- FT: JKT Tanzania 0-3 Yanga SC, Simba SC 1-0 KMC FC, Fountain Gate 4-3 Singida Black Stars
- Yanga SC bingwa NBC Premier League 2025/26 ikiwa ni mara ya 5 mfululizo mbele ya mtani Simba SC
- SportPesa Blog tumekuletea matokeo ya mechi zote, timu ambazo zimeshuka daraja na zitakazocheza mtoano
Yanga SC bingwa NBC Premier League 2025/26 ikifikisha jumla ya pointi 75 ikicheza mechi 30. Matokeo ya mchezo wa Juni 30,2026 Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo ubao ukisoma JKT Tanzania 0-3 Yanga SC yamekamilisha kazi. Mabao ya ushindi yamefungwa na Prince Dube dakika ya 8, Maxi Nzengeli dakika ya 50 na Deou dakika ya 66.
Soma rekodi za Job: Dickson Job beki wa kazikazi Yanga SC | Rekodi zake, tuzo kabatini, mataji
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Yanga SC bingwa NBC Premier League 2025/26 rekodi imeandikwa

Mwisho wa msimu Yanga SC bingwa NBC Premier League 2025/26 akimshinda mshindani wake wa karibu Simba SC. Huu unakuwa ni ubingwa wa 5 mfululizo kwa watoto wa Jangwani. Baada ya mechi 30 imefikisha jumla ya pointi 75 ikiwa ni nyingi kuliko timu zote kwenye ligi.
Simba SC 1-0 KMC FC ni matokeo rasmi mchezo wa funga msimu uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Ni pointi 73 wanafikisha wakiwa nafasi ya pili. Bao la ushindi kwenye mchezo limefungwa na Inno Loemba kwa mkwaju wa penati dakika ya 55.
Timu ambazo zimeshuka daraja
Mtibwa Sugar imemaliza msimu ikiwa nafasi ya 15 na pointi 27. KMC FC imemaliza msimu ikiwa nafasi ya 16 ikiwa na pointi 9. Hizi zote mbili zimeshuka daraja zitashiriki Championship msimu wa 2026/27.
Timu ambazo zitacheza mchezo wa mtoano
Timu mbili Tanzania Prisons iliyomaliza msimu ikiwa nafasi ya 13 na pointi 32 itacheza mchezo wa mtoano. Ni Tanzania Prisons vs Mbeya City iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 na pointi 27. Zote hizi maskani yake ni Mbeya zinatumia Uwanja wa Sokoine. Mshindi wa mchezo atasalia kwenye ligi na timu itakayopoteza itakuwa na kazi kucheza na timu inayoshiriki Championship kutetea nafasi ya kubaki ama kushuka.
Matokeo ya mechi za Juni 30,2026

Soma usajili wa Yanga SC: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
| Mechi | Matokeo |
|---|---|
| JKT Tanzania vs Yanga SC | 0-3 |
| Simba SC vs KMC FC | 1-0 |
| Azam FC vs Dodoma Jiji | 2-0 |
| Mashujaa FC vs Tz Prisons | 0-1 |
| Mbeya City vs TRA United | 0-0 |
| Coastal Union vs Pamba Jiji | 2-1 |
| Fountain Gate vs Singida Black Stars | 4-3 |
| Namungo FC vs Mtibwa Sugar | 2-1 |

