Simba SC vs Pamba Jiji FCMpanzu vs Pamba Jiji FC
  • Ni Simba SC vs Pamba Jiji FC NBC Premier League Juni 14, 2026, Uwanja wa KMC Complex.
  • Mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Kirumba ulisoma Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC
  • H2H Simba SC imepata ushindi kwenye mechi 2 na sare 1

Ni Simba SC vs Pamba Jiji FC NBC Premier League Juni 14, 2026 ni ratiba inayofuata mzunguko wa pili. Mnyama amekutana mara moja na Pamba Jiji FC ndani ya ligi walipofungana 1-1. Wababe hawa wanatarajiwa kukutana Jumapili 16:00 UTC.

SOMA HII: Ratiba ya Simba SC mwezi huu wa 6, 2026 | Ligi Kuu NBC na CRDB Federation Cup, Takwimu |Mechi 6 za kufa na kupona | SportPesa Blog

Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Kivumbi cha Simba SC vs Pamba Jiji FC kupigwa KMC Complex

Simba SC vs Pamba Jiji FC
Mpanzu vs Pamba Jiji FC

SOMA HII: Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi | NBC Premier League na CRDB Federation Cup | SportPesa Blog

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Wababe wawili Simba SC vs Pamba Jiji FC kivumbi chao ni Uwanja wa KMC Complex katika mchezo ujao wa ligi. Hii ni vita ya kuwania kutwaa ubingwa na kuwa ndani ya 10 bora. Mnyama yupo nafasi ya pili kwenye msimamo akiwa na pointi 58 huku wapinzani nafasi ya 7 na pointi 33.

Ushindi kwa Simba SC utaongeza nguvu kuzidi kuifukuzia Yanga SC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 60. Ikiwa wageni watapata pointi 3 wataongeza uwezekano kumaliza ligi ndani ya 10. Hii ni mechi kali inayosubiriwa kwa shauku kubwa.

Rekodi ya Mechi za Pamba Jiji FC dhidi ya Simba SC

TareheTimu NyumbaniMatokeoTimu Wageni
19/03/2026Pamba Jiji FC1 – 1Simba SC
08/05/2025Simba SC5 – 1Pamba Jiji FC
22/11/2024Pamba Jiji FC0 – 1Simba SC

Muhtasari wa Takwimu

KipengelePamba Jiji FCSimba SC
Mechi Zilizochezwa33
Ushindi02
Sare11
Kufungwa20
Magoli Yaliyofungwa27
Magoli Yaliyoruhusiwa72

Wachezaji wakuchungwa

Kuelekea mchezo ujao kwa wawili hawa kuna wachezaji wakali wakuchungwa kila timu. Hii inatokana na uwezo walionao uwanjani. Wenyeji chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker wamekuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri, hawa hapa wachezaji muhimu:-

Clatous Chama

Simba SC vs Pamba Jiji FC
Clatous Chama kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

SOMA HII: Pamba Jiji FC waigomea Simba SC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings, goal

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC amekuwa tegemeo eneo la kiungo. Magoli 8 aliyofunga kwenye ligi yanampa nguvu kuwa kwenye mwendelezo bora. Kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC alikosa penalti iliyosababishwa na Ellie Mpanzu.

Mpanzu

Ellie Mpanzu aliandika rekodi kutwaa tuzo ya mchezaji bora dhidi ya Dodoma Jiji FC ikiwa ni mara ya kwanza. Alisababisha penati a alifunga goli. Hivyo ni mchezaji mwenye hatari akiwa uwanjani.

Seleman Mwalimu

Huyu ni mshambuliaji wa Simba SC. Magoli 8 amefunga akiwa ni mshambuliaji pekee ndani ya kikosi cha mnyama. Amekuwa imara zaidi akianzia sub kutokana na mbinu za mwalimu.Je mchezo ujao ataanza kikosi cha kwanza?

Yona Amos

Huyu ni mlinda mlango namba moja wa Pamba Jiji FC.Miongoni mwa nguzo imara kwenye kupambania ulinzi ndani ya lango.Wachezaji wa Simba SC watakuwa na kazi kubwa kupenya kwenye nyavu za kipa huyu ikiwa ataanza langoni kutokana na uwezo alionao.

Mathew Tegisi

Kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kwenye kucheka na nyavu. Wakati ubao wa Kirumba ukisoma Pamba Jiji FC 2-3 Tanzania Prisons alifunga magoli 2. Alifunga goli la ushindi dhidi ya KMC FC, kwenye mechi 2 mfululizo kafunga magoli 3. Huyu anajua kufunga hivyo ana hatari asipochukwa.

Zabona

Uzoefu kwenye ligi unampa nguvu kuwa mhimili ndani ya kikosi cha Pamba Jiji FC. Ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye mechi za ushindani. Kocha Mkuu wa Pamba Jiji Francis Baraza amekuwa akimpa majukumu mara kwa mara uwanjani.

Hitimisho

Burudani inarejea huku Simba SC vs Pamba Jiji FC NBC Premier League ikiwa ni mechi inayotazamiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mnyama anapambania pointi 3 kuwania ubingwa huku Pamba Jiji FC anapigania kuwa 10 bora. Je nani ataibuka mshindi mchezo ujao? Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this: