- Hii hapa orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 katika makala haya
- Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao raia wa Mali ameshaanza kazi tayari akifungua akaunti Rwanda
- Wachezaji 10 Simba SC wamepewa Thank You akiwemo Mzamiru Yassin, Mousa Camara
Ijue orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Dirisha la usajili lilifunguliwa rasmi Julai 6,2026 linatarajiwa kufungwa Agosti 15,2026. Tayari kuna vyuma vipya vimetambulishwa unyamani mara baada ya taratibu za usajili kukamilika.
Ujue usajili mpya Simba SC: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog

Hii hapa orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27
Hatari ya mshambuliaji mpya Simba SC ipo hivi: Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC raia wa Mali | SportPesa Blog
Kuna orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 mara baada ya dirisha la usajili kufunguliwa. Miongoni mwa sehemu ambazo zimefanyiwa maboresho ni eneo la ushambuliaji akitambulishwa raia wa Mali, Ibrahim Doumbia. Nyota huyu kwenye Kagame Cup, nchini Rwanda alifungua akaunti ya mabao alipofunga dhidi ya Singida Black Stars.
Makala haya imekuletea orodha ya wachezaji wapya tayari kwa kazi. Mshambuliaji Seleman Mwalimu alitangazwa kuongeza mkataba kablaya mabosi wake Wydad Casablanca kumuhitaji kurejea katika timu yake. Ikumbukwe kwamba Agosti 8,2026 ni siku maalumu kuwatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi 2025/26. Katika wachezaji waliopewa Thank You jina la Mzamiru Yassin lipo kwenye orodha.
Makgalwa
Simba wamemtambulisha winga wa Sekhukhune United. Huyu ni raia wa Afrika Kusini,Keletso Makgalwa mwenye miaka 29.
Msimu ulipita nyota huyo alitoa asisiti 6 kwenye mechi 27 alizocheza ligi ya Afrika Kusini alitambulishwa Julai 25,2026.
Doumbia
Ibrahim Doumbia raia wa Mali ni mshambuliaji mpya alitambulishwa rasmi Julai 24 kutoka Klabu ya Association Sportive de Korofina ya Mali. Rekodi zinaonyesha kuwa alifunga msimu akiwa na mabao 17 akiwa ni mfungaji bora.
Nashon
Kelvin Nashon kiungo mkabaji alitambulishwa Simba SC rasmi Julai 19,2026. Nyota huyu mzawa msimu wa 2025/26 alikuwa Pamba Jiji FC. Tayari ameanza majukumu mapya akiwa na uzi wa unyamani.
Chilambo
Nathaniel Chilambo beki wa kulia alitambulishwa rasmi Julai 20 2026 kikosi cha Simba SC. Mbavu hii ya kulia 2025/26 ilikuwa Azam FC. Atakuwa akishirikiana na beki Shomari Kapombe ambaye ni nahodha wa timu hiyo.
Msimu
Bakari Msimu winga mpya ndani ya kikosi cha Simba SC. Nyota huyu alikuwa anakipiga ndani ya Coastal Union. Ni mzawa ambaye amebainisha kuwa amejiunga na timu hiyo kupambana kusaka matokeo mazuri.
Orodha ya wachezaji waliopewa Thank You
Mnyama Julai 16 aliandika rekodi kuachana na nyota 7 kwa mpigo. Mpaka sasa ni wachezaji 10 wameondolewa katika kikosi hicho. Miongoni mwa hao ni mshambuliaji Jonathan Sowah ambaye ametambulishwa Singida Black Stars.
Chamou Karabou
Karabou huyu ni raia wa Ivory Ivory Coast. Alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC kisha akatolewa kwa mkopo TRA United. Amepata timu mpya ambayo ni Al Talaba SC.
Naby Camara
Huyu ni raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 30. Ni kiungo wa kati. Hatakuwa kwenye kikosi cha unyamani 2026/27 baada yakupewa Thank You.
Edwin Balua
Kiungo mzawa ambaye alikuwa ni mkali kwenye mapigo huru. Alijiunga na Simba SC akitokea Tanzania Prisons ambayo imeshuka daraja. Hatakuwa kwenye kikosi cha Simba SC 2026/27.
Joshua Mutale
Kiungo mshambuliaji ambaye kiwango chake kilikuwa chakupanda na kushuka. Amekutana na Thank You jumlajumla.
Awesu Awesu
Nyota huyu alikuwa Police ya Kenya kwa mkopo.Alisajiliwa na Simba SC akitokea KMC FC inayotumia Uwanja wa KMC Complex. Kwa sasa hayupo kwenye mpango wa timu hiyo mara baada ya kupewa Thank You.
Omari Omari
Huyu ni chipukizi aliyekuwa kwenye kikosi cha Simba SC 2025/26. Hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza. Atakuwa kwenye changamoto nyingine nje ya Simba SC.
Moussa Camara
Mlinda mlango ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu msimu wa 2025/26. Hii ilitokana na kutokuwa fiti. Alikutana na Thank You rasmi Julai 16,2026.
Mzamiru Yassin
Ratiba ya Simba SC: Ratiba ya Simba SC mechi 10 za msimu mpya 2026/27 : Ligi Kuu NBC , Takwimu |Kukutana na Yanga SC ‘Kariakoo Dabi’ Oktoba 10, 2026 | SportPesa Blog
Mkongwe kwenye eneo la ukabaji huyu alikuwa ndani ya TRA United kwa mkpo. Mzamiru Yassin kiungo punda alipewa Thank You Julai 17,2026. Huyu ni mzawa mwenye kipaji halisi na imara katika mbinu za ukabaji.
Ladack Chasambi
Mtoto wa maajabu Chasambi alikutana na Thank You Julai 17,2026. Anashikilia rekodi ya kuwa mzawa aliyetoa hat trick ya asisti kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar. Ametambulishwa Singida Black Stars.
Jonathan Sowah
Simba mweusi amerejea kuwa chui kwa mara nyingine. Alikutana na Thank You Julai 17,2026. Kwa sasa yupo ndani ya Singida Black Stars huyu ni mshambuliaji.
Hitimisho
Kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 hakuna jina kubwa ambalo limekuwa gumzo. Bado dirisha la usajili halijafungwa lolote linaweza kutokea. Msimu mpya unatarajiwa kuanza Agosti 14,2026 na mchezo wa Ngao ya Jamii ni Yanga SC vs Simba SC, Agosti 12, 2026.



