- USA vs Belgium FIFA Kombe la Dunia 2026, ni mechi kali inayotarajiwa kupigwa usiku wa saa tisa kwa saa za Afrika Mashariki kuamkia Jumanne 7 July 2026.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Lumen Field au Seattle, huko Seattle, USA.
- USA wakiongozwa na mastaa Christian Pulisic na Weston McKennie, watapambana uso kwa uso na Belgium ya Jeremy Doku na Lomelo Lukaku.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Timu ya Taifa ya USA ambayo imekuwa na moto wa kuotea mbali katika mashindano ya FIFA Kombe la Dunia 2026, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ubelgiji. Mechi hii itapigwa saa tisa usiku wa kuamkia Jumanne 7 July 2026, katika Uwanja wa Seattle nchini Marekani. Mchuano huu ni vita ya timu iliyoanza kwa nguvu kubwa ya wenyeji USA, dhidi ya timu iliyokuwa na nyakati za kusuasua ya Belgium. Hapa tunachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya USA vs Belgium
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo (Yaliyoboreshwa na ya Kipekee) |
|---|---|
| Mashindano | Huu ni mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Timu zote mbili zinapambana katika mfumo wa mtoano, ambapo mshindi ataendelea hadi hatua ya robo fainali huku timu itakayoshindwa ikimaliza safari yake kwenye mashindano. |
| Tarehe na Muda | Mechi inatarajiwa kuchezwa saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, usiku wa kuamkia Jumanne, tarehe 7 Julai 2026. Kwa muda wa eneo la Seattle, Marekani, mchezo utaanza Jumatatu, tarehe 6 Julai 2026. |
| Uwanja | Pambano hili litachezwa katika Uwanja wa Seattle ulioko jijini Seattle, Marekani. Uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vilivyochaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo mbalimbali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 8 ZA HATUA YA 16 BORA, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora | Mechi zote 8 | Utabiri | Odds kubwa | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa USA vs Belgium FIFA Kombe la Dunia 2026

Harakati za Marekani (USA), kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002 zitaendelea Jumatatu watakapovaana na Ubelgiji. Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Lumen Field jijini Seattle. USA ambao ni waandaaji wenza wa Kombe la Dunia 2026, walifuzu hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Bosnia na Herzegovina mabao 2-0. Ubelgiji wao walipata nafasi ya kucheza 16 bora baada ya kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Senegal.
Mafanikio makubwa zaidi ya Marekani kwenye Kombe la Dunia, ni yale ya kumaliza nafasi ya tatu mwaka 1030. USA iliyo chini ya kocha, Mauricio Pochettino kilimaliza kileleni mwa Kundi D kwa pointi 6 na kufuzu hatua ya 32 Bora. Katika hatua hiyo waliichapa Bosnia na Herzegovina kwa mabao 2-0.
Mshindi wa mechi ya USA vs Belgium atavaana na mshindi wa mechi ya Portugal vs Spain katika hatua ya Robo Fainali. Mara ya mwisho kwa USA kuvaana na Belgium ilikuwa Machi 2026, ambapo Ubelgiji iliibuka na ushindi mkubwa wa mabao 5-2. Kwa upande wa Ubelgiji, wao walimaliza kileleni mwa Kundi G, kwa kukusanya pointi 5 na kuvaana na Senegal, ambao waliwachapa 3-2.
KUANGALIA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA ARGENTINA: Prediction Argentina vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, h2h, odds, habari za timu
Habari za Timu na majeruhi
Marekani walipata pigo baada ya straika wao hatari, Folarin Balogun kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bosnia na Herzegovina. Staa huyo tayari amefunga mabao matatu katika Kombe hili la Dunia. Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Ricardo Pepi, ambaye ameifungia Marekani mabao 13 katika mechi 41 alizoichezea timu ya taifa.
Nyota wengine, Mark McKenzie (jeraha la mguu) na Cristian Roldan (jeraha la misuli) watafanyiwa tathmini kabla ya mchezo, kujua ikiwa watapatikana. Kwa upande wa Ubelgiji, staa wao, Zeno Debast yuko kwenye hatihati ya kutocheza, kutokana na jeraha la mguu. Leandro Trossard yuko fiti licha ya hofu ya majeraha, huku Kevin De Bruyne na Jeremy Doku wakitarajiwa pia kuanza katika kikosi cha kwanza cha Ubelgiji.
Vikosi Vinavyowezekana
USA

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Matt Freese atalinda lango la timu, akitarajiwa kuonyesha utulivu, umakini na uwezo wa kuanzisha mashambulizi kutoka eneo la nyuma. |
| Mabeki | Safu ya ulinzi itaundwa na Freeman, Richards, Ream, na Robinson, wakiwa na jukumu la kuzuia mashambulizi ya wapinzani huku wakisaidia kujenga mchezo kutoka nyuma. |
| Viungo | Eneo la kiungo litahusisha Tillman, Adams, na McKennie, ambao watasimamia umiliki wa mpira, kulinda safu ya ulinzi na kuunganisha mchezo kati ya mabeki na washambuliaji. |
| Washambuliaji | Mbele kutakuwepo Dest, Pepi, na Pulisic, wakilenga kutumia kasi, ubunifu na umaliziaji mzuri ili kutengeneza na kufunga mabao. |
Ubelgiji
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Thibaut Courtois anatarajiwa kuanza langoni, akitegemewa kutumia uzoefu wake, uwezo wa kuokoa michomo hatari na kuiongoza safu ya ulinzi. |
| Mabeki | Safu ya ulinzi itajumuisha Castagne, Theate, Mechele, na De Cuyper, ambao watakuwa na jukumu la kuzuia mashambulizi ya wapinzani huku wakichangia katika ujenzi wa mashambulizi kutoka nyuma. |
| Viungo | Eneo la kiungo litaundwa na Vanaken na Tielemans, wakisimamia umiliki wa mpira, kusambaza pasi na kuleta uwiano kati ya ulinzi na ushambuliaji. |
| Washambuliaji wa Pembeni | Trossard, De Bruyne, na Doku wanatarajiwa kuongoza mashambulizi kutoka maeneo ya mbele kwa kutumia ubunifu, kasi na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao. |
| Mshambuliaji | Charles De Ketelaere ataongoza safu ya ushambuliaji, akilenga kutumia nafasi zitakazotengenezwa na wachezaji wa nyuma yake ili kutikisa nyavu. |
Utabiri (mabao zaidi ya 2, yaani over 2.5)
Huu ni mchezo mgumu sana kutabiri, na haitakuwa ajabu kama utamalizika kwa mikwaju ya penalti. Hata hivyo, timu zote mbili zimeonyesha wastani mkubwa wa kufunga mabao, hivyo huenda ikashuhudiwa mabao mengi, angalau mabao 3 na zaidi. Ikumbukwe utabiri huu sio matokeo halisi, hivyo Bashiri kistaarabu.
KUJUA KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA BRAZIL, SOMA HII: Prediction Brazil vs Norway FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, h2h, lineups, team news
Rekodi ya USA vs Belgium H2H

Timu hizi zimekutana mara 7 katika mashindano tofauti na mechi za kirafiki, ambapo Belgium amekuwa na rekodi bora zaidi akishinda mechi 6. USA ameshinda mchezo mmoja pekee na hakuna rekodi ya matokeo ya sare wanapokutana. Je nini kitatokea katika mchezo huu? Mashabiki wanasubiri dakika 90 za mechi.
Hitimisho
Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaonysha tunatarajia mchezo mgumu sana, lakini jambo moja ambalo linaonekana rahisi kubashirika ni uwezekano wa kutokea mabao mengi. Ubashiri wetu na maoni ya uhariri ni uwezekano wa kupata mabao zaidi ya 2, kwani timu zote zina wastani mzuri wa kufunga mabao. Licha ya matarajio hayo, pia inatarajiwa mchezo utakuwa mgumu, fuatilia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

