- Feisal Salum kusajiliwa Simba SC dirisha kubwa la usajili tetesi zinaeleza hivyo
- Yanga SC waingilia kati dili wanaiwinda saini ya kiungo huyo wa Azam FC
- Kiungo huyo ameanza maandalizi na Azam FC iliyoweka kambi Rwanda
Feisal Salum kusajiliwa Simba SC ni tetesi ambazo zinaendelea kwa sasa kwenye dirisha la usajili. Nyota huyo amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa katika rada za timu za Kariakoo. Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwania saini ya kiungo huyo ni Yanga, Simba SC, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini zote zilikuwa zinaiwinda saini ya kiungo huyu.
Tetesi za Feisal Salum:Feisal Salum ‘Feitoto’ ashtua! tetesi za usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Feisal Salum kusajiliwa Simba SC dirisha kubwa la usajili
Mkataba wa kufuru kusaini Feitoto: Rasmi Feisal akubali kusaini mkataba wa kufuru
Kiungo Feisal Salum kusajiliwa Simba SC dirisha kubwa ambalo lilifunguliwa Julai 6,2026 na linatarajiwa kufungwa Agosti 15,2026. Zimesalia siku 4 kwa dirisha la usajili kufungwa huku ikielezwa kuwa kuna uwezekano kiungo huyo akamalizana na Simba SC.
Ikiwa Simba SC itamalizana na Feisal Salum huu utakuwa ni usajili mkubwa zaidi kufanyika kwenye dirisha la msimu huu. Kwenye wachezaji wapya waliosajiliwa na mnyama bado hakuna jina ambalo limetikisa. Jina la Feisal linatajwa kuwa kubwa kutokana na ubora wa mchezaji huyo ambaye ni mali ya Azam FC.
Hansrafael kuhusu dili la Feisal
Mchambuzi Hansrafael kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna hii: “Simba wameweka mezani ofa kubwa (haijafichuka) ambayo imeambatana na mkataba wa miaka miwili. Kuhusu Azam FC, mnyama anasubiri mauzo ya jezi yakamilike ili wavunje mkataba wa Fei na Azam. (Pia Simba wanatumia nguvu ya ziada kutoka juu ili kulainisha jambo)
“Simba wanataka Fei atambulishwe Zanzibar Agosti 12 2026 dhidi ya Yanga.Wakati huo huo tayari Fei Toto ana makubaliano binafsi na Yanga SC, ofa ya Yanga SC ina mkataba wa miaka minne wenye thamani ya tsh 3bilion (tsh 750m kila mwaka) kama Sign-on fee na wiki iliyopita GSM alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wamiliki wa Azam FC.
“Mpango wa Yanga SC ni kumsainisha mkataba,Fei Agosti 13 baada ya nyota huyo kutoka Rwanda. Simba SC na Yanga SC wako kwenye vita kali sana. Chochote kinaweza kutokea kuanzia sasa,” ameandika Hans.


