- Simba Day msimu wa 17unatarajiwa kuwa na upekee mkubwa na uzinduzi wake itakuwa mkoano Iringa, wilayani Mafinga.
- Nahodha mstaafu John Bocco na kiungo mkabaji Jonas Mkude kupewa tuzo za heshima Uwanja wa Mkapa.
- Ubaya Ubwela no 2 ni kaulimbiu ya Simba SC, matukio makubwa kuelekea kilele cha Simba Day Septemba 10 2025.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema Simba Day msimu huu itakuwa ya viwango. Tamasha hilo ni maalumu kwa utambulisho wa wachezaji, benchi la ufundi na jezi zitakazotumika msimu wa 2025/26. Pia wachezaji wawili wataagwa rasmi ambao ni John Bocco na Jonas Mkude.
Shinda mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa
Ni rahisi sana wiki hii kushinda mamilioni sasa hivi. Unachotakiwa kufanya ni kupaisha Kindege cha SportPesa. Cheza Aviator upate mgao wako.

Kuhusu Simba Day kuwa Septemba badala ya Agosti

Soma hii: Kitaumana Uwanja wa Mkapa Agosti 3 2024 Uwanja wa Mkapa
Ahmed amesema: “Wote mnakumbuka tulitangaza kwamba Septemba 10, 2025 itakuwa Simba Day. Mnafahamu mara nyingi Simba Day inafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane. Lakini kutokana na kubanana kwa ratiba na hasa mashindano ya CHAN imefanya imesogea hadi mwezi wa tisa.
“ Mwezi wa tisa haikuwa rahisi kupata tarehe sababu ya ratiba. Kuanzia tarehe moja hadi nane ni kalenda ya FIFA, kwa mujibu wa kalenda ya TFF ilionyesha Ngao ya Jamii ilikuwa Septemba 11-14, 2025. Haikuwa na namna nyingine zaidi ya kuiweka Simba Day katikati ya wiki.
“Fanya shughuli zako maliza, Septemba 10, 2025 tunakuhitaji uwanja wa Mkapa. Hii siku haihitaji sababu, hakikisha unakuja uwanjani. Kwa kawaida Simba Day inakuwa na mfululizo wa matukio ambayo yanaunda Simba Week. Yapo matukio ya kibiashara, yapo ya kijamii, yapo matukio ya aina mbalimbali kunogesha wiki ya Simba.
“Katika msimu huu wa 17 wa Simba Day, utazinduliwa rasmi Agosti 30, 2025. Kama ambavyo tumeanzisha utamaduni wa kufanya uzinduzi wa Wiki ya Simba nje ya jiji la Dar es Salaam basi na mwaka huu itakuwa hivyo. Mwaka jana ilikuwa Morogoro na mwaka huu tutazindua mkoani Iringa kwenye wilaya ya Mafinga.
“Tutaondoka Dar 30/08/2025 na uzinduzi rasmi utafanyika Agosti 31, 2025 kwenye viwanja vya Mafinga vilivyopo Mafinga Mjini. Kutakuwa na burudani za kutosha na shangwe kubwa vibaya mno.
Mpango wa dua kwa Hans Poppe
“Lakini pia tunaangalia uwezekano mkubwa na tumeshaanza kufanya maandalizi ya kwenda kufanya dua kwenye kaburi la mmoja wa aliyekuwa kiongozi wetu, Zacharia Hans Poppe. Baada ya uzinduzi wa Wiki ya Simba Agosti 31, 2025 tutarejea Dar es Salaam. Septemba mosi, 2025 itakuwa ni mapumziko kuondoa uchovu.
Ratiba ya Septemba Simba Week ipo hivi

Soma hii: Simba Day Septemba 10 2025
“Septemba 2, 2025 ni siku ya kitaifa ya Wanasimba kuchangia damu kwenye hospitali mbalimbali. Tuna wajibu wa kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu. Hapa Dar es Salaam tutakuwa na vituo mbalimbali vya kutolea damu.
“Septemba 3, 2025 kutakuwa na droo ya bonanza. Mwaka jana mmnakumbuka tulikuwa na bonanza lilishirikisha matawi. Na mwaka huu tutarudisha tena na linahusisha matawi yote ya Simba Sports Club. Matawi yote ambayo yanataka kushiriki tutawapa namba ya kutuma jina lenu kushiriki. Tunafanya hivi ili kutengeneza umoja na upendo kwenye matawi ya Simba.
“Septemba 4, 2025 ni siku ya matawi, tunafahamu yapo matawi mengi yanahitaji kuzinduliwa. Tayari tuna matawi mawili hapa. Kama kuna mwingine amekamilisha utaratibu wote awasiliane na mkurugenzi wa Wanachama wa Simba.”
“Septemba 5, 2025 itakuwa ni biryan day. Tutakwenda kupata lunch kwenye kituo cha watoto yatima ambacho tutakichagua na kukitangaza, tutawapa taarifa. Tunafanya hivi kurudisha kwa jamii lakini pia kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Ukikaa na watoto wale yatima mkagonga biryan watoto wanafurahi wanaomba dua na Simba tunaneemika. Tarehe 5 njoo na njaa yako utashiba kwenye biryan la Simba Sports Club.
“Septemba 6, 2025 kutakuwa na bonanza tutafanyia kwenye viwanja vya Mwembe Yanga. Septemba 7, 2025 itakuwa Simba Day Fun Run hii itakuwa siku maalumu. Baada ya kufanya bonanza itakuwa ni malaumu Wanasimba kukimbia au ukiamua hata kutembea. Mbio zetu zitaanzia round about ya Agha Khan, tutapita daraja la Tanzanite, tutapita Coco Beach hadi Sea Cliff alafu tutarudi Coco Beach. Kiingilio pekee ni jezi yako mpya ya msimu huu.
“Septemba 8, 2025 tutarudisha kwa jamii tukiwa na timu nzima kuanzia wachezaji, makocha na viongozi wa Simba SC tutakwenda kutoa msaada kwenye kituo pendekezwa cha watoto yatima. Septemba 9, 2025 itakuwa kufanya mazoezi, kuongea na waandishi wa habari kuelekea Simba Day. Niwambie tu hii ni Simba Day ya 17 ambayo hakuna Mwanasimba yeyote ambayo amewahi kuiona kuanzia mpangilio wa matukio hadi timu yetu ilivyo bora. Mwanasimba ataondoka uwanjani anafika hadi anapokwenda akiwa anacheka.
Viingilio hivi hapa
“Viingilio ni Mzunguko – Tsh. 7,000, VIP C – Tsh. 20,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP A – Tsh. 100,000, Platinum – Tsh. 250,000, Tanzanite – Tsh. 350,000.”
Mkude na Bocco kuagwa rasmi

John Raphael Bocco zama akiwa na uzi wa Simba SC.
Soma hii: Simba panga likipita, ‘fungafunga’ aombewa 2024/25
“Mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika na kuwatunza wachezaji wa zamani ambao wamefanya makubwa na tutawapa tuzo ya heshima. Wachezaji hawa ni John Bocco lakini vile vile tutakwenda kumuaga nahodha wetu mwingine ambaye ameitumikia Simba SC kwa miaka 15, Jonas Gellard Mkude na tutaendelea kuwaaga malenge wetu taratibu taratibu tutakapopata nafasi. Mnayemsubiri tutamuaga akishamaliza kuchukua pension yake,” alimaliza Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC.
Hitimisho
Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kurejea Agosti 28, 2025. Kwa sasa kipo kambini Misri. Kauli mbiu ni Ubaya Ubwela no 2.


