Uwanja wa MkapaUwanja wa Mkapa
  • Simba SC ilirejesha kwa jamii ikiwa ni matukio muhimu ambayo yalifanyika katika Simba Week.
  • Simba Day Septemba 10 2025 sold out zimetangazwa mapema siku mbili kabla ya jambo lenyewe kufanyika.
  • Mchezo wa kirafiki wa kimataifa Simba SC vs Gor Mahia utanogesha burudani huku wasanii wakubwa wakitarajiwa kupanda jukwaani.

Simba Day 2025 Septemba 10 2025 ni mwendo wa soldout. Mashabiki wamenunua tiketi zote ikiwa ni siku mbili kabla ya tamasha kubwa Uwanja wa Mkapa. Hii inamaanisha itakuwa ‘FullHouse’ ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Simba Day
Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasilino Simba SC.

Soma hii: Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC: highlight, vikosi, h2h, Ubaya Ubwela Part 2 moto utawaka!

Paisha kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Rahisi sana kwa kila rubani ambaye anapaisha Kindege cha SportPesa. Kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

Simba Day 2025 mchezo wa kirafiki wa kimataifa kuchezwa

Simba Day ni tamasha maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi. Katika tamasha hilo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Simba SC vs Gor Mahia watakutana uwanjani.

Mashabiki wamenunua tiketi kwa wingi mara baada ya siku ya tamasha kutajwa. Simba SC ilikuwa na kampeni nyingi zilizofanyika. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC alikuwa anasimamia shughuli zote.

Ratiba ya Simba Week ilikwenda namna hii

Septemba 2, 2025 ilikuwa ni siku ya kitaifa Wanasimba kuchangia damu kwenye hospitali mbalimbali. Kwa mujibu wa Ahmed Ally aliweka wazi kuwa ni muhimu kujitoa kwa ajili ya jamii. Hilo lilifanyika kwa mashabiki wa Simba SC Tanzania nzima.

 “Tuna wajibu wa kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu. Hapa Dar es Salaam tutakuwa na vituo mbalimbali vya kutolea damu. Na wale wa mkoani nao ni muhimu kufanya hivyo.

“Septemba 3, 2025 kutakuwa na droo ya bonanza. Mwaka jana mmnakumbuka tulikuwa na bonanza lilishirikisha matawi. Na mwaka huu tutarudisha tena na linahusisha matawi yote ya Simba Sports Club.

Katika tamasha hilo bingwa alikuwa ni Mpira Pesa. Mshindi alitwaa taji na zawadi ya fedha shilingi milioni mbili. Ni TemboCard Simba Matawi Bonanza ilifanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga.

Mpira Pesa ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Nguvu ya Simba. Katika mashindano hayo CEO Zubeda Sakuru alikuwepo. Nusu fainali ilikuwa Kamati ya Roho Mbaya 0-0 Nguvu ya Simba na penati ilikuwa Kamati ya Roho Mbaya 10-11 Nguvu ya Simba.


Septemba 4, 2025 ilikuwa ni siku ya kuzindua matawi. Ahmed Ally alizindua matawi zaidi ya mawili. Miongoni mwa matawi ambayo yalizinduliwa ni tawi la Simba la VIP A Magomeni.

Septemba 5, 2025 ilikuwa ni biryan day. Siku hiyo Simba SC ilirejesha kwa jamii kwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha Umra. Kituo hicho kipo Magomeni, Dar.

 Ahmed Ally alisema: “Tunarejesha kwa jamii kwa kuwa ukiwa unakula na yatima unapata baraka. Huu ni utamaduni wetu Simba SC. Tutaendelea kufanya hivyo kila wakati ni baraka.

Hii hapa ilikuwa bei ya viingilio

Viingilio mzunguko Tsh. 7,000, VIP C – Tsh. 20,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP A – Tsh. 100,000, Platinum – Tsh. 250,000, Tanzanite – Tsh. 350,000.

Tayari imeshatangazwa tiketi zote zimeisha. Hivyo kilichobaki kwa sasa ni mashabiki kujitokeza uwanjani. Huu unakuwa mchezo wa kwanza wa ushindani wa Simba SC, Uwanja wa Mkapa baada ya kutoka kambini Misiri.

Orodha ya wasanii watakaotoa burudani

Kuna orodha kubwa ya wasanii watakaotoa burudani Simba Day. King Kiba, Ali Kiba anatarajiwa kuwa msanii kiongozi wa wasanii wote. Hii inatokana na kazi yake anayofanya kukubalika kwa jamii.

Msanii Wizzy MP, Joh Makini, Mboso amethibitisha kuwa atakuwepo. Hivyo kutakuwa na burudani kubwa uwanja wa Mkapa.

Wachezaji Simba SC kamili

Mpanzu Misri (-)
Mpanzu winga wa Simba SC.

Soma hii: Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na Jonas Mkude kupewa tuzo Simba Day

Septemba 9 2025 wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa. Miongoni mwa wachezaji hao ni Ellie Mpanzu Jonathan Sowah, Joshua Mutale. Awesu Awesu, Jean Ahoua. Mzamiru Yassin, David Kameta.

Fadlu Davids azungumzia Simba Day

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amebainisha kuwa ni tamasha kubwa. Wapo tayari kuwapa burudani mashabiki. Aliongeza kuwa wanawaheshimu wapinzani.

Simba SC vs Gor Mahia FC
Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC.

Soma hii: Simba Day 2025 msimu wa 17 viwango vingine

“Simba Day ni tamasha kubwa. Tupo tayari kwa ajili ya kutoa burudani. Mashabiki wajitokeze kwa wingi.”

Hitimisho

Simba Day ya msimu huu inakuwa ni ya 17. Utachezwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia. Mashabiki wanasubiri kwa shauku kuwaona wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25.

image
Share this: