- Yanga SC usajili mpya 2026/27 unakaribia kukamilika ambapo, semaji Ali Kamwe ameweka wazi wamebaki Nyota wawili watakaotambulishwa kwa kishindo.
- Baada ya kutikisa na usajili wa straika wa Namibia, Peter Shalulile sasa usajili mpya ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa ni wa kiungo namba 6.
- Baada ya muda mrefu kuhusishwa na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto’ taarifa kutoka ndani ya Yanga SC zimefichua kuwa namba 6 hiyo mpya ni Fred Ngoma.
- Makala hii inakuchambua kwa ufupi kuhusu Nyota huyu raia wa Congo Brazzaville, ambaye inaelezwa tayari amekamilisha kila kitu na anasubiri utambulisho.
Mabingwa watetezi Yanga SC wanaendelea kutangaza Nyota wao wapya ambao wamekamilisha usajili, kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Hii inakuja zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026/27, ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 14. Mpaka sasa Yanga SC imekamilisha usajili na kutambulisha wachezaji 10, huku ikieleza bado kuna Nyota wawili watakaoshushwa. Miongoni mwa Sajili zinazosubiriwa kwa hamu ni mchezaji namba 6, na Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za Nyota Fred Ngoma anayetajwa ndiye Nyota mpya namba 6 wa Yanga SC.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu Yanga SC usajili mpya 2026/27 na utambulisho wa Fred Ngoma
Ngoma anatarajiwa kutambulishwa na Yanga SC akijiunga nayo kutokea klabu ya Olimpique de safi, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco. Kabla ya kutua Yanga SC Nyota huyo amefanikiwa kupita kwenye timu mbalimbali za Libya, Morocco na Congo Brazzaville. Nyota huyo anatarajiwa kuwa mchezaji wa 11 kukamilisha usajili wake na kujiunga na Yanga SC.
KUSOMA ZAIDI KUHUSU USAJILI MPYA YANGA SC 2026/27, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog
Taarifa binafsi za mchezaji
Jina : Fred Duval Ngoma
Kuzaliwa: 24/11/1997 (28)
Mahali: Pointe-Noire Congo
Urefu: 1,73 m
Uraia: Congo Brazzaville
Nafasi: Kiungo mkabaji
KUFAHAMU KUHUSU NYOTA WAPYA WAWILI WA YANGA SC, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC balaa: Ali Kamwe atangaza mashine mbili mpya, namba 6 yatikisa, je ni Feisal?
Mafanikio binafsi ya Ngoma na takwimu
Tofauti na wachezaji wanaocheza nafasi za ushambuliaji na makipa, mara nyingi mafanikio ya viungo wakabaji ni uwezo wao wa kiulinzi na kuhakikisha timu inapata matokeo. Hivyo mara nyingi mafanikio yao yanapimwa kwa ukubwa wa timu, walizochezea ligi na idadi ya michezo. Akiwa na jezi za timu mbalimbali alizopitia, Ngoma amefanikiwa kuzichezea mechi 84 akitumia dakika 6669 na kuhusika kwenye mabao 4.
KUHUSU REKODI ZA USAJILI YANGA SC, SOMA HII: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili Ecua afungua Agosti / Walioongeza mikataba/ Usajili
Kuhusu ishu ya Feisal Salum ‘Feitoto’ kutua Yanga SC
Akizungumzia uwezekano wa Yanga SC kumsajili Feitoto, Ofisa Habari wa Yanga SC Ali Kamwe amesema: “Usajili wa namba sita ndiyo usajili mkubwa tulioufanya msimu huu, tayari tumekamilisha kila kitu, kilichobaki ni siku ya utambulisho. Wanaomtaja Morice Chukwu nawaomba waondoe hofu siye tunayemzungumzia. Usajili wetu tayari umekamilika. Usajili tuliofanya msimu huu unaonyesha kiwango tulichojiwekea.
“Tumekusudia kufanya jambo kubwa na msimu huu hatukuja kutania. Feisal Salum ni mchezaji mzuri sana, lakini Yanga SC tumeshafunga usajili wetu wa ndani. Hakuna mazungumzo yoyote kati ya Yanga na Fei au Azam. Mashine mbili zilizobaki zote ni za kimataifa.”
Hitimisho
Yanga SC usajili mpya 2026/27 umekuwa kivutio cha aina yake na mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka. Wakiwa wamekamilisha usajili wa Nyota 10 mpaka sasa, usajili huu wa namba 6 unatarajiwa kuwa usajili wa 11. Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga SC huu kwao unatarajiwa kuwa usajili mkubwa zaidi, na maswali yamebaki mengi juu ya mapokezi ya Nyota huyo. Endelea kufuatilia SportPesa blog.




