- Uwanja mpya wa Yanga SC ndiyo habari ya mjini kwenye vijiwe vya michezo leo Mei 15, 2026.
- Hii ni baada ya Uongozi wa klabu ya Yanga SC kufanya tukio kubwa na la kihistoria, la utiaji sahihi wa makubaliano ya ujenzi wa uwanja huo.
- Yanga SC imeingia makubaliano ya kiuwekezaji na Kampuni ya GSM kama mbia wa ujenzi huo, huku makubaliano yakiwa ni wa umiliki wa asilimia 50/50.
- Rais Dkt. Samia atajwa kusaidia miundombinu.
Ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC ndiyo Habari ya mjini kwenye vijiwe mbalimbali vya michezo leo Mei 15, 2026. Hii ni baada ya Uongozi wa klabu ya Yanga SC kufanya tukio kubwa na la kihistoria, la utiaji sahihi wa makubaliano ya ujenzi wa uwanja huo. Yanga SC imeingia makubaliano ya kiuwekezaji na Kampuni ya GSM kama mbia wa ujenzi huo, huku makubaliano yakiwa ni wa umiliki wa asilimia 50/50. Makala hii inachambua baadhi ya matukio muhimu yaliyotokea.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Kuhusu tukio la utiaji sahihi wa makubaliano ya ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC
Uongozi wa Wananchi leo Mei 15, 2026 wamefikia makubaliano na kampuni ya GSM, kuwa mbia wa ujenzi Uwanja mpya wa Yanga SC. Mgeni rasmi wa tukio hilo alikuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, akiongozana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne. Tukio hilo lilifanyika makao Makuu ya Yanga SC, Jangwani Dar es Salaam.
Rais wa Yanga SC, Hersi Said afunguka

Akizungumza katika tukio hilo, Rais wa Yanga SC, Hersi Said amesema: “Kwa kipindi cha takribani miaka 90, klabu hii imeendelea kubeba ndoto na dhamira ya dhati ya kuwa na uwanja wake binafsi. Sisi, kama Wananchi tunajivunia mno maono, juhudi na uzalendo wa viongozi waliotutangulia. Viongozi hao walijitolea kwa hali na mali, kuhakikisha wanatuachia msingi imara unaobeba historia, heshima na utambulisho wa klabu yetu.
“Kupitia juhudi zao, klabu ilifanikiwa kumiliki eneo la ardhi lenye ukubwa wa mita za mraba 35,000. Hazina hii imehifadhiwa kwa zaidi ya miaka 50. Leo hii, kwa fahari kubwa Wananchi tunaelekea kutimiza ndoto hiyo ya kihistoria kwa kuanza safari ya kujenga uwanja wetu wenyewe.
“Dhamira yangu kuu nilipoingia katika uongozi ilikuwa ni kuhakikisha klabu inajenga uwanja wake. Hata hivyo, nilibaini kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo, ilikuwa muhimu kwanza klabu ipate mafanikio makubwa ndani ya uwanja wa mchezo ili iweze kuvutia wawekezaji. Tulipoanza kufanya vizuri watu wengi walivutiwa kuwekeza ndani ya klabu yetu. Hali hiyo ikaamsha ari, hamasa na matumaini mapya ya kutimiza ndoto ya kuwa na uwanja wetu wenyewe.
SOMA HII PIA: Uwanja wa Yanga SC watikisa! GSM aonyesha jeuri ya pesa, Ali Kamwe afunguka mazito
GSM aibuka kidedea zabuni ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC

Hersi ameendelea kusema: “Tulipotangaza zabuni ya ujenzi wa uwanja, wawekezaji wengi walijitokeza kuonesha nia ya kushiriki katika mradi huo. Baada ya kupitia mchakato husika, Kamati Kuu hatimaye iliidhinisha GSM Group kuwa mbia mkuu wa ujenzi wa uwanja huo. Nathibitisha rasmi leo kuwa Young Africans SC, imeingia makubaliano ya ubia wa umiliki wa uwanja wetu mpya kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 na GSM Group.
“Tunamshukuru kwa dhati Ghalib Said Mohamed kwa moyo wake wa kizalendo, na uamuzi wake wa kuweka usawa katika umiliki wa mradi huu mkubwa. Licha ya kuwa yeye ndiye anayechangia sehemu kubwa zaidi ya uwekezaji wa kifedha. Kwa upande wa klabu, Young Africans SC itatoa ardhi kwa ajili ya mradi huo, huku mchango wa GSM Group ukiwa ni uwekezaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa.
SOMA HII ZAIDI: Azam yawabadilishia Uwanja Yanga Sc | Na ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania imebadilika
Uwanja mpya Yanga SC unakamilika lini?

Hersi amesema: “Matarajio yetu ni kwamba ujenzi wa uwanja huu utakuwa umekamilika na kuzinduliwa rasmi, ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 20 ijayo. Tuna imani na matumaini makubwa kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati uliopangwa, na kuwa sehemu muhimu ya historia ya klabu yetu. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mara nyingine kwa Ghalib Said Mohamed pamoja na familia yake, kwa maamuzi yao makubwa na ya kizalendo waliyochukua kusaidia kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Yanga SC.
Rais Samia atajwa miundombinu

Katika hotuba yake kuhusu tukio hilo, RC Albert Chalamila amesema: “Watu kama GSM ni watu wa kuwalinda sana. Ukiona mtu anachukua timu, kelele za mishahara zinapotea, timu inasajili vizuri. Baadae wanaachana na hekaheka za vilio ghafla wanahamia kwenye ujenzi wa uwanja, basi ujue klabu hiyo imepata mtu sahihi. Wananchi mnapaswa kumlinda sana Ghalib Said Mohamed.
“Ujenzi wa uwanja wa wa Yanga SC unahitaji sana miundo mbinu ya eneo la Jangwani kuwa imara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu alitenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Jangwani. Tunamshukuru sana Mh Rais kwa kuondoa adha ya mafuriko eneo hilo, ili kutoa fursa ya ufanisi wa ujenzi wa uwanja wa Yanga SC.
“Kabla hujaikosoa Yanga SC jiulize wewe una mchango gani kwa klabu. Nafikiri mmeona mchango wa GSM kwa Klabu yetu, hatimaye anatujengea uwanja, klabu hii haiendeshwi kwa mdomo na makelele pekee. Hatuwezi kutegemea wafadhili pekee yake. Huwezi kuwa mtu ambaye unakosoa tu timu ikifungwa, fukuza makocha lakini huchangii chochote. Ni muda sasa kuchangia klabu hii ili kusaidia klabu kupiga hatua.”
SOMA HII PIA: Yanga SC yatambulisha mashine mpya nne 2025/26 | Benchi la ufundi balaa zito
Hitimisho
Kuanza kwa ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC, kunaonyesha dhamira ya wazi ya Uongozi wa timu hiyo kuleta mapinduzi ya kisoka. Yanga SC inafuata hatua ya klabu nyingine kadhaa, ambazo zinamiliki viwanja vyao wakiwemo Singida Black Stars, Azam FC, KMC n.k. Ni wakati kqwa timu nyingine kuiga msimamo wa uwekezaji huu, ili kukuza soka letu.

