- Coastal Union vs Simba SC ni mechi kali ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), itakayopigwa kesho Alhamisi 21/5/2026.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani kuanzia majira ya saa 12:30 jioni.
- Mechi ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa Aprili 2, 2026 ambapo matokeo yalikuwa Simba SC 2-0 Coastal Union.
- Makala hii inakuletea dondoo muhimu za mchezo huo.
Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), itaendelea tena kesho Alhamisi 21/5/2026 kwa michezo kadhaa, huku Coastal Union vs Simba SC ukiwa mchezo mkubwa zaidi. Mechi hii inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani kuanzia saa 12:30 jioni. Mechi ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa Aprili 2, 2026 ambapo matokeo yalikuwa Simba SC 2-0 Coastal Union. Makala hii inakuletea dondoo muhimu za mchezo huo.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Coastal Union vs Simba SC h2h

Timu hizi zimekutana katika mechi 24 za ushindani, ambapo Simba SC wameshinda mechi 17, na Coastal Union wakiibuka na ushindi kwenye mechi moja tu. Mechi 6 katika mikutano yao ziliisha bila kupatikana mbabe. Historia mpya itaandikwa kesho kwa kuendana na matokeo. Jedwali hili linaeleza takwimu hizo;
| Tarehe | Mashindano | Timu ya Nyumbani | Matokeo | Timu ya Ugenini |
|---|---|---|---|---|
| 2 Aprili 2026 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba SC | 2-0 | Coastal Union |
| 1 Machi 2025 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Coastal Union | 0-3 | Simba SC |
| 4 Oktoba 2024 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba SC | 2-2 | Coastal Union |
| 9 Machi 2024 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Coastal Union | 1-2 | Simba SC |
| 21 Septemba 2023 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba SC | 3-0 | Coastal Union |
| 9 Juni 2023 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba SC | 3-1 | Coastal Union |
| 3 Desemba 2022 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Coastal Union | 0-3 | Simba SC |
| 7 Aprili 2022 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Coastal Union | 1-2 | Simba SC |
SOMA HII PIA: Taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union (2-0) | Highlights, msimamo, h2h | Clatous Chama
Coastal Union, Simba SC wanasemaje?
Simba SC

Akizungumzia mchezo huo, Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker Ally amesema: “Maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu kati yetu dhidi ya Coastal Union yanaendelea. Wachezaji wameandaliwa kisaikolojia zaidi na kimwili, kuhakikisha wanacheza katika ubora utakaotupatia matokeo ya ushindi. Tuna kazi ngumu ya uhakikisha tunapata ushindi ili kulinda ‘gap’ la alama mbili tulizoachwa na Yanga SC.
“Haitakuwa kazi rahisi kwani Point hizo mbili, zinashikiliwa na timu bora, na yenye uzoefu wa kukaa kileleni. Kingine sio rahisi kucheza dhidi ya Coastal Union hasa ikiwa nyumbani kwake, lakini tuna ari ya kuutaka ushindi kwenye mechi hii. Tunawaomba mashabiki zetu wajitokeze kutupa nguvu.”
Kwaniaba ya wachezaji wenzake, beki wa Simba David Kameta ‘Duchu’ amesema: “Kila mchezaji yupo sawa kwa ajili ya mchezo huu, tunafahamu hautakuwa mchezo rahisi lakini tutapambana.”
SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Coastal Union 02/4/2026: Live score, h2h, vikosi, ratiba, utabiri wa matokeo na Habari za timu
Coastal Union

Naye kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias amesema: “Tunacheza nyumbani, hivyo lengo letu ni kupata matokeo na kuendelea hatua inayofuata. Tumefanya maandailzi ya kutosha ya mchezo huu, tunatarajia mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tutapambana kupata matokeo.
“Kesho ndio siku ya kuthibitisha kwamba Coastal Union inataka kuendeleza makali yake. Tumewasoma wapinzani na tunajua jinsi gani ya kupanga mbinu zetu. Tunawaita mashabiki wajitokeze kwa wingi.”
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Geofrey Manyasi anasema mechi ya kesho inakwenda kuwa nzuri kwao.
Hitimisho

Coastal Union vs Simba SC ni vita ngumu licha ya rekodi kuonyesha Simba SC, wamekuwa na matokeo bora dhidi ya mpinzani wao. Mechi ya kesho Jumapili inatarajiwa kuwa ngumu pia, kwakuwa timu zote mbili zina wachezaji bora. lakini ni wazi kasi ya Simba SC kwenye michezo kadhaa iliyopita inawaongezea ari n nafasi ya kuibuka na ushindi.
SOMA HII PIA: Mzizima Dabi yaiachia maumivu Simba SC 2025/26 | Highlights, msimamo, h2h, ratiba mechi zijazo

