- Spain vs Austria Kombe la Dunia 2026, ni ratiba inayosubiriwa kwa hamu kujua ni nani atafanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
- Mechi hii itapigwa 2 July 2026 katika Uwanja wa Los Angles, USA kuanzia majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
- Spain inayobebwa na mastaa kama, Lamine Yamal, Pedri na Mikel Oyarzabal watavaana uso kwa uso na mastaa David Alaba na Marcel Sabitzer wa Austria.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Spain waliomaliza kileleni mwa Kundi H la Kombe la Dunia 2026, watavaana na washindi wa pili wa Kundi J Australia siku ya Alhamisi 2 July 2026. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Los Angles, USA ambapo mshindi wa mchezo atakuwa amefuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora ya mashindano. Hii inatarajiwa kuwa vita kali baina ya mastaa wa Spain wakiongozwa na Yamal, dhidi ya wale wa Austria wakiongozwa na Alaba. Makala hii inachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups nk
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Spain vs Austria
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Mechi ya hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo Hispania na Austria zinapambana kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya 16 Bora. |
| Tarehe na Muda | Mchezo umepangwa kuchezwa Alhamisi, 2 Julai 2026, kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). |
| Uwanja | Pambano litafanyika katika Los Angeles Stadium, Marekani, ambao utakuwa mwenyeji wa mechi hii muhimu ya hatua ya mtoano. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa Spain vs Austria
Hispania inapewa nafasi kubwa ya kuiondoa Austria katika mchezo wa hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia 2026, utakaochezwa Alhamisi usiku nchini Marekani. Hispania wanaingia kwenye mchezo huu, wakiwa hawajapoteza mechi yoyote katika mashindano haya. Austria ilimaliza nafasi ya pili katika Kundi J nyuma ya mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Argentina, na hivyo kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 70. Mshindi wa pambano hili atakutana na mshindi kati ya Ureno na Croatia katika hatua ya 16 Bora.
Habari za Timu na majeruhi
Kwa upande wa Hispania, Nico Williams na Yeremy Pino ni majeruhi wapya baada ya kuumia katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi. Inaonekana Yeremy Pino ana uwezekano mdogo wa kucheza tena, katika mashindano haya. Kocha Luis de la Fuente anatarajiwa kuanza na kikosi kitachopatikana, huku Mikel Oyarzabal akiendelea kuwa mshambuliaji mkuu baada ya kuhusika katika mabao matatu kati ya matano yaliyofungwa na Hispania kwenye mashindano haya. Lamine Yamal wa Barcelona pia ameonyesha kiwango bora, na anatarajiwa kuanza kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuanzia benchi katika mchezo wa kwanza.
Vikosi Vinavyotarajiwa
Hispania
| Nafasi | Wachezaji Wanaotarajiwa |
|---|---|
| Kipa | Simon |
| Safu ya Ulinzi | Llorente, Cubarsi, Laporte, Cucurella |
| Safu ya Kiungo | Merino, Rodri, Pedri |
| Safu ya Ushambuliaji | Yamal, Oyarzabal, Baena |
Austria

| Nafasi | Wachezaji Wanaotarajiwa |
|---|---|
| Kipa | A. Schlager |
| Safu ya Ulinzi | Posch, Lienhart, Alaba, Mwene |
| Safu ya Kiungo | Siewald, X. Schlager, Laimer, Schmid, Sabitzer |
| Mshambuliaji | Arnautovic |
Spain vs Austria h2h
Timu hizi zimeandikisa mechi 16 katika mikutano yao, ambapo Spain imeandikisha ushindi wa mechi 9, Austria wao wameshinda mechi 4 pekee, huku mechi 3 ziiisha kwa sare. Jedwali lifuatalo, linatoa taswira ya baadhi ya mechi zao za h2h.
Mechi Tano Zilizopita Kati ya Hispania na Austria
| Tarehe | Mchezo | Matokeo |
|---|---|---|
| 18 Novemba 2009 | Austria vs Hispania | Austria 1-5 Hispania |
| 1 Septemba 2001 | Hispania vs Austria | Hispania 4-0 Austria |
| 11 Oktoba 2000 | Austria vs Hispania | Austria 1-1 Hispania |
| 4 Septemba 1999 | Austria vs Hispania | Austria 1-3 Hispania |
| 27 Machi 1999 | Hispania vs Austria | Hispania 9-0 Austria |
Utabiri (ushindi kwa Spain)
Ingawa mchezo unatarajiwa kuwa wa ushindani, lakini Spain wanapewa nafasi kubwa ya kushinda, mechi za hatua ya mtoano. Baada ya timu kubwa kama Ujerumani na Uholanzi kuondolewa mapema, Hispania haiwezi kuichukulia Austria kwa wepesi. Hata hivyo, kutokana na uchambuzi wa uimara wao tunabashiri ushindi kwa Spain, ikimbukwe haya sio matokeo halisi hivyo Bashiri kistaarabu.
Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unawapa nafasi kubwa Spain kuibuka na ushindi, hii ni kwa kuzingatia ubora wa vikosi vya timu zote 2. Mechi hii inatarajiwa kuwa na mabao kwa kuzingatia, wasimu wa mastaa wao. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Spain vs Austria na mechi nyingine za hatua ya 32 bora kwenye SportPesa. Tafadhali bashiri kistaarabu.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)
Spain vs Austria itaanza saa ngapi?
Mechi inatarajiwa kuanza saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT), Alhamisi July 2, 2026.
Spain imeshinda mara ngapi kombe la Dunia?
Spain imefanikiwa kushinda Kombe la Dunia mara 1 tu, katika historia ya Taifa hilo, ambapo ilikuwa mwaka 2010 pale Afrika Kusini.
Spain vs Austria zimewahi kukutana?
Ndiyo Spain na Austria zimekutana katika michezo 16 ambapo, Spain wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 9 sare 3 na kupoteza mechi 4.
KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA FRANCE, SOMA HII: France vs Sweden Kombe la Dunia 2026 hatua ya 32 bora: Live score, h2h, odds na habari za timu

