
Azam FC, Klabu yenye makazi yake Chamazi, Dar ni moja ya timu inayoonyesha ushindani mkubwa katika Ligi Kuu Bara. Msimu wa 2026/27 umeshika kasi, na ‘Wana Lambalamba’ wanajitahidi kuonyesha ubora wao katika kila mchezo. Kuna matokeo, ratiba kamili ya mechi zijazo na mwendo wa Azam FC.
Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina kuhusu Azam FC, tukijikita kwenye takwimu muhimu, mechi zilizopita na zile zinazokuja. Pia tutaangalia msimamo wao wa sasa na nini kinatarajiwa kutoka kwao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Ujue usajili wa Azam FC: Usajili wa Azam FC 2026/27: Ilese, Taiwo Adolf Mtasigwa akutana na Thank You | SportPesa Blog
Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.
Matokeo ya hivi karibuni ya Azam FC
Azam FC imeanza msimu wa 2026/27 kwa kufungua pazia la mechi ugenini ikipata sare ya kufungana 1-1 Polisi Tanzania. Kila mchezo umekuwa na ushindani mkubwa malengo ni kupata pointi. Matokeo ya hivi karibuni yanaonyesha jinsi timu ilivyojipanga na mikakati ya Kocha Mkuu,Florent Ibenge.
Katika mechi zao za awali, Azam FC imeweza kuonyesha uwezo wa kushambulia na kujilinda. Ushindi dhidi ya Pamba Jiji FC ni mfano mmoja wa jinsi walivyoweza kutumia fursa na kupata pointi tatu muhimu. Hata hivyo, ligi bado ni ndefu na ushindani ni mkali.
Ratiba kamili ya Azam FC Ligi Kuu Bara 2026/27
Ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27 imejaa mechi za kusisimua kwa Azam FC. Kila mchezo ni muhimu, na mashabiki wanatarajia kuona timu yao ikifanya vizuri dhidi ya wapinzani wao. Hapa chini ni baadhi ya mechi muhimu zinazokuja:
| Tarehe | Mchezo | Uwanja | Muda (EAT) |
| 07 Septemba 2026 | Azam FC vs Namungo FC | Uwanja wa Azam Complex | Saa 1:00 usiku |
| 08 Oktoba 2026 | Coastal Union vs Azam FC | Uwanja wa Mkwakwani | Saa 3:00 usiku |
| TBD | Azam FC vs Mashujaa FC | Uwanja wa Azam Complex | TBD |
Msimamo wa Azam FC kwenye Ligi Kuu Bara
| Nafasi | Timu | Mechi | Pointi |
| 1 | Yanga SC | 5 | 15 |
| 2 | Simba SC | 5 | 15 |
| 3 | Azam FC | 5 | 11 |
| 4 | Singida Black Stars | 5 | 10 |
Uchambuzi wa kikosi na wachezaji muhimu
Azam FC inawachezaji wenye uzoefu mkubwa na majina katika kutimiza majukumu. Wachezaji kama vile Iddi Nado, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Aishi Manula wamekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya timu. Uwezo wao wa kufunga mabao na kuunda nafasi umekuwa muhimu sana.
Kocha mkuu wa Azam FC anaendelea kujenga timu imara yenye uwezo wa kushindana katika viwango vya juu. Mikakati yake ya kiufundi na uwezo wa kuhamasisha wachezaji ni muhimu katika kuhakikisha timu inafanya vizuri katika kila mchezo.
Usome muongozo wa Azam FC: Azam FC 2025: Mwongozo Kamili Kuhusu Kikosi, Benchi la Ufundi, na Urithi wa Klabu
Mechi inayofuata: Azam FC vs Namungo FC
Azam FC vs Namungo FC ni mchezo ujao kwenye ratiba. Huu unakuwa mchezo wa mzunguko wa 6 kwa matajiri wa Dar. Timu hiyo bado haijapoteza mchezo ndani ya msimu wa 2026/27.
Namungo FC inahitaji ushindi kutokana na mwendo wake. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 6. Azam FC ipo nafasi ya 3 ndani ya NBC Premier League.
Hitimisho
Azam FC inaendelea kuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27. Kwa matokeo yao ya hivi karibuni, ratiba iliyopangwa, na msimamo wao wa sasa, ‘Wana Lambalamba’ wako tayari kwa changamoto. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi na uchambuzi wa kina wa Ligi Kuu Bara.


