Simba Day 2026 |Emmanuel Okwi, Medie Kagere kuwasha moto Uwanjani | Ali Kiba, Chino Kidd kukiwasha jukwaani

ByJoel Thomas

August 7, 2026
Okwi na Kagere Simba Day ----Okwi na Kagere Simba Day ----Okwi na Kagere Simba Day ----
  • Simba day 2026 inakuwa msimu wa 18 tangu kuanzishwa kwake, ambapo linatarajiwa kuisimamisha nchi kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru.
  • Habari kubwa kuelekea tukio hilo ni kurejea kwa ‘Malejendi’ wa timu hiyo Emmanuel Okwi na Medie Kagere ambao watashuka uwanjani.
  • Jukwaani msanii Ali Kiba ametangazwa tena kuwa ndiye ataongoza Kundi la wanamuziki watakaotumbuiza Jukwaani.
  • Makala hii inakuletea uchambuzi kwa ufupi wa kile kinachotarajiwa kutokea kwenye tamasha hilo kubwa na kongwe zaidi la michezo.

Mambo yameiva ndani ya Simba SC, kuelekea tukio kubwa la Simba day 2026. Tamasha hilo kubwa na kongwe zaidi la soka nchini Tanzania linatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi ya Agosti 8, 2026. Ikumbukwe huu unakuwa msimu wa 18 wa tamasha hili tangu kuanzishwa kwake, ambapo kwa mwaka huu limebeba dhima ya kuadhimisha miaka 90, tangu timu hiyo ianzishwe. Makala hii inachambua mambo muhimu ya kuyatarajia kwenye Simba Day 2026.

Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa-Aviator-Rain-Free-Bets----Mil-----x---

Cheza Aviator na upate nafasi ya kushinda hadi TZS milioni 800 kwa raundi.

Kuhusu tamasha la Simba day 2026

Simba Day 2026
Mo Dewji

Safari yaanzia Ngorongoro

Tukio la Simba Day 2026 lilianza katika hifadhi ya Ngorongoro, ambapo uongozi wat imu hiyo ulifanya uzinduzi wa jezi zao mpya za msimu huu wa 2026/27. Kufuatia uzinduzi huo Mkurugenzi wa kampuni iliyo na dhamana ya uzinduzi wa jezi hizo, Joekl Rwegasira alisema: “Tumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa sababu haijawahi kutokea binadamu yoyote ambaye amashawahi kuwa shabiki wa Simba, kushuhudia miaka 90 ya Simba Sports Club. Sisi leo tumeweza kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu yetu, wengi walitamani kufika leo lakini hawakuweza, sisi tumefika.

“Niwashukuru Wanasimba, wamekuwa watu wakuisapoti klabu yetu kipindi chote. Hii inaonyesha kwamba ile Nguvu Moja haitokei mdomoni, bali kwenye chemchemi ya mioyo yao. Watu wanlijiuliza jezi ya mwaka huu itakuwa kali kuliko ya msimu ya msimu uliopita? Wote mmeona jezi ya sasa ni ya kuotea mbali.”

Utaratibu wa kuchangia damu

Kama ilivyo kawaida yao kama sehemu ya kutekeleza tukio la wiki ya Simba na Simba day, uongozi na mashabiki walifanya tukio la kuchangia damu. Tukio la kuchangia damu liliongozwa na Rais wa heshima wa Simba SC , Mohammed Dewji. Matukio kama hayo yalifanyika kote nchini.

Ali Kiba kuongoza burudani jukwaani

Baada ya kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika tamasha la Simba Day 2023, akiwa kama msanii namba moja hatimaye staa wa bongo fleva, Ali Kiba anatarajia kuongoza tena jukwaa la Simba Day 2026. Ali Kiba anatarajiwa kutumbuiza nyimbo zake bora ikiwemo nyimbo ya Mnyama. Pamoja naye wasanii wengine wengi wanatarajia kushusha shoo kubwa, akiwemo Chino Kidd na bendi ya Twanga Pepeta.

Semaji Ahmed ataingiaje?

Ahmed Ally Simba
Ahmed Ally Simba

Kila mwaka kumekuwa na bunifu mbalimbali ambazo amekuwa akizitumia Meneja wa Habari na mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally kuingia uwanjani. Sasa kuelekea tukio la mwaka huu Semaji amesema atatumia mtindo wa sayansi ya aina yake, ya kutumia ‘ungo’. Je, atatimiza Ahadi yak, au alikuwa anatania? Tutaona kesho Jumamosi.

KUHUSU SIMBA DAY 2025, SOMA HII: Simba Day 2025 ni viwango vingine | John Bocco na Mkude kuagwa rasmi | Ijue ratiba na matukio muhimu

Okwi, Kagere kuteka shoo

Malejendi wawili wa Simba SC, Medie Kagere na Emmanuel Okwi wanatarajiwa kuwa kivutio kikukbwa kesho. Hii ni pale watakaposhuka uwanjani katika Mchezo wa utangulizi wa viongozi wa Simba SC na wadau.

Ni Simba SC vs Polisi FC

Kama sehemu ya kukamilisha tukio hilo, Simba SC wanatarajiwa kucheza Mchezo mkali wa kirafiki dhidi ya Polisi FC ya Kenya. Mchezo huu unatarajiwa kutumika kama sehemu ya kutesti mitambo, na utambulisho wa kikosi cha msimu huu mpya. Baada ya Mchezo huu Simba watakuwa wanajiandaa kuvaana na Yanga SC katika ngao ya jamii.

Meena Ally, Adam Mchomvu kuongoza washereheshaji

Simba Day
Simba Day

Watangazaji Meena Ally na Adam Mchomvu wanatarajiwa kuongoza listi ya washereheshaji wa tukio hilo. Wengine ni MC Petit n.k. Hawa wote wanatarajiwa kuvamia jukwaa hilo kuhakikisha watu wanaburudika.

KUHUSU KUMBUKUMBU YA SIMBA DAY 2025, SOMA HII: Simba Day Septemba 10 2025 fullhouse mapema | Matukio yalibamba

Hitimisho:

Simba day 2026 ni tukio la kihistoria ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wat imu hiyo, na wadau wa soka nchini. Haya ni maandalizi rasmi ya msimu mpya na utimilifu wa tamaduni ya timu hiyo. Ikiwa inaingia katika msimu wa 18, wengi wanatamani kuona kutakuwa na kitu gani cha tofauti. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.