Utabiri wa Netherlands vs Sweden Kombe la Dunia – Kundi G
- Netherlands vs Sweden Kombe la Dunia 2026 ni vita ya rekodi na kisasi, pambano hili litapigwa 20 June 2026, kwenye Uwanja wa NRG Stadium, Houston.
- Mechi hii ya Kundi F itapigwa saa 2 usiku kwa saa za afrika. Ikumbukwe matokeo ya mechi za kwanza yalikuwa Netherlands 2-2 vs Japan, na Sweden 5-1 Tunisia.
- Mechi hii inabeba vita kuwa ya safu za ushambuliaji ambapo Sweden watakuwa na Victor Gyokeres na Alexander Isak, huku Netherlands wakiwa na Cody Gakpo na Memphis Depay.
Netherlands watavaana na Sweden tarehe 20 June 2026, mechi hii itapigwa Uwanja wa NRG Stadium, Houston saa 2 usiku kwa saa za afrika mashariki. Mchezo huu ni wa Kundi F la Kombe la Dunia 2026. Katika mechi ya kwanza Netherlands walipata sare ya mabao 2-2 vs Japan, huku Sweden wakiikandamiza Tunisia na ushindi mkubwa wa magoli 5-1. Mechi hii inabeba hatima ya mataifa haya kufuzu hatua ya mtoano ya 32 bora.
Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Kombe la Dunia 2026 – Kundi F, mechi za mzunguko wa pili wa hatua ya makundi |
| Tarehe na Muda | Jumamosi, 20 Juni 2026, saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) |
| Uwanja | NRG Stadium, Houston, Texas, Marekani |
| Msimamo wa Kundi F | Baada ya mechi za ufunguzi: Uswidi pointi 3, Japan pointi 1, Uholanzi pointi 1, Tunisia pointi 0 |
| Umuhimu kwa Uholanzi | Uholanzi wanahitaji ushindi ili kuendelea kuwa na nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano na kudhibiti hatma yao kwenye kundi. |
| Umuhimu kwa Uswidi | Ushindi utawapa Uswidi pointi 6, hatua itakayowaweka karibu sana na tiketi ya kwenda Raundi ya 32. |
| Matokeo ya Sare | Sare itawaacha Uholanzi wakiwa chini ya presha kubwa kabla ya mechi yao ya mwisho, huku Uswidi wakibaki kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele. |
| Athari ya Kushindwa | Kipigo kwa Uholanzi kitaweka matumaini yao ya kufuzu kwenye hatari kubwa, ilhali kushindwa kwa Uswidi kutaufanya mchuano wa kufuzu kuwa wazi zaidi kwa timu zote za kundi. |
Kuangalia ratiba ya mechi zote 104 za Kombe la Dunia 2-26, soma hii: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Wapi kwa kutazama (How to watch) Netherlands vs Sweden
Mashabiki wanaweza kufuatilia Netherlands vs Swedenkupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Muhtasari wa utabiri na uchambuzi wa mechi ya Netherlands vs Sweden
Uholanzi waliingia kwenye Kombe hili la Dunia wakiwa miongoni mwa timu zilizotarajiwa kufika mbali, hata hivyo, sare ya 2-2 dhidi ya Japan haukutarajiwa. Kuongoza mara mbili kwa mabao ya Virgil van Dijk na Crysencio Summerville, kisha kusawazishiwa kumeonyesha udhaifu wa safu yao ya ulinzi. Netherland wameshinda mechi mbili pekee kati ya tano zao za mwisho, huku kipigo chao pekee katika kipindi hicho kikiwa ni cha bao 1-0 dhidi ya Algeria kwenye mechi ya kirafiki.
Memphis Depay, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Uholanzi, aliingia akitokea benchi dhidi ya Japan lakini anatarajiwa kuanza mechi hii badala ya Donyell Malen au Tijani Reijnders. Kiungo chao kinachoongozwa na Frenkie de Jong na Ryan Gravenberch, kinatarajiwa kubaki bila mabadiliko. Cody Gakpo ataendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji.
Sweden wameanza vizuri mashindano haya, hii ni baada ya kuichapa Tunisia mabao 5-1. Yasin Ayari wa Brighton ndiye aliyeng’ara zaidi, akifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia. Viktor Gyökeres na Alexander Isak, ambao wengi wanawaona kama washambuliaji hatari zaidi, kutoka Ligi Kuu ya Uingereza katika Kombe hili la Dunia wote walifunga na wanatarajiwa kuanza tena.
Katika historia ya Kombe la Dunia, Sweden wamewahi kuwa washindi wa pili mwaka 1958, walipokuwa wenyeji. Walifika robo fainali mwaka 2018, na walikosa nafasi ya kushiriki mashindano ya 2022.
Habari za timu na vikosi vinavyotarajiwa kuanza

Hakuna mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kwenye vikosi, hii ni kutokana na taarifa kuwa hakuna majeruhi wapya. Vikosi tarajiwa ni hivi hapa chini, lakini vikosi kamili vitatolewa saa chache kabla ya mchezo. Hili linatarajiwa kufanywa na mabenchi ya ufundi.
| Nafasi | Netherlands | Sweden |
|---|---|---|
| Golikipa | Flekken | Olsen |
| Beki wa kulia | Dumfries | Lustig |
| Beki wa kati | Van Dijk | Lindelöf |
| Beki wa kati | De Vrij | Hien |
| Beki wa kushoto | Aké | Augustinsson |
| Kiungo wa ulinzi | De Jong | Svanberg |
| Kiungo wa ulinzi | Gravenberch | Cajuste |
| Kiungo wa kulia | Reijnders au Depay | Ayari |
| Kiungo mshambuliaji | Gakpo | Claesson |
| Kiungo wa kushoto / mshambuliaji wa pembeni | Summerville | Isak |
| Mshambuliaji | Malen au Depay | Gyökeres |
Takwimu Muhimu
- Uholanzi walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Japan katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi F. Waliongoza mara mbili kupitia mabao ya Virgil van Dijk na Crysencio Summerville.
- Uholanzi wameshinda mechi 2 pekee kati ya 5 zao za mwisho, huku kipigo chao pekee katika kipindi hicho kikiwa ni cha mabao 1-0 dhidi ya Algeria kwenye mchezo wa kirafiki.
- Mwenendo wa Uholanzi (mechi 5 zilizopita): D W L D W.
- Uholanzi walikosa kushiriki Kombe la Dunia la 2018 na walitolewa katika hatua ya robo fainali mwaka 2022. Hawajawahi kutwaa Kombe la Dunia licha ya kufika fainali mara tatu (1974, 1978 na 2010).
- Jurrien Timber alikosekana katika mchezo dhidi ya Japan. Hali yake itathibitishwa kabla ya mechi kuanza.
- Memphis Depay, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Uholanzi, aliingia akitokea benchi dhidi ya Japan na anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza.
- Cody Gakpo anaendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Uholanzi.
- Uswidi waliifunga Tunisia mabao 5-1 katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi F, ikiwa ni moja ya ushindi mkubwa zaidi katika raundi ya ufunguzi ya mashindano haya.
- Mwenendo wa Uswidi (mechi 5 zilizopita): W D L W W.
- Yasin Ayari wa Brighton alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia.
- Viktor Gyökeres na Alexander Isak wote walifunga dhidi ya Tunisia na wanaendelea kuwa miongoni mwa washambuliaji walio katika kiwango bora kwa sasa.
- Matokeo bora zaidi ya Uswidi katika Kombe la Dunia ni kuwa washindi wa pili mwaka 1958 walipokuwa wenyeji wa mashindano hayo.
- Uswidi walifika robo fainali mwaka 2018 lakini walikosa kufuzu kwa Kombe la Dunia
- H2H (last 5): Netherlands 2-0 Sweden (2017); Sweden 1-1 Netherlands (2016); Sweden 3-2 Netherlands (2011); Netherlands 4-1 Sweden (2010); Netherlands 3-1 Sweden (2008). Netherlands kushinda 3, Sweden kushinda 1, sare 1.
- Msimamo wa Kundi (baada ya mechi ya kwanza): Sweden pointi 3, Japan pointi 1, Netherlands pointi 1, Tunisia 0pts.
Historia ya Mikutano (Head-to-head) Netherlands vs Sweden
Netherlands wana rekodi bora zaidi katika mikutano yao ya hivi karibuni dhidi ya Sweden, wakiwa wameshinda mechi tatu kati ya tano za mwisho walizokutana. Mchezo wao wa mwisho ulikuwa mwezi Oktoba 2017, ambapo Netherlands walishinda mabao 2-0. Ushindi pekee wa Sweden katika kipindi hicho ulikuwa wa mabao 3-2 mnamo Novemba 2011. Hizi ni timu mbili za Ulaya zinazofahamiana vizuri na zimekutana mara kwa mara kupitia mashindano mbalimbali.
| Tarehe | Matokeo |
|---|---|
| 10 Oktoba 2017 | Uholanzi 2–0 Uswidi |
| 6 Septemba 2016 | Uswidi 1–1 Uholanzi |
| 10 Novemba 2011 | Uswidi 3–2 Uholanzi |
| 12 Oktoba 2010 | Uholanzi 4–1 Uswidi |
| 19 Novemba 2008 | Uholanzi 3–1 Uswidi |
Utabiri Wetu

Netherlands wanaingia katika mchezo huu wakiwa na presha kubwa zaidi. Ikiwa watapoteza pointi kwa mara ya pili mfululizo, wanaweza kuweka matumaini yao ya kufuzu hatua ya mtoano katika hatari kubwa. Hata hivyo, Sweden nao watakuwa na morali kubwa. Timu zote mbili zina uwezo mkubwa wa kufunga mabao, na kwa tathimini hii tunatabiri mechi itakuwa na magoli kwa timu zote (Both team to score).
Jinsi ya Kubashiri na SportPesa
1. Fungua ukurasa wa mechi ya Netherlands vs Sweden kwenye SportPesa.
2. Chagua aina ya masoko unayotaka kuweka dau lako – Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB)
3. Weka kiasi cha dau lako na uthibitishe.
Kuangalia uchambuzi wa mechi ijayo ya USA, soma hii: USA vs Australia Kombe la Dunia 2026: prediction, Live score, lineups, vikosi, h2h, live score, odds
Hitimisho
Utabiri wetu wa kiuhariri unaipa nafasi kubwa mechi kuwa na matokeo ya magoli kutoka pande zote mbili, hii ni kutokana na tathmini ya ubora wa vikosi na na kimbinu. Japo kwa ujumla mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Netherlands vs Sweden kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator
Kufahamu utabiri na uchambuzi wa mechi inayofuata ya South Africa, soma hii: Brazil vs Haiti FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, prediction, h2h
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ)

Je, mchezo kati ya Netherlands vs Sweden unaanza saa ngapi?
Mchezo unaanza saa 2 usiku tarehe 20 June 2026, katika Uwanja wa NRG, Houston, Texas, Marekani.
Nini kilitokea kwenye mchezo wa kwanza wa Netherlands kwenye Kombe la Dunia 2026?
Uholanzi walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Japan katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi F, licha ya kuongoza mara mbili. Virgil van Dijk na Crysencio Summerville walifunga mabao kwa Uholanzi.
Nini kilitokea kwenye mchezo wa kwanza wa Sweden kwenye Kombe la Dunia 2026?
Sweden waliifunga Tunisia 5-1 katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi F. Yasin Ayari alifunga magoli 2, huku Viktor Gyökeres na Alexander Isak pia wakifunga mabao. Ilikuwa mojawapo ya ushindi mkubwa zaidi wa siku ya kwanza ya mashindano.
Rekodi ya Netherlands vs Sweden ni ipi?
Uholanzi wanaongoza kwa rekodi ya hivi karibuni, wakiwa wameshinda mechi tatu kati ya tano za mwisho. Mchezo wao wa mwisho ulikuwa ushindi wa 2-0 kwa Uholanzi Oktoba 2017. Ushindi wa mwisho wa Uswidi dhidi ya Uholanzi ulikuwa 3-2 Novemba 2011.
Netherlands vs Sweden wako kundi gani kwenye Kombe la Dunia 2026?
Timu zote mbili ziko Kundi F pamoja na Japan na Tunisia. Baada ya mchezo wa kwanza, Uswidi wanaongoza kwa pointi 3, wakati Japan na Uholanzi wote wana pointi 1.
Wachezaji muhimu wa Netherland kwenye Kombe la Dunia 2026 ni akina nani?
Nahodha Virgil van Dijk anaiongoza timu na alifunga dhidi ya Japan. Memphis Depay, mfungaji bora wa muda wote wa Uholanzi, anatarajiwa kuanza. Cody Gakpo anaongoza safu ya ushambuliaji. Frenkie de Jong na Ryan Gravenberch wanadhibiti kiungo cha kati.
Wachezaji muhimu wa Sweden kwenye Kombe la Dunia 2026 ni akina nani?
Viktor Gyökeres na Alexander Isak wanaunda moja ya michanganyiko hatari zaidi ya washambuliaji kwenye mashindano. Yasin Ayari (Brighton), aliibuka nyota wa kushangaza kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Tunisia katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia.

