Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi leo Juni Mosi 2026 kwa maandalizi ya mechi zinazofuata. Mnyama ana mechi 5 za NBC Premier League na mchezo mmoja wa hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup. Uwanja wa Mo Arena umeanza kazi mara baada ya mapumziko ya siku 7. Mchezo uliopita ilikuwa Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC Uwanja wa KMC Complex. Mchezo ujao ni Simba SC vs Pamba Jiji FC.
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi leo Juni Mosi 2026

SOMA HII: Simba SC yajivunia ubora wa kikosi 2025/26 | Fixture, Standings

Baada ya mapumziko muda kuisha kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi leo Juni Mosi 2026. Timu hiyo kwenye ligi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 baada ya mechi 25. Maandalizi yameanza kuelekea mchezo ujao dhidi ya Pamba Jiji FC, Juni 14, 2026.
Kwenye mechi 5 za ligi mnyama atacheza mchezo mmoja saa 8:00 mchana ugenini. Hii ni rekodi mpya kwa msimu wa 2025/26 kucheza mara ya kwanza mchana. Mechi zilizopita ilikuwa ni jioni na usiku.
Ni Juni 18, 2026 itakuwa Mbeya City FC vs Simba SC utapigwa saa 8:00 mchana baada ya mabadiliko kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Baada ya mchezo huo kibarua kingine kitakuwa kwenye CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali vs Coastal Union. Je mnyama atatoboa mchana?
Steve Barker ameanza na wachezaji hawa Mo Simba Arena
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC ameanza kazi na baadhi ya wachezaji ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa. Kwa sasa ligi imesimama kwa muda kupisha mechi za kimataifa ambazo zipo kwenye kalenda ya FIFA. Mpaka Juni 13, 2026 ligi inatarajiwa kurejea.
Miongoni mwa wachezaji ambao wameripoti kambini ni Ellie Mpanzu mfungaji wa goli la ushindi mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC. Duchu, Inno Loemba, Morice Abraham ambaye ni kiungo mshambuliaji.Yusuph Kagoma huyu ni kiungo mkabaji. Rushine De Reuck ambaye ni beki chaguo la kwanza yupo kambini.
Neno la Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC

“Baada ya mapumziko kukamilika sasa wachezaji wanarejea kambini rasmi kwa maandalizi ya mechi zinazofuata. Wale ambao wapo kwenye majukumu ya taifa hao wataendelea na kazi huko walipo. Lakini wengine waliokuwa Canada, Msumbiji, Dubai wamerejea na kuanza program chini ya benchi la ufundi.
“Tunahitaji kukamilisha msimu kwa mafanikio kwenye mechi ambazo zimebaki. Kikubwa ni maandalizi mazuri na hilo linawezekana tukianzia Uwanja wa Mo Simba Arena.Kuna mechi za CRDB Federation Cup na NBC Premier League hizi zote ni muhimu kwetu,” amesema Ahmed.
Mchezo ujao ni Simba SC vs Pamba Jiji FC, Juni 14, 2026 Uwanja wa KMC Complex
Kwa mujibu wa ratiba mchezo unaofuata ni Simba SC vs Pamba Jiji FC, Juni 14, 2026 NBC Premier League. Huu unakuwa mchezo wa mzunguko wa pili. Walipokutana mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Pamba Jiji FC 0-0 Simba SC, wababe hawa waligawana pointi mojamoja.
Ratiba ya mechi zijazo Simba SC NBC Premier League
| 14 Juni 2026 | Simba SC vs Pamba Jiji FC | KMC Complex |
| 18 Juni 2026 | Mbeya City vs Simba SC | Sokoine, Mbeya |
| 24 Juni 2026 | Mtibwa Sugar vs Simba SC | Jamhuri |
| 27 Juni 2026 | Simba SC vs Singida Black Stars | KMC Complex |
| 30 Juni 2026 | Simba SC vs KMC | KMC Complex |
Hitimisho
Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi ikiwa ni maandalizi ya mechi za kuhitimisha msimu wa 2025/26. Mnyama baada ya kumalizana na Coastal Union kwenye ligi atakutana naye CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali. Je Simba SC itatinga fainali ama Coastal Union? Kwa taarifa za hivi punde na matokeo endelea kufuatilia SportPesa Blog.

