- Seleman Mwalimu ametambulishwa Yanga SC akitokea Wydad Casablanca ya Morocco
- Simba SC walikuwa kwenye mpango wa kumuongezea mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja
- Yanga SC vs Simba SC anatarajiwa kuwa kwenye kikosi 2026/27
Seleman Mwalimu ametambulishwa Yanga SC rasmi Agosti 11,2026 akitokea Wydad Casablaca. Nyota huyu alikuwa kwenye mpango wa watani za jadi Simba SC ambao walikuwa naye msimu wa 2025/26.Alifunga mabao 9 ndani ya NBC Premier League msimu uliopita akiwa unyamani.
Dili la Seleman na Yanga SC lilianza huku: Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26 | Yanga SC watajwa
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Seleman Mwalimu ametambulishwa Yanga SC, Simba SC wapishana naye

Orodha ya wachezaji Simba SC: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 | Thank You | SportPesa Blog
Surprise! Seleman Mwalimu ametambulishwa Yanga SC tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2026/27. Timu hiyo inazidi kujiimarisha kwenye eneo la ushambuliaji ikizidi kuwa na safu kali zaidi. Mwalimu anaungana na Peter Shalulile raia wa Afrika Kusini aliyewahi kucheza Mamelod Sundowns.
Simba SC wamepishana naye baada ya kumtambulisha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo. Utambulisho wa Mwalimu kusalia unyamani uliingia dosari baada ya Klabu ya Wydad Casablanca kubainisha kuwa hakuna makuliano waliyofikia. Mchezaji huyo alikuwa na Simba SC kambini Rwanda lakini hakucheza mchezo wowote wa Kagame Cup.
Alitambulishwa Simba SC Agosti 28,2025 alikuwa hapo kwa msimu mmoja 2025/26. Katika taarifa za hivi karibuni alifikia hatua ya kurejea unyamani kwa mara nyingine. Inatajwa kuwa alitarajiwa kuwa sehemu ya Simba Day, Agosti 8,2026 masuala ya makubaliano hayakufikia sehemu nzuri.

