Job DJob D

Beki wa Yanga SC, Dickson Job ni beki wa kazikazi kutokana na kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja. Job kwa sasa jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji wanaocheza CHAN 2024 akipeperusha bendera ya Tanzania. Akiwa na jezi ya Tanzania, Job anavaa kitambaa cha unahodha kuwaongoza wachezaji wengine kuvuja jasho la ushindi.

Vuna mamilioni rubani ukipaisha kindege cha SportPesa

SEO Banner LV

Muda wa kuvuna mamilioni kwa kila rubani. Unastahili kupata kilicho bora na rahisi kwelikweli.Unachotakiwakufanya ni kucheza Aviator upate mgao wako sasa hivi.

Kutoka Morogoro mpaka Dar kwa changamoto mpya

Job taji
Job akiwa na taji la NBC msimu wa 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii: Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa Simba SC

Job alitambulishwa rasmi Yanga SC 2021 akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Amekuwa kwenye mwendo mzuri katika mechi ushindani kitaifa na kimataifa. Msimu wa 2024/25 alikuwa ni chaguo la kwanza chini ya Miloud Hamdi.

 2022/23 alitwaa tuzo ya beki bora wa ligi. Msimu huo pia jina lake lilikuwa katika orodha ya wachezaji 11 wa ligi. Ni miongoni mwa wazawa wanaojituma muda wote bila kuchoka.

Job na Tanzania

Katika timu ya taifa ya Tanzania, CHAN 2024 ipo kundi B. Tanzania imemaliza mechi za hatua ya makundi ikiwa inaongoza kundi na pointi zake kibindoni ni 10. Ilishinda tatu, ilitoshana nguvu mchezo mmoja. Katika mechi hizo nne ambazo ni dakika 360, ukuta umeruhusu kufungwa bao moja na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 5.

Ukuta mgumu Yanga SC 2024/25

Job
Job kwenye maandalizi ya mechi msimu wa 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii: Dickson Job kusaini mkataba mpya

Job alikuwa anaunda safu ya ulinzi ya Yanga SC ambayo inau kuta mgumu. Msimu wa 2024/25 wa NBC ni mabao 10 timu hiyo ilifungwa. Hiyo ni baada ya mechi 30.

Mlinda mlango namba moja wa Yanga SC ni Djigui Diarra aliyekuwa anaimarisha ulinzi lango. Diarra alikuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mabeki wa Yanga SC wakiongozwa na Job. Alikusanya jumla ya hati safi 17. Ni kipa namba mbili kukusanya hati safi nyingi ndani ya ligi.

Kinara kwenye eneo hilo ni Moussa Camara wa Simba SC. Camara ana hati safi 19. Katika hati hizo Camara alikwama kukusanya mbele ya Yanga SC. Kwenye Kariakoo Dabi mechi zote mbili ambazo ni dakika 180 alitunguliwa.

Yanga SC bingwa 2024/25 Job ndani

Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi ya NBC ikiwa na pointi 82 kwenye mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Job alicheza jumla ya mechi 26. Ni dakika 2,252 Job alitumia uwanjani.

Alikosekana kwenye mechi nne ndani ya msimu ambazo ni dakika 360. Miongoni mwa mchezo ambao aliukosa ilikuwa dhidi ya Tabora United. Mchezo huo ulichezwa Aprili 2 2025, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 0-3 Yanga SC. Pointi tatu zilikuwa ni mali ya Yanga SC. Kwenye mzunguko wa kwanza, Yanga SC 1-3 Tabora United, hivyo wababe hawa waligawana pointi tatutatu.

Yeye na kucheka na nyavu

Job
Job Dickson beki wa Yanga SC 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii: SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7 kupitia Ofa kubwa ya kihistoria

  Msimu wa 2023/24 Job alikuwa mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi ndani ya Yanga SC. Bao hilo alifunga kwenye mchezo dhidi ya KMC. Hiyo ilikuwa Uwanja wa Azam Complex Yanga SC.

Mwisho wa msimu Yanga SC ilimaliza ikiwa imetupia mabao 71. Katika mabao hayo 71 Job alifunga bao moja pekee. Yote hii inatokana na nafasi ambayo anacheza yeye ni beki.

 msimu wa 2024/25 umegota mwisho bila yeye kufunga. Mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC alikuwa ni Maxi Nzengeli. Ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Mkataba wake ndani ya Yanga SC

SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii:Wapya watatu kutambulishwa Yanga SC

Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC kwa asilimia 100 imekamilisha makubaliano ya pande zote mbili. Katika mazungumzo hayo Yanga SC imempa mkataba wa miaka miwili ambao una maboresho makubwa. Kwa sasa ni suala la muda beki huyo taarifa zake kuwa wazi kuhusu kuongeza mkataba mpya.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe aliweka wazi kuwa kwa mchezaji ambaye wanahitaji huduma yake itakuwa ngumu kuodoka kwenye kikosi hicho. Kamwe aliongeza kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi hicho thamani yake ni kubwa.

“Kwa mchezaji ambaye tunahitaji huduma yake basi tutaweka hela ili abaki. Unakumbuka kuhusu Aziz Ki? Kuna timu zilikuwa zinamuhitaji lakini tukamuongezea mkataba. Mpaka anaondoka tumeona sasa akapate changamoto mpya.

“Ambacho tunakifanya ni kuboresha kikosi chetu. Ni kama nyumba vile unaona kuna sehemu hakupo imara unaboresha. Sio kuanza kujenga timu hiyo hatua tayari tumeshatoka.”

Hitimisho

Yanga SC imewaongezea mikataba nyota wake kwa ajili ya msimu wa 2025/26. Miongoni mwa hao ni Duke Abuya, Maxi Nzengeli. Kiungo Pacome ambaye alikuwa anatajwa kuwa ataondoka naye ni uhakika kucheza Yanga SC msimu wa 2025/26.

image
Share this: