- France vs Sweden Kombe la Dunia 2026, ni ratiba ya vita nyingine ya kuisaka hatua ya 16 bora ambayo itapigwa Jumatano 1 Julai 2026 katika Uwanja wa New York New Jersey, USA.
- Mechi hii kali inatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa sita kamili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mshindi wa mechi hii anafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.
- France chini ya mastaa wao, Kylian Mbappe na Ousmane Dembele watakutana uso kwa uso na jeshi la Sweden linaloongozwa na mastraika, Victor Gyokeres na Alexander Isak.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Ufaransa wana kibarua kizito katika mchezo wao wa kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora, hii ni pale watakapovaana na Sweden siku ya Jumatano 1 July 2026. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New York New Jersey USA, kuanzia saa 6 usiku. Mchezo huu unatarajiwa kuwa vita kali ya washambuliaji upande mmoja ukiwa na Kylian Mbappe na Ousmane Dembele, huku upande wa pili ukiwa na Victor Gyokeres na Alexander Isak. Je, ni France au Sweden? Majibu ni baada ya dakika tisini za mwamuzi, ila Makala hii itakusaidia kuchambua matokeo na kubashiri.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya France vs Sweden
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Mchezo wa Hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. |
| Tarehe na Muda | Pambano hili litachezwa Jumatano, 1 Julai 2026, kuanzia saa 6:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). |
| Uwanja | New York New Jersey Stadium nchini Marekani utakuwa mwenyeji wa mchezo huu wa hatua ya mtoano. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa France vs Sweden

Ufaransa itaanza safari yake ya hatua za mtoano za Kombe la Dunia 2026, itakapokutana na Sweden katika mchezo wa hatua ya 32 Bora utakaochezwa kwenye Uwanja wa New York New Jersey Stadium. Baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi I kwa alama zote tisa, Ufaransa wanapewa nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye mashindano haya. Sweden wao walifanikiwa kufuzu kwa taabu, baada ya kuwa miongoni mwa timu nane bora zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi.
Ousmane Dembele aliifungia Ufaransa mabao matatu dhidi ya Norway, jambo lililoonyesha kuwa timu hiyo ina silaha nyingi za ushambuliaji zaidi ya nyota wake Kylian Mbappe. Ufaransa wamefika fainali katika michuano miwili mfululizo iliyopita, yaani 2018 na 2022. Hata hivyo, safari yao kuelekea fainali haitakuwa rahisi. Ikiwa wataendelea kusonga mbele, wanaweza kukutana na Ujerumani katika hatua ya 16 Bora, kisha Netherlands au Morocco robo fainali, na baadaye Hispania au Portugal katika nusu fainali.
Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa
Beki wa kati wa Ufaransa William Saliba alipumzishwa dhidi ya Norway kutokana na maumivu ya mgongo, lakini anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo huu. Dayot Upamecano ataendelea kuunda safu ya ulinzi wa kati, huku Aurelien Tchouameni na Adrien Rabiot wakitarajiwa kuanza katika nafasi za kiungo. Baada ya kutoka patupu vs Norway nahodha wa Kylian Mbappe atakuwa anawinda kufunga bao lake la tano katika mashindano haya.
Ufaransa
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Mike Maignan |
| Safu ya Ulinzi | Jules Kounde, Dayot Upamecano, William Saliba, Theo Hernandez |
| Safu ya Kiungo | Aurelien Tchouameni, Adrien Rabiot |
| Safu ya Ushambuliaji | Michael Olise, Ousmane Dembele, Desire Doue |
| Mshambuliaji wa Kati | Kylian Mbappe |
Sweden

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Jacob Zetterström |
| Safu ya Ulinzi | Gustaf Lagerbielke, Victor Lindelöf, Gabriel Gudmundsson |
| Safu ya Kiungo | Anton Bernhardsson, Lucas Bergvall, Yasin Ayari, Stroud |
| Safu ya Ushambuliaji | Anthony Elanga, Viktor Gyökeres |
| Mshambuliaji wa Kati | Alexander Isak |
Utabiri wetu (Ushindi kwa Ufaransa)
Ufaransa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa inapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele, kutokana na ubora wa kikosi chake na nguvu kubwa iliyonayo katika safu ya ushambuliaji. Ingawa Sweden wana wachezaji wenye uwezo wa kuleta madhara mbele ya lango, safu yao ya ulinzi imeonyesha udhaifu. Hali hiyo inaweza kuifanya ishindwe kuhimili mashambulizi ya Ufaransa kwa dakika 90.
KUJUA RATIBA NA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA SENEGAL, SOMA HII: Prediction Belgium vs Senegal FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, lineups, odds
Rekodi ya France vs Sweden (H2H)

Timu hizi zimekutana mara 23 katika historia yao, ambapo Ufaransa wana rekodi bora zaidi wakishinda mechi 12. Sweden wao wameshinda mechi 6, huku mechi 5 zikiisha kwa matokeo ya sare. Hivyo mchezo huu ni nafasi nyingine kwa timu hizi kuandika rekodi mpya.
Hitimisho
Utabiri wetu wa kiuhariri unawapa nafasi kubwa Ufaransa kuibuka na ushindi, hii ni kwa kuzingatia ubora wa vikosi vya timu zote 2. Mechi hii inatarajiwa kuwa na mabao mengi kwa kuzingatia, wasimu wa mastaa wao. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za France vs Sweden na mechi nyingine za hatua ya 32 bora kwenye SportPesa. Tafadhali bashiri kistaarabu.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

France vs Sweden itaanza saa ngapi?
Mechi inatarajiwa kuanza saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT), Jumatano July 1, 2026.
Ufaransa imeshinda mara ngapi kombe la Dunia?
Ufaransa imefanikiwa kushinda Kombe la Dunia mara 2, ambapo ilikuwa mwaka 1998 na mwaka 2018. Ufaransa pia wamefika fainali mara mbili mfululizo zilizopita.
France na Sweden zimewahi kukutana?
Ndiyo France na Swedenzimekutana katika michezo 23 ambapo, France wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 12 sare 5 na kupoteza mechi 6.
KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA MEXICO, SOMA HII: Mexico vs Ecuador FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 32 bora: Prediction, odds, team news, lineups

