Matokeo na ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27 | Unbeaten | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

October 31, 2026
Matokeo na ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27Chama- Oura na MpanzuChama- Oura na Mpanzu
Yao X Oura
Yao vs Oura
  • Tumekosogezea matoko na ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27
  • Kwenye ratiba kuna mechi kali zinafuata ikiwemo Simba SC vs Namungo FC, Yanga SC vs Simba SC
  • Simba SC ni unbeaten imeshinda mechi zote 9 ikiwa na pointi 27 kwenye msimamo inafuatiwa na Yanga SC iliyo nafasi ya pili.

Msimu umeanza tumekuletea matokeo na ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27.Chini ya Kocha Mkuu,Steve Barker raia wa Afrika Kusini watoto wa Msimbazi ni Unbeaten.Mechi 9 ushindi asilimia 100 mchezo ratiba ya mechi inayofuata ni dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Uhuru, Novemba 2,2026.

SOMA HII PIA:Fountain Gate 0-1 Simba SC: NBC Premier League, Matokeo, Highlights, magoli, Rushine aibeba Simba SC

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege

Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.

image

Haya hapa Matokeo na ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27

Mchezo uliopita matokeo ilikuwa Fountain Gate FC 0-1 Simba SC.Bao la ushindi lilifungwa na beki Rushine akitumia pasi ya Nathaniel Chilambo wakiwa ugenini.Kikosi kimerejea Dar kwa maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Namungo FC.

TareheMchezoUwanjaMatokeoHali ya Mchezo
29 Oktoba 2026Fountain Gate FC vs Simba SCUgenini0 – 1Ushindi
13 Oktoba 2026Simba SC vs Mashujaa FCNyumbani6 – 1Ushindi
10 Oktoba 2026Simba SC vs Yanga SCNyumbani2 – 1Ushindi
Mwezi Oktoba 2026Simba SC vs Dodoma Jiji FCNyumbani1 – 0Ushindi
16 Septemba 2026Azam FC vs Simba SCUgenini0 – 2Ushindi
31 Agosti 2026Simba SC vs Geita Gold FCNyumbani2 – 0Ushindi
27 Agosti 2026Simba SC vs Coastal UnionNyumbani1 – 0Ushindi
19 Agosti 2026Pamba Jiji FC vs Simba SCUgenini1 – 2Ushindi
16 Agosti 2026Kagera Sugar vs Simba SCUgenini0 – 2Ushindi

Ratiba ya mechi zijazo Simba SC NBC Premier League

Simba SC vs Namungo FC, Novemba 2,2026, Uwanja wa Uhuru

JKT Tanzania vs Simba SC, Novemba 21,2026, Uwanja wa Mej.Gen.Isahmuyo

TRA United vs Simba SC, Desemba 11,2026, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Polisi Tanzania vs Simba SC, Desemba 31,2026, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Coastal Union vs Simba SC, Februari 2,2027, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

Yanga SC vs Simba SC,Februari 6,2027, Uwanja wa Uhuru, Dar

Mnyama mechi ya kufunga kazi 2026 itakuwa ugenini dhidi ya Polisi Tanzania.Atafungua ukurasa mpya 2027 kwa kuvaana na Coastal Union ya Tanga akiwa nyumbani.Kariakoo Dabi inatarajiwa kupigwa Februari 6,2027.

SOMA HII PIA:Simba SC imepangwa Kundi C CAF: RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe Sportive

Hitimisho

Kwenye matokeo na ratiba ya Simba SC mechi kali zinafuata NBC Premier League.Kikosi hicho kimepata ushindi katika mechi 9 kikiwa na pointi 27.Mchezo unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya Namungo FC,Novemba 2,2026 Uwanja wa Uhuru.

Share this: