- Kuelekea Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026 mambo ni moto huku Sold Out zikitangazwa mapema kabla ya shughuli
- Yanga SC vs Aigles du Congo mchezo mkali wa kirafiki utachezwa Uwanja wa Uhuru
- Peter Shalulile mshambuliaji mpya raia wa Afrika Kusini, Farouk Komara ni miongoni mwa wachezaji wapya watakaotambulishwa
Ni Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026 imepamba moto kutokana na matukio ambayo yanaendelea kabla ya kilele cha tamasha lenyewe. Agost 9,2026 itakuwa kilele cha tamasha huku Yanga SC vs Aigles du Congo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watashuka uwanjani. Mbali na mchezo huo wa kimataifa kutakuwa na utambulisho wa wachezaji wapya na benchi la ufundi.
Wajue wachezaji wapya wa Yanga SC: Usajili Yanga SC 2026/27: Hawa hapa wachezaji wapya 5 wazawa
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Matukio makubwa Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026

Namba 6 yatikisa Yanga SC: Usajili mpya Yanga SC balaa: Ali Kamwe atangaza mashine mbili mpya, namba 6 yatikisa, je ni Feisal?
Kuna matukio makubwa Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026 yanatarajiwa kuratibiwa kwa umakini mkubwa. Hii inatokana na mwitikio katika kila hatua ambayo walikuwa wanapitia. Ikumbukwe kwamba miongoni mwa majukumu ambayo yamefanyika ni kuchagia damu, kutembea vituo vya wenye mahitaji maalumu. Pia jezi mpya ya Yanga SC imetambulishwa rasmi. Hapa tunakuletea matukio makubwa yanayosubiriwa kwenye kilele namna hii:-
Utambulisho wa wachezaji wapya
Yanga SC imefanya usajili mkubwa kwenye kila idara. Ambacho mashabiki wanasubiri ni namna ambavyo mastaa hao watatambulishwa uwanjani kwa mara ya kwanza. Kuna baadhi ya wachezaji wapya wanaosubiriwa kwa shauku hawa hapa:-
Farouk Komara
Alitambulishwa Agosti 4,2026. Huyu ni mali ya Yanga SC. Ni raia wa Ivory Coast kitasa mwenye uwezo wa kucheza kiungo mkabaji. Ana umri wa miaka 26 alikuwa Klabu ya Golden Arrowsya Afrika Kusini kabla ya kutambulishwa Jangwani.
Peter Shalulile
Mshambuliaji wa zamani wa Mamelod Sundowns alitambulishwa Yanga SC, Julai 27,2026.Ni kandarasi ya miaka miwili amesaini. Yupo Dar tayari amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Albert Kangwanda
Huyu ni MVP wa Zambia,Albert Kangwanda. Msimu uliopita alifunga mabao 17 na asisti 9 amesaini dili la miaka miwili. Amecheza Al Hilal Omdurman ya Sudan, CSF Spartanii (Moldava), HNK Gorica, (Croatia) na Red Arrows ya Zambia. Julai 24 2026 alitambulishwa
Cheikh Touré
Nyota huyu amewahi kupita kwenye vilabu vya AS Nancy ya Ufaransa na Al-Jabalain ya Saudi Arabia. Julai 24 2026 alitambulishwa. Ana umri wa miaka 29.
Yanga SC vs Aigles du Congo mechi ya kimataifa
Mchezo mkali wa kimataifa unasubiri kuwashuhudia wachezaji wote wakiwa kazini kwa mara ya kwanza. Ni Yanga SC vs Aigles du Congo mechi ya kimataifa ya kirafiki. Wababe hawa watamenyana katika dakika 90 kusaka ushindi.
Sababu kubwa ya mchezo huu kuwa moja ya matukio muhimu ni uwepo wa wachezaji wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi msimu uliopita. Benchi zima la ufundi ambalo nalo ni jipya litaonyesha hadharani mbinu. Huu utakuwa ni mwanzo kuelekea msimu mpya wa 2026/27.
Uzi mpya wa Yanga SC
Mara baada ya Yanga SC kutambulisha uzi mpya tayari mashabiki wameendelea kununua kwa wingi. Uwepo wa mashabiki uwanjan utaonyesha picha halisi ya walionunua uzi mpya. Hapa itafahamika ni jezi ipi ambayo imekubalika zaidi mara baada ya kutambulishwa na kuwa sokoni.
Full House Uwanja wa Uhuru
Sold Out zimezidi kutembea kutokana na mashabiki kununua kwa wingi tiketi za tamasha la Yanga Day. Royal rasmi ni Sold Out na VIP pia. Asilimia ndogo imebaki kukamilisha Sold Out kwenye jukwaa la mzunguko.
Bei ilikuwa namna hii upande wa viingilio: Royal 300,000, VIP 100,000 na mzunguko 20,000. Hivyo kuna uwezekano mkubwa Agosti 9,2026 ikiwa ni Full House.
Hitimisho
Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026 inasubiriwa kwa shauku kubwa kabla ya pazia la NBC Premier League kufunguliwa. 2025 tamasha lilifanyika Uwanja wa Mkapa ambao kwa sasa unafanyiwa maboresho. Mashabiki wamekuwa na mwitikio mkubwa kutokana na hamasa ambazo zinafanyika.

