- Ni Senegal vs Iraq FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo wa mwisho Kundi I
- Mshindi wa mchezo anafufua matumaini ya kufuzu hatua ya 32 kupitia timu zitakazomaliza nafasi ya 3
- SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi wa kina, rekodi wachezaji wakuchungwa kuelekea mchezo huu
Senegal vs Iraq FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo wa mwisho Kundi I. Senegal watakuwa na nafasi yao ya mwisho ya kujinusuru watakapokutana na Iraq Ijumaa jioni mjini Toronto. Simba wa Teranga wamepoteza michezo yao miwili ya mwanzo dhidi ya France na Norway. Katika mchezo wao wa hivi karibuni, walifungwa mabao 3-2, huku Erling Haaland akifunga mabao mawili na kuwa chachu ya ushindi wa Norway.
Isome ratiba ya Kombe la Dunia: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mecchi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Senegal vs Iraq angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa uwajibikaji.

Taarifa kuhusu mechi
| Mashindano | FIFA Kombe la Dunia 2026 |
| Kundi | Kundi I |
| Timu | Senegal vs Iraq |
| Tarehe | Ijumaa, Juni 26, 2026 |
| Muda wa kuanza | Saa 4:00 usiku (EAT) |
| Uwanja | BMO Field |
| Mechi ya wakati mmoja | Norway vs France |
| Hali ya kundi | Norway 6 pts, France 6 pts, Senegal 0 pts, Iraq 0 pts |
| Jukwaa la kubashiri | SportPesa |
Senegal vs Iraq taarifa kuhusu timu
Iraq wamefungwa jumla ya mabao saba na kufunga bao moja pekee katika michezo yao miwili ya kwanza ya kundi. Timu zote mbili zipo mkiani mwa Kundi I bila kuwa na pointi yoyote. Senegal na Iraq bado wana matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano kupitia nafasi za timu bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu, hivyo ushindi ni muhimu kwa kila upande ili kuendelea kuwa na matumaini ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.
Senegal wanalenga kurudia mafanikio yao ya Kombe la Dunia lililopita, ambapo walifanikiwa kuvuka hatua ya makundi na kufika hatua ya 16 bora. Rekodi yao bora zaidi katika historia ya mashindano haya bado ni ya mwaka 2002, ambapo walitolewa katika hatua ya robo fainali.
Kwa kuwa nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano ipo mezani, Senegal wanatarajiwa kuanza na kikosi chao bora kabisa.Nahodha Kalidou Koulibaly ameendelea kuwa imara katika ulinzi na anatarajiwa kuongoza safu ya nyuma akiwa pamoja na Moussa Diakhate.Nyota Sadio Mané bado hajawa katika kiwango bora katika mashindano haya, lakini anatarajiwa kuanza.
Wengine watakaoanza ni Iliman Ndiaye na Ismaïla Sarr, ambaye alifunga mabao mawili dhidi ya Norway.Mshambuliaji Nicolas Jackson amekuwa na changamoto ya kutumia nafasi, lakini ataendelea kuaminiwa kuanza mbele.
Kwa upande wa Iraq, hawatarajiwi kufanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi kilichopoteza dhidi ya France. Wataingia na kikosi kilekile, huku Aymen Hussein akiongoza mashambulizi.
Hali ya timu na historia ya makabiliano

Takwimu za Japan vs Sweden hizi hapa: Japan vs Sweden FIFA Kombe la Dunia 2026: Prediction, h2h, lineups, odds, Kundi F
Senegal wamepoteza michezo 3 kati ya 5 ya mwisho, jambo linaloongeza umuhimu wa kushinda mchezo huu. Wameshinda mchezo mmoja pekee katika kipindi hicho.
Iraq nao wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa kwenye mfululizo wa kupoteza mechi tatu mfululizo, wakifungwa mabao tisa na kufunga bao moja pekee.
H2H Senegal vs Iraq
Hii itakuwa mara ya kwanza kabisa timu hizi mbili kukutana katika historia yao ya mashindano. (Kumbuka: kuna taarifa zilizochanganyika zinataja Iran/Iraq, lakini mechi inayohusika hapa ni Senegal dhidi ya Iraq).
Utabiri wa Senegal vs Iraq
Senegal wana uzoefu mkubwa zaidi wa Kombe la Dunia, ubora wa juu wa wachezaji mmoja mmoja, pamoja na nguvu kubwa ya kimwili na kasi uwanjani.Iraq wanatarajiwa kupambana kwa juhudi kubwa, lakini bado wanaweza kukutana na changamoto dhidi ya ubora wa Senegal katika maeneo yote ya uwanja.
Kwa ujumla, Senegal wanaonekana kuwa na silaha za kutosha za kushinda mchezo huu na kupata ushindi wao wa kwanza katika mashindano haya, huku wakidumisha matumaini yao ya kufuzu hatua ya mtoano. Senegal 2-1 Iraq, ni maoni ya mhariri sio matokeo kamili.

Jinsi ya Kubashiri na SportPesa
Fungua ukurasa wa mechi ya Senegal vs Iraq kwenye SportPesa (link above).
Chagua aina ya masoko unayotaka kuweka dau lako – Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB)
Weka kiasi cha dau lako na uthibitishe.
Kiwango cha sasa (Current form)
Senegal – LLDLW
= Kipigo, Kipigo, Sare, Kipigo, Ushindi
Iraq – LLLDW
= Kipigo, Kipigo, Kipigo, Sare, Ushindi
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Senegal vs Iraq utachezwa muda gani?
Saa 04:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Juni 26, 2026, Uwanja wa BMO Field, Totonto, Ontario, Canada.
Senegal ama Iraq zinaweza kufuzu hatua inayofuata?
Timu zote mbili zinaweza kufuzu hatua ya 32 bora kupitia nafasi ya timu zitakazomaliza nafasi ya 3 kwa sababu Ufaransa na Norway tayari zimeshafuzu.
Senegal waliwahi kuwa na kiwango bora Kombe la Dunia?
Hatua kubwa ambayo Senegal wamefika ni robo fainali ilikuwa 2002 na waliushangaza ulimwengu kwa kupata ushindi dhidi ya Ufanrasa katika hatua ya makundi.
Senegal na Iraq zimewahi kukutana?
Hapana. Huu unakuwa mchezo wa kwanza.
Senegal na Iraq wapo kundi gani?
Timu zote zipo Kundi I wakiwa na Ufaransa na Norway ambazo baada ya mechi mbili zimekuanya pointi 6 huku Senegal na Iraq zote zina 0.

