- FT: Simba SC 2-0 Coastal Union, magoli ya Seleman Mwalimu na Ismail Traore, Aprili 2,2026
- Taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union, (2-0), Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.
- Ahmed Ally amwaga cheche akibainisha mashaka waliyokuwa nayo kuwakabili wapinzani wao
- Usajili wa Clatous Chama akitokea Singida Black Stars umeongeza nguvu eneo la kiungo
Taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union (2-0) mchezo wa NBC Premier League Aprili 2, 2026. Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili kwa kuwashusha Azam FC. Magoli ya Simba SC Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo yalifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 25 na Ismail Traore dakika ya 45+3.
SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo, Takwimu na historia
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union (2-0)

Hii ni taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union (2-0). Uongozi wa mnyama umebainisha kwamba ulikuwa na mashakamashaka kuwakabili wapinzani wao. Hii inatokana na matokeo ya mzunguko wa kwanza 2024/25 ubao kusoma 2-2.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliongeza kuwa wapinzani wao wana timu imara. Licha ya kupata matokeo walitumia ubora wa wachezaji kushinda. Aida amewaomba mashabiki kuendeleza mshikamano.
Ahmed Ally amwaga cheche

“Tumepata ushindi mbele ya Coastal Union lakini tulikuwa na mashakamashaka. Hii inatokana na ubora wa mpinzani wetu. Tunakumbuka msimu uliopita tulianza kuongoza kwa magoli mawili na mwisho ilikuwa 2-2. Mashabiki wazidi kuwa nasi kila wakati,”.
Takwimu Simba SC 2-0 Coastal Union
| Simba SC | Coastal Union | |
| 14 | Mashuti | 3 |
| 6 | Lenga lango | 2 |
| 52% | Umiliki | 48% |
| 8 | Mashuti yasiyolenga lango | 1 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 1 | Kadi ya njano | 2 |
| 8 | Kona | 1 |
| 2 | Magoli | 0 |
SOMA HII: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi

Msimamo wa NBC Premier League
Tazama msimamo mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26. Jedwali hili linaonyesha takwimu za mechi na nafasi. Mabingwa watetezi ni Yanga SC.
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| Yanga SC | 16 | 11 | 5 | 0 | 38 |
| Simba SC | 15 | 10 | 4 | 1 | 34 |
| 3. Azam FC | 16 | 8 | 8 | 0 | 32 |
| 4. JKT Tanzania | 17 | 7 | 7 | 3 | 28 |
| 5.Pamba Jiji FC | 16 | 6 | 7 | 3 | 25 |
| 6.Singida Black Stars | 16 | 7 | 4 | 5 | 25 |
| 7.Mtibwa Sugar | 17 | 5 | 7 | 5 | 22 |
| 8.Namungo FC | 17 | 5 | 6 | 6 | 21 |
| 9.Dodoma Jiji FC | 17 | 5 | 6 | 6 | 21 |
| 10.TRA United SC | 16 | 5 | 5 | 6 | 20 |
| 11.Mashujaa FC | 17 | 4 | 7 | 6 | 19 |
| 12.Fountain Gate FC | 16 | 4 | 4 | 8 | 16 |
| 13.Coastal Union | 17 | 3 | 6 | 8 | 15 |
| 14.Mbeya City | 16 | 3 | 4 | 9 | 13 |
| 15.Tanzania Prisons | 17 | 3 | 4 | 10 | 13 |
| 16. KMC FC | 16 | 2 | 2 | 12 | 8 |
SOMA HII: NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili | Azam FC vs Simba SC | Yanga SC vs Prisons | Msimamo

H2H Simba SC vs Coastal Union
02/04/2026, Simba SC 2-0 Coastal Union
01/03/2025, Coastal Union 0-3 Simba SC
04/10/2024, Simba SC 2-2 Coastal Union
09/03/2024, Coastal Union 1-2 Simba SC
21/09/2023, Simba SC 3-0 Coastal Union
09/06/2023, Simba SC 3-1 Coastal Union
03/12/2022, Coastal Union 0-3 Simba SC
07/04/2022, Coastal Union 1-2 Simba SC
31/10/2021, Simba SC 0-0 Coastal Union
11/07/2021, Simba SC 2-0 Coastal Union
21/11/2020, Coastal Union 0-7 Simba SC
Usajili wa Clatous Chama umeongeza nguvu

Usajili wa Clatous Chama kutoka Singida Black Stars umeongeza nguvu eneo la kiungo. Raia huyo wa Zambia mwenye miaka 34 alihusika katika goli la kwanza kwa kutoa asisti. Goli la pili ni Neo Maema ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Chama anauhakika wa namba chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker raia wa Afrika Kusini.
SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito

Mechi zijazo kwa Simba SC NBC Premier League
Azam FC vs Simba SC, Aprili 5,2026 saa 1:00 usiku
Fountain Gate FC vs Simba SC, Aprili 9, 2026, saa 10:00 jioni
Namungo FC vs Simba SC, Aprili 15,2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs JKT Tanzania, Aprili 19,2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs Tanzania Prisons, Aprili 29, 2026 saa 1:00 usiku
Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2026 saa 11:00 jioni.
Mashujaa FC vs Simba SC, saa 12:15, jioni.
Coastal Union vs Simba SC, Mei 16,2026 saa 10:00 jioni
Simba SC vs Dodoma Jiji FC, Mei 20,2026, saa 1:00 usiku.
Hitimisho
Taarifa mpya baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Coastal Union (2-0). Mnyama anapanda kwa nafasi moja kwenye msimamo. Pointi 4 bado kumfikia kinara wa ligi ambaye ni Yanga SC mwenye pointi 38.

