- England vs DR Congo FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 32 bora Julai Mosi
- Uwanja wa Atlanta wawakilishi kutoka Afrika, DR Congo watakuwa kazini kusaka tiketi kutinga 16 bora
- SportPesa Blog imekuletea uchambuzi wa mchezo huu muhimu, wachezaji na taarifa kuhusu timu
England vs DR Congo FIFA Kombe la Dunia 2026 watakutana Jumatano Atlanta. Timu ya Thomas Tuchel ilimaliza kileleni mwa Kundi L bila kupoteza, baada ya ushindi dhidi ya Croatia na Panama, lakini sare tasa dhidi ya Ghana iliibua maswali kuhusu uwezo wao wa kushambulia. Ingawa wameonyesha uimara wa kiulinzi, mara nyingi wamekuwa wakihangaika kuvunja ngome za wapinzani wanaojipanga kwa nidhamu changamoto ambayo huenda ikajirudia tena dhidi ya Congo.
Ijue ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mecchi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya England vs DR Congo angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa uwajibikaji.

Taarifa ya mechi
| Mashindano | Mechi | Uwanja | Tarehe | Muda | Hatua | Jukwaa la kubashiri |
|---|---|---|---|---|---|---|
| FIFA Kombe la Dunia 2026 | England vs DR Congo | Atlanta | Julai 1, 2026 | Saa 1:00 usiku (EAT) | 32 bora | SportPesa |
England vs DR Congo taarifa za timu
DR Congo walimaliza kama timu bora zaidi kati ya zilizoshika nafasi ya tatu, wakipata alama muhimu dhidi ya Ureno na ushindi wa 3-1 dhidi ya Uzbekistan. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa. England wakitafuta uthibitisho wa ubora wao, huku Congo wakitaka rekodi kufika hatua ya 32 bora.
Hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa DR Congo kucheza hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, na wameibuka haraka kama moja ya matumaini makubwa ya Afrika baada ya kuonyesha uimara katika hatua ya makundi. Ushindi wao dhidi ya Uzbekistan na sare dhidi ya Ureno uliwapa heshima kubwa na kuonyesha kwamba wanaweza kushindana na wakubwa.
Kwa upande wa England, nahodha Harry Kane aliweka historia kwa kufunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Panama, na kufikia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England katika Kombe la Dunia kwa mabao 11. Kane pia amefunga katika mechi mbili kati ya tatu zilizopita dhidi ya wapinzani kutoka Afrika, jambo linaloongeza matumaini kwa mashabiki wa Three Lions.
England na DR Congo habari za vikosi

Takwimu mechi hatua ya 32 bora: Prediction Belgium vs Senegal FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, lineups, odds
Kwa upande wa England, Thomas Tuchel anaweza kufanya marekebisho katika safu ya ushambuliaji kutokana na wasiwasi wa ukosefu wa mabao. Harry Kane ataongoza mstari wa mbele, huku nyota wa Arsenal Bukayo Saka akitarajiwa kuendelea katika kikosi cha kwanza. Marcus Rashford anaweza kupewa nafasi, jambo litakalomfanya Antony Gordon kuanzia benchi. Katika safu ya ulinzi, Jarrel Quansah aliumia dhidi ya Panama na Reece James tayari ametolewa nje, hivyo Djed Spence ataendelea kuanza huku walinzi wengine wakibaki vilevile. Kiungo wa Real Madrid Jude Bellingham, aliyefunga bao lake la kwanza katika mashindano haya dhidi ya Panama, ataendelea kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Kwa upande wa Congo, wanabaki na kikosi ambacho hakitakuwa na mabadiliko makubwa. Wanatarajiwa kuanza na wachezaji wale wale waliocheza dhidi ya Uzbekistan. Nyota wao Yoanne Wissa, aliyefunga mabao mawili katika mchezo huo, ataongoza safu ya ushambuliaji ya Leopards.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa, huku England wakitafuta uthibitisho wa ubora wao na Congo wakitaka kuendeleza historia yao kwa kushtua dunia.
Katika historia ya England na DR Congo, hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa mataifa haya mawili kukutana katika mchezo wa mashindano rasmi.
Hali ya sasa ya vikosi
- England hawajapoteza katika mechi tano zilizopita, wakishinda nne na kutoka sare tasa dhidi ya Ghana.
- Congo wamepata ushindi mmoja pekee katika kipindi hicho, lakini wanafurahia historia ya kufuzu kwa hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza.
Rekodi ya matokeo ya karibuni
- England – WDWWW
- Congo – WLDLD
Prediction England vs DR Congo
England inapewa nafasi kubwa kupata ushindi kwenye mchezo huu wa hatua ya 32 bora. Ni asilimia 77 za ushindi kwa England huku DR Congo ikipewa asilimia 7. Sare kwenye mchezo huu ama uwezekano kwenda kwenye muda wa nyongeza ni asilimia 16.
Matokeo utabiri: England 3-1 DR Congo. Haya sio matokeo kamili ni maoni ya mhariri.
Namna ya kubashiri kupitia SportPesa

Fungua ukurasa wa tukio la England vs DR Congo kwenye SportPesa.
Chagua soko lako — Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB) mara tu mechi itakapoanza.
Weka dau lako na thibitisha ubashiri.

