- Usajili mpya Yanga SC 2026/27 umeandikisha majina 13 kwa ajili ya mapambano rasmi ya kutetea ubingwa wao msimu huu.
- Ikumbukwe dirisha kubwa la usajili kwa Tanzania lilifungwa rasmi jana Jumamosi Agosti 15, 2026 baada ya kuwa wazi kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja.
- Mastaa wapya 13 wa Yanga SC ni; Juma Abushiri, Hussein Mihambo, Abdulnasir Muhamed, Mohamed Mussa, Erick Mwijage, Suleiman Mbarouk, Ibrahima Toure, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Peter Shalulile, Fred Ngoma, Selemani Mwalimu na Aziz Ki.
- Makala hii inachambua kwa ufupi usajili mpya uliokamilika wa Yanga SC 2026/27.
Dirisha kubwa la usajili kwa Ligi zilizo chini ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), umefungwa rasmi jana Jumamosi Agosti 15, 2026. Hii ni baada ya kuwa wazi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, tangu Julai 6, 2026. Uongozi wa Yanga SC umefanya maboresho makubwa ya kikosi chao, kwa kusajili Nyota wapya 13 ambao watatumika msimu huu. Makala hii inachambua kwa ufupi mastaa wapya wazawa watakaovaa uzi wa Yanga SC msimu wa 2026/27.
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Muhtasari Kuhusu usajili mpya Yanga SC 2026/27, Bilioni 15!
Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe amenukuliwa akisema kuwa bajeti ya usajili msimu huu viongozi wao walitenga bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 15 za kitanzania. Kwa sehemu kubwa bajeti hiyo imewezeshwa na wafadhili wao, akiwemo mfadhili mkuu Kampuni bora ya michezo ya kubashiri SportPesa. Bajeti hiyo kubwa imewapa jeuri timu hiyo, kufanya usajili wa majina makubwa akiwemo straika Peter Shalulile.
Huu hapa usajili uliokamilika wa wachezaji wapya wa Yanga SC 2026/27
Azizi Ki Stephanie

Ndio usajili mpwa wa mwisho kutangazwa. Ukipewa jina la ‘X Factor’, utambulisho wa Aziz Ki ulifanyika jana Agosti 15, 2026 kwenye Uwanja wa KMC. Aziz Ki anarejea Yanga aliyoichezea kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha misimu mitatu, akitokea Al Ittihad ya Libya.
KUJUA ZAIDI KUHUSU USAJILI MPYA YANGA SC, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog
Mohamed Mussa
Nyota huyu ni mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC, ambaye msimu uliopita alikuwa akihudumu na kikosi cha Mashujaa FC ya Kigoma. Alitambulishwa Jangwani rasmi Julai 21, 2026. Mussa amesajiliwa kuongezea nguvu safu ya ulinzi ya Yanga SC.
Peter Shalulile

Shalulile amejiunga na Yanga SC, baada ya kuachana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Kabla ya kutua Yanga SC Shalulile amewahi kupita kwenye timu za Tura Magic ya Namibia, Highlands Park na Mamelodi za Afrika Kusini. Nyota huyo tayari amefanikiwa kufunga mabao 2 katika mechi 3 akiwa na Yanga SC.
ALICHOSEMA ALI KAMWE KUHUSU USAJILI WA YANGA SC, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC balaa: Ali Kamwe atangaza mashine mbili mpya, namba 6 yatikisa, je ni Feisal?
Juma Issa Abushir
Mchezaji wa kwanza kutambulishwa mitaa ya Jangwani ni beki chipukizi ambaye ni mzawa. Julai 18,2026 alitambulishwa Juma Issa Abushir huyu ni beki kutoka Fountain Gate maarufu kwa jina la Chuga Boy. Alianza maisha ya soka kwenye kituo cha Future Stars kilichopo Arusha akiwa na miaka 6 tu.
Albert Kangwanda
Huyu alishinda tuzo ya MVP wa ligi ya Zambia msimu uliopita, kwenye ligi kuu ya Zambia msimu uliopita wa 2025/26 alifunga mabao 17 na asisti 9 na amesaini dili la miaka miwili. Miogoni mwa timu ambazo amecheza ni Al Hilal Omdurman ya Sudan, CSF Spartanii (Moldava), HNK Gorica, (Croatia) na Red Arrows ya Zambia. Nyota huyu alitambulishwa Julai 24, 2026 alitambulishwa.
Selemani Mwalimu

Utambulisho wake ulizua gumzo kubwa Tanzania, hii ni baada ya kutambulishwa Yanga SC muda mchache baada ya kutua Tanzania kama mchezaji wa Simba SC. Nyota huyo msimu uliopita alihudumu ndani ya Simba SC, kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca. Selemani Gomez nim wananchi msimu huu.
KUHUSU USAJILI YA NAMBA 6 MPYA YANGA SC, SOMA HII: Yanga SC usajili mpya 2026/27: Wat a pleyaa namba 6 huyu hapa, kutambulishwa kesho Jumamosi
Hussein Mihambo
Mali nyingine mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC ni mshambuliaji wa kazi. Anaitwa Hussen Mihambo aliyekuwa akicheza Mashujaa FC. Ni Julai 20,2026 alitambulishwa Jangwani kuwa ingizo jipya.
Farouk Komara
Alitambulishwa Agosti 4, 2026, ni raia wa Ivory Coast beki mwenye uwezo wa kucheza kiungo mkabaji. Ana miaka 26 tu. Ametokea Klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini kabla ya kutambulishwa Jangwani.
Cheikh Touré
Huyu ni mshambuliaji raia pacha wa Ufaransa na Senegal, ana miaka 29. Nyota hoyo amewahi kupita kwenye vilabu vya AS Nancy ya Ufaransa na Al-Jabalain ya Saudi Arabia. Julai 24 2026 alitambulishwa kuwa njano na kijani.
Erick Mwijage

Mwijage amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kutoka kikosi cha KMC ambayo tayari imeshuka daraja. Mwijage ndani ya Ligi Kuu ya NBC amefanikiwa kupita ndani ya timu mbalimbali ikiwemo; Kagera Sugar na Geita Gold. Mwijage anakuwa mchezaji wa 5 kusajiliwa na Yanga SC na kutambulishwa ndani ya dirisha hili la usajili.
Abdulnasir Muhamed
Beki wa kulia Abdulnasir Muhamed aliyekuwa Mashujaa FC naye ni kijani na njano. Alitambulishwa Julai 20,2026 kuwa mtaa wa Kariakoo.Ni kandarasi ya miaka miwili inaelezwa kuwa amesaini.
Housseine Zakouani
Housseine Zakouani (28) raia wa Comoros amejiunga na Yanga SC akiwa mchezaji huru. Nyota huyo amelelewa kwenye academy ya Olympique Marseille Ufaransa, pia amecheza kwenye vilabu vya Châteauroux, Hyères 83 FC na US Thionville Lusitanos zote za Ufaransa. Alitambulishwa Julai 24,2026.
Suleiman Mbarouk
Klabu ya Young Africans SC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Suleiman Mbarouk, mwenye umri wa miaka 18, akitokea JKU FC ya Zanzibar. Suleiman ameweka saini ya mkataba wa miaka mitatu na Yanga SC, huku klabu hiyo ikikamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake uliokuwa umebaki kwa mwaka mmoja na JKU.
Hitimisho
Usajili mpya Yanga SC 2026/27 umekamilika na unaakisi taswira ya mchanganyiko wa uzoefu na ubora. Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano kutoka Jangwani, amebainisha malengo yao ni kufanya makubwa msimu huu. Timu hiyo ina kibarua cha kutetea ubingwa 2026/27. Endelea kufuatilia SportPesa blog kwa taarifa mbalimbali.

