kabla ya dakika 90.Bashiri kwa uwajibikaji, bofya link hapa chini:-

JKT Tanzania vs Azam FC taarifa
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Mchezo | JKT Tanzania vs Azam FC |
| Uwanja | Maj. Gen. Isamuhyo |
| Tarehe | 31/10/2026 |
| Timu mwenyeji | JKT Tanzania |
JKT Tanzania vs Azam FC H2H
Kwenye mechi za hivi karibuni walipokutana Azam FC imekuwa ikipata matokeo mazuri.Katika mechi 6,ushindi ilikuwa ni mechi 4 zote matajiri wa Dar walishinda.Sare mechi mbili, kwenye safu ya ushambuliaji Azam FC ilifunga jumla ya mabao 11 na JKT Tanzania mabao 3.
17 Apr 2026: Azam FC 3 – 0 JKT Tanzania
01 Okt 2025: JKT Tanzania 1 – 1 Azam FC
27 Des 2024: Azam FC 3 – 1 JKT Tanzania
28 Ago 2024: JKT Tanzania 0 – 0 Azam FC
21 Mei 2024: JKT Tanzania 0 – 2 Azam FC
11 Des 2023: Azam FC 2 – 1 JKT Tanzania
Wachezaji muhimu na mbinu za kimchezo
Kwa Azam FC, wachezaji akiwemo Feisal Salim, Sopu, Aishi Manula na Iddy Seleman Nado wamekuwa nguzo muhimu katika mechi za ushindani. Uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao utakuwa muhimu. JKT Tanzania watahitaji kutegemea ulinzi wao imara na mashambulizi ya kushtukiza ili kuwapa changamoto Azam FC.
Mbinu za kimchezo zitategemea sana jinsi makocha watakavyoamua kucheza. Azam FC huenda watajaribu kumiliki mpira na kushambulia kwa kasi, huku JKT Tanzania wakilenga kujilinda na kutumia mipira mirefu au mashambulizi ya kushtukiza.
SOMA HII PIA:Usajili wa Azam FC 2026/27: Ilese, Taiwo Adolf Mtasigwa akutana na Thank You | SportPesa Blog
Utabiri na mtazamo wa wahariri
Kutokana na takwimu za hapo awali na hali ya sasa ya timu, Azam FC wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huu. Hata hivyo, JKT Tanzania wamekuwa wakionyesha upinzani mkali wanapocheza nyumbani, na wanaweza kusababisha mshangao.
Tunatarajia mchezo wa kuvutia na ushindani mkali. Matokeo ya mwisho yatategemea sana jinsi timu zitakavyoingia uwanjani na kutumia nafasi watakazopata.JKT Tanzania 1-2 Azam FC haya ni maoni ya mhariri, matokeo rasmi yatapatikana baada ya mchezo.
Hitimisho
Wanakutana JKT Tanzania vs Azam FC katika pambano la NBC Premier League.Wazee wa mapigo na mwendo kwenye msimamo nafasi ya 4 na pointi 17 wanautana na Azam FC nafasi ya 3 na pointi 20.Vinara ni Simba SC wakiwa na pointi 27.

