Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwaDj Zee
  • Ni Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa wakipita kwa watani wa jadi Simba SC mtaa wa Msimbazi
  • Mara 5 mfululizo wamefanikiwa kutwaa taji hilo mdhamini mkuu ni SportPesa kampuni yenye odds kubwa katika kubashiri
  • Prince Dube amewaaga rasmi mashabiki na wachezaji baada ya kuwa na kikosi 2025/26

Ni mwendelezo wa historia, Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa Jangwani Julai 4, 2026. Huu ni ubingwa wa 32 kwa timu hiyo. Parade la mabingwa lilianza mapema saa 4;00 asubuhi. Ni mtaa wa Karume- Msimbazi-Jangwani ambapo kuliandaliwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Usajili na historia ya Yanga SC: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa orodha ya watoa burudani

 Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa
Yanga SC paredi

Kwenye paredi kubwa la ubingwa lililofanywa na Yanga SC kuna orodha ndefu ya wasanii ambao walinogesha shughuli. Click Master, Ndaro, Dj Allybi, Marioo. K Pizo kutoka Morogoro, Kidensa MC, Poor Billionare, Dogo Paten, D.Voice.

Beki wa Yanga SC, Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni miongoni mwa waliowatambulisha wachezaji wa Yanga SC jukwaani. Zimbwe alipachikwa jina la DJ Zee. Ikumbukwe kwamba mchezaji huyu alisajiliwa Yanga SC akitokea kwa watani zao wa jadi Simba SC.

SportPesa mdhamini mkuu mabingwa mara 5

Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa
SportPesa mdhamini mkuu wa mabingwa mara 5.

Mpango wa Yanga SC na uwanja: Uwanja mpya wa Yanga SC huu hapa | GSM 50/50 Wananchi, Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)

SportPesa kampuni yenye odds kubwa katika ubashiri wapo bega kwa bega na Yanga SC ni mdhamini mkuu wa mabingwa mara 5. Yanga SC wamekuwa na mafanikio makubwa wakishirikiana na SportPesa hatua kwa hatua. Timu hiyo imeandika rekodi kutwaa ubingwa miaka mitano mfululizo.

Mbali na kutwaa ubingwa wa ligi imefika hatua ya nusu fainali katika taji la CRDB Federation Cup. Timu ya Yanga SC ilitwaa taji la ligi msimu wa 2025/26 ikiwa na pointi 75. Mchezo wa mwisho ilipata ushindi dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

Ni tofauti ya pointi 2 waliwaacha watani zao wa jadi Simba SC. Mtani alikuwa na pointi 73 na Yanga SC pointi 75. Ulikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa huku mabingwa wakiwa ni watoto wa Jangwani.

Prince Dube awaaga Yanga SC

Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube leo Julai 4, 2026 amewaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo na uongozi.Katika mchezo wa funga kazi Juni 30, 2026 alifunga bao la ufunguzi dhidi ya JKT Tanzania. Msimu wa 2026/27 hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC atakuwa kwenye changamoto mpya.

Mchezaji huyo amesema kwa muda ambao amekuwa Tanzania furaha kubwa ilikuwa kwenye kutimiza majukumu yake. Aliongeza kuwa yupo Zimbabwe bado ataendelea kuwafuatilia Yanga SC.

“Ninawashukuru Watanzania kutokana na sapoti yao ambayo wamekuwa wakinipa. Kwa sasa nimerejea Zimbabwe lakini bado nitaendelea kuwafuatilia Yanga SC. Asante sana kwa kuwa kwenye kila mechi walikuwa wanajitokeza kutushangilia jambo ambalo ni furaha kwangu,”.

Yanga SC yautaka ubingwa tena mwakani

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amebainisha kuwa mwakani tena wanahitaji kutetea taji hilo. Amewaomba mashabiki kuendelea kuwa na timu hatua kwa hatua.

“Tunawashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wamekuwa nasi kila nyakati. Mwakani tena tunahitaji kuwa hapa na kulitwaa taji hili. Mipango inafanyika na viongozi wanatambua kuna kazi kubwa inatakiwa kufanywa. Wachezaji na benchi la ufundi kazi kubwa watafanya uwanjani kwa mara nyingine tena,”.

Sportpesa-Aviator-Rain-Free-Bets

Hitimisho

Yanga SC yafanya paredi kubwa la ubingwa huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi. Timu hii inayodhaminiwa na SportPesa imekuwa na mwendelezo mzuri katika ligi ya ndani ikiwa ni timu iliyotwaa mara nyingi taji la ligi. Kwenye kabati imefikisha jumla ya mataji 32.

Share this: