Kagera Sugar 0-2 Simba SCMpanzu Kagera
  • FT: Kagera Sugar 0-2 Simba SC NBC Premier League
  • Peter Shalulile ameanza kazi kufunga ndani ya ligi mchezo wake wa kwanza
  • Namungo FC 1-3 Yanga SC, Uwanja wa Majaliwa, Agosti 15,2026

Burudani imerejea na Kagera Sugar 0-2 Simba SC ni matokeo rasmi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Bukoba.JKT Tanzania 1-1 TRA United ulikuwa mchezo wa mwisho kukamilisha mzunguko wa kwanza. Jumla yamefungwa mabao 17 huku Singida Black Stars ikiwa timu ya kwanza kuongoza ligi msimu mpya.

Ijue ratiba ya NBC Premier League: Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Mechi zote 240 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Play Aviator on SportPesa – maximum payout TZS 800 million

Matokeo Kagera Sugar 0-2 Simba SC, Duchu aonyeshwa kadi nyekundu

Kagera Sugar 0-2 Simba SC
Duchu beki wa Simba SC.

Wakati ligi ikianza mchezo wa Kagera Sugar 0-2 Simba SC umeandika rekodi kushuhudia kadi nyekundu ya kwanza kwa mnyama. Beki David Kameta maarufu kama Duchu alionyeshwa kadi nyekundu. Kadi hiyo alionyeshwa dakika ya 53 kwa kumchezea faulo David Luhende.

Mlinda mlango namba moja wa Simba SC, Mamadou Kassali alipata maumivu ya goti kwenye mchezo. Nafasi yake ilichukuliwa na kipa namba mbili, Hussen Abel. Kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye mechi zijazo za ligi.

Agosti 14,2026

Pamba Jiji FC 1-1 Dodoma Jiji FC. Beno Ngasa wa Dodoma Jiji FC mfungaji wa bao la kwanza msimu wa 2025/26 ilikuwa dakika ya 17 na bao la Pamba Jiji FC lilifungwa na Deogratius Judica dakika ya 24, Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Mbeya City 0-1 Geita Gold, mfungaji Obrey Chirwa dakika ya 15

Singida Black Stars 3-0 Fountain Gate, Uwanja wa Airtel, wafungaji Jonathan Sowah dakika ya 28, Yusuph Dunia dakika ya 81 na Mathew Tegis dakika ya 90+4.

Agosti 15,2026

Kagera Sugar 0-2 Simba SC
Wachezaji wa Yanga SC wakishangilia mtindo wa Shalulile.

Yanga SC bingwa: Yanga SC bingwa NBC Premier League 2025/26/ Matokeo yote/ Zilizoshuka daraja

Polisi Tanzania 1-1 Azam FC, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wafungaji ni Anuary Jabir dakika ya 89 na Abdul Suleiman dakika ya 75 kwa Azam FC. Mabao yote yalifungwa kwa mkwaju wa penati.

Coastal Union 0-1 Mashujaa FC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mtupiaji wa bao la ushindi ni Crispin Ngushi dakika ya 87.

Namungo FC 1-3 Yanga SC, Uwanja wa Majaliwa, Lindi . Watupiaji ni Herbert Lukindo kwa Namungo FC dakika ya 75, mabao ya Yanga SC yalifungwa na Chadrack Boka dakika ya 68, Maxi Nzengeli dakika ya 71 na Peter Shalulile dakika ya 89.

Agosti 16,2026

Kagera Sugar 0-2 Simba SC, Uwanja wa Kaitaba watupiaji ni Ismail Toure dakika ya 45+2 na Elie Mpanzu dakika ya 68.

JKT Tanzania 1-1 TRA United, Uwanja wa Mej.Jen.Isamuhyo watupiaji ni Tobias Omondi dakika ya 13 na Godfrey Luzendaze dakika ya 50.

Hitimisho

Kagera Sugar 0-2 Simba SC ni mchezo wa ufunguzi kwa wababe hawa wawili. Juma Kaseja Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema watafanyia kazi makosa yaliyopita. Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuanza kwa ushindi ni jambo linaloongeza nguvu ya kujiamini.

Share this: