Switzerland vs ColombiaSwitzerland vs Colombia
  • Switzerland vs Colombia FIFA Kombe la Dunia 2026, ni ratiba ya mechi kali inayotarajiwa kupigwa usiku wa Jumanne 7 July 2026, saa 5 kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa BC Place Vancouver, huko Vancouver Canada.
  • Switzerland ya mkongwe Granit Xhaka na mlinzi Manuel Akanji wataongoza mapambano dhidi ya Colombia ya Luis Diaz na James Rodriguez.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

Switzerland watashuka tena usiku wa Jumanne, kuvaana na Colombia katika mchezo mkali wa hatua ya 16 bora ya FIFA Kombe la Dunia 2026. Mechi hii itapigwa saa tano usiku wa Jumanne 7 July 2026, katika Uwanja wa BC Place Vancouver nchini Canada. Hii ni vita kati ya majina makubwa ikiwemo; Granit Xhaka na Manuel Akanji wa Switzerland, dhidi ya Luis Diaz na James Rodriguez wa Colombia. Hapa tunachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Switzerland vs Colombia

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Switzerland vs Colombia
Switzerland vs Colombia

Maelezo ya Mechi

Switzerland vs Bosnia (-)
Switzerland kwenye WC 2026
KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo huu ni sehemu ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo mfumo wa mtoano unatumika. Timu itakayopata ushindi itafuzu moja kwa moja kwenda robo fainali, huku timu itakayopoteza ikiondolewa rasmi kwenye mashindano.
Tarehe na MudaMechi imepangwa kuchezwa Jumanne, tarehe 7 Julai 2026, kuanzia saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
UwanjaTimu hizo zitakutana katika Uwanja wa BC Place uliopo Vancouver, Canada. Uwanja huu ni mmoja wa viwanja rasmi vinavyotumika kuandaa michezo ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kutokana na miundombinu yake ya kisasa na uwezo mkubwa wa kuhudumia mashindano ya kimataifa.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 8 ZA HATUA YA 16 BORA, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora | Mechi zote 8 | Utabiri | Odds kubwa | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa Switzerland vs Colombia FIFA Kombe la Dunia 2026

Uswisi na Colombia zitamenyana katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, utakaochezwa Jumanne jioni jijini Vancouver. Timu zote mbili zinaingia kwenye mchezo huu, zikiwa hazijapoteza hata mechi moja katika mashindano haya, jambo linaloweka mazingira ya pambano kali. Switzerland ilitinga hatua hii baada ya kuifunga Algeria mabao 2-0 katika hatua ya 32 Bora, huku Colombia ikiiondoa Ghana kwa ushindi wa bao 1-0.

Hadi sasa Colombia imeruhusu bao moja pekee, ikiwa ndiyo timu yenye safu bora zaidi ya ulinzi kwenye mashindano haya. Switzerland itakuwa na kazi ngumu kuvunja safu ya ulinzi ya Colombia, lakini nao wanajivunia rekodi ya ukali wa kufunga mabao. Ikumbukwe Colombia imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu, kati ya mechi tatu ilizocheza katika hatua ya 16 Bora kwenye historia yake.

KUANGALIA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA USA: Prediction | USA vs Belgium FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, Ratiba, Live score, h2h, odds na habari za timu

Habari za timu na majeruhi

Switzerland wana pigo kubwa ambapo watawakosa Denis Zakaria na Luca Jaquez, ambao wote wanaendelea kuuguza majeraha. Hata hivyo, timu hiyo inaendelea kunufaika na kiwango bora cha chipukizi Johan Manzambi, ambaye tayari amehusika katika mabao matano kwenye Kombe hili la Dunia. Kwa Colombia, bado hakuna taarifa rasmi ya majeruhi wapya.

Vikosi vinavyotarajiwa Switzerland vs Colombia

Switzerland

NafasiMchezaji
KipaGregor Kobel
Beki wa KuliaDenis Zakaria
Beki wa KatiNico Elvedi
Beki wa KatiManuel Akanji
Beki wa KushotoRicardo Rodríguez
Kiungo wa KatiRemo Freuler
Kiungo wa KatiGranit Xhaka
Winga wa KuliaDan Ndoye
Kiungo MshambuliajiJohan Manzambi
Winga wa KushotoRubén Vargas
MshambuliajiBreel Embolo

Colombia

Switzerland vs Colombia FIFA Kombe la Dunia 2026
Kikosi cha Colombia
NafasiMchezaji
KipaCamilo Vargas
Beki wa KuliaDaniel Muñoz
Beki wa KatiDavinson Sánchez
Beki wa KatiJhon Lucumí
Beki wa KushotoJohan Mojica
Kiungo wa KatiGustavo Puerta
Kiungo wa KatiJefferson Lerma
Kiungo wa KatiJhon Arias
Winga wa KuliaJames Rodríguez
MshambuliajiJhon Córdoba
Winga wa KushotoLuis Díaz

Rekodi ya Switzerland vs Colombia h2h

Switzerland vs Canada FIFA Kombe la Dunia 2026
Switzerland

Timu hizi zimekutana mara tatu katika historia yao na hakuna hata mechi moja iliyomalizika kwa sare. Colombia imeshinda mara mbili, huku Uswisi ikishinda mchezo mmoja. Mchezo huu ni nafasi ya kuandika rekodi mpya. Jedwali hapo chini linachambua rekodi hizi;

MchezoMatokeo
25 Machi 2007Colombia iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uswisi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
27 Juni 1994Colombia iliifunga Uswisi 2-0 katika mechi ya hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la FIFA 1994.
4 Februari 1991Uswisi iliichapa Colombia kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliokuwa na ushindani mkubwa.

Utabiri wa mechi (magoli zaidi ya mawili, yaani over 1.5)

Diaz (-)
Diaz

Hapa ni vita katia timu iliyo na rekodi bora zaidi ya kufunga, dhidi ya timu iliyo na rekodi bora zaidi ya kuzuia hivyo mchezo mgumu unatarajiwa. Kila timu hapa ina uwezo wa kufunga angalau bao moja, hivyo ubashiri wetu ni wa matokeo ya jumla ya mabao 2 au zaidi yaani over 1.5. Ikumbukwe huu ni utabiri unaotokana na maoni ya kiuhariri, sio matokeo halisi hivyo chambua mkeka wako na bashiri kistaarabu.

KUJUA KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA PORTUGAL, SOMA HII: Prediction Portugal vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, h2h, odds na habari za timu

Hitimisho

Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaonyesha tunatarajia mchezo mgumu sana, lakini jambo moja ambalo linaonekana rahisi kubashirika ni uwezekano wa kutokea mabao. Ubashiri wetu na maoni ya uhariri ni uwezekano wa kupata mabao 2 au zaidi, kwani timu zote zina uwezo mzuri wa kufunga mabao. Licha ya matarajio hayo, pia inatarajiwa mchezo utakuwa mgumu, fuatilia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.